Acha wivu ndugu yangu.hakuna jipya hapo watu wanakusanyika hapo kwa wingi sio kwa kusikiliza sera zenu wengine wapo hapo kutafuta wachumba wangine kuiba na wengine kupoteza muda tu cku iende wanawafanya CDM kama wasanii wakuwaburisha mnapokuwa mnatoa hadithi zenu kama za elfu ulelaulela
Kama hujui siasa kaa kimya au uulize tukufundishe na sio kuropoka tu hapa.
Siasa siku zote tena dunia nzima inahitaji WATU, MANENO na HARAKATI.
Kuwepo kwa wingi wa watu kwenye mkutano wa kisiasa ni ISHARA kwamba watu Wamehamasika, Wanashauku, Wamekukubali.
Embu jiulize maswali haya kama umati wa watu hauna maana yoyote kisiasa;
1/Kwanini CCM tukifanya mkutano mahali popote Tz kwa sasa, lazima tubebe watu toka sehemu mbalimbali, tuwalipe posho wananchi, Tuwahonge(kanga, Fulana, Vitenge au Pilau), Tulete wasanii wa Bongo flavour kuburudisha ili kujaza watu?
2/Kwanini CUF mwaka jana aliamua kukodisha mabasi mengi kubeba watu kutoka Dar kwenda kuhudhuria mkutano wao wa hadhara kule Arusha?