Tundu Lissu anawatisha nini CCM?

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,459
2,000
Hiki kiwewe cha CCM dhidi ya Tundu Lisu kinatokana na nini hasa? Aliposema kwamba anagombea Urais wa TLS timu nzima ya CCM kuanzia Mwenyekiti wao wa taifa ikawehuka. Wengine tukajiuliza kwani TLS imeanza wakati Lissu anatangaza kugombea huo Urais wa TLS?

Wakati wa kupitisha Mswada wa Sheria ya Habari tulishuhudia bunge likiendeshwa hadi usiku sana huku wabunge wa CCM kama vile walikuwa wamejifunga kibwebwe dhidi ya Lissu. Hadi wengine tukapata hofu kwamba labda huenda Lissu anamiliki chombo cha habari ambacho sheria husika ikipitishwa basi serikali itafaidika kwa kukifuta chombo hicho.

Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 inasemwa kwamba Jakaya Kikwete alipata kusema ni heri watu wa Jimbo la Lissu wasimchague yeye kuwa Rais lakini pia wasimchague na Lissu kuwa Mbunge. Hapa tena tukasema inakuwaje mtu anayetaka kuwa Rais anaona ni bora mgombea wa chama chake ashinde ubunge lakini yeye pia asipewe kura na hao hao anaoomba wamchague mgombea wake ubunge!? Kisa Lissu!

Kwa nini Jeshi zima la CCM huamia kwenye mapambano na Lissu kwenye kila jambo analolisimamia? Wakati Lissu anawatetea watu wa Bhulyankulu dhidi ya wachimbaji wawekezaji, CCM nzima ilikuwa kinyume chake. Leo wanadai anaogopa kesi wakati hajawahi kukosa kuhudhuria hata zile kesi wanazomzushia kila uchao.

CCM kwa nini inapagawa kwenye mambo mengi sana anayoyafanya Lissu?
 

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,459
2,000
Sijawahi Kuona Mwanasheria Bogus kama Tobo Lissu!
Iwavyo vyovyote vile kama ni Tobo ama Tundu Lissu, hoja hapa ni wakati gani Lissu aliwahi kawatetea wezi wa Rasirimali zetu? Tatizo viongozi wa CCM roho huwa haziwaumi kwa kuwa fedha zinazotumika kulipa hizo fidia huwa hazitoki kwenye mifuko yao bali huwa zinatoka kwenye hazina ya nchi yetu inayojazwa na kodi toka kwa wananchi maskini!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom