Ameongelea mengi si rahisi sana kueleza kwa ufasaha hata kwa dondoo. Hopefully, tutapata hotuba yake baadaye humu na YouTube. Nilimkuta anaendelea but in short, niliyoweza kuyadaka ni kama haya:-
(i) Budget ya Mahakama: Ameichana Serikali kwa kushindwa kutenga budget ya kutosha kwa ajili ya kuendesha shughuli za mhimili wa utoaji haki - Mahakama. Kasema maelfu ya kesi zimerundikana mahakamani kwa ukosefu wa fedha ingawa ilishapendekezwa budget ya mahakama iwe asilimia fulani ya badget ya nchi, Serkali imegoma kufanya hivyo kwa sababu zao. Ametaja, kwa idadi, mlolongo wa kesi zilizorundikana kuanzia mahakama ya Rufaa hadi za Mwanzo - ni malaki ya kesi.
(ii) Uwezo Mdogo wa Majaji: Ameilaumu mamlaka ya uteuzi wa majaji kwa kinachodaiwa kutofuata taratibu katika uteuzi wa majaji hivyo kupatikana kwa baadhi ya majaji wenye uwezo mdogo kiutendaji kuanzia kendesha kesi, kuandaa ripoti za kimahakama, utafiti, na hata uwezo mdogo wa kimombo ambayo ndio lugha rasmi ya kimahakama. Badala yake uteuzi wa baadhi ya majaji unaonekana kama kulipana fadhila ili wahusika wapate marupurupu makubwa wakati wa kustaafu kwani marupurupu ya majaji yameboreshwa sana hivi karibuni.
(iii) Tume ya Katiba: Amesema ni jambo jema kwa wajumbe wa tume kufanya kazi zao katika mazingara bora. Lakini pia haiingii akilini posho za kutisha wanazolipwa kila siku kwa mwaka mzima. Amependekeza, ni bora walipwe mishahara, ikiwezekana mshahara wa juu kabisa nchini still fedha nyingi zitaweza kuokolewa kuliko ilivyo sasa ambapo hakuna maelezo ya wazi. Amesema haiingii akili fedha za walipa kodi kufujwa kiasi hicho lakini linapokuja suala la watumishi wengine kama madaktari, walimu, n.k. kudai maslahi bora wanaambiwa hakuna fedha au wanafunzi wa elimu ya juu wanaambiwa "sungura mdogo".
(iv) Uteuzi wa Wakuu wa Wailaya na Mikoa: Hii amesema imekuwa kulipana fadhila miongoni mwa wana-CCM kutokana na sababu mbalimbali. Ametoa mifano kadhaa hapa kuthibitisha hilo ikiwemo viti maalumu ambao amesema maelezo yanahitajika kujua kama hakuna muingiliano wa majukumu kati ya mihimili miwili. Pia amehoji wanapokuwa Bungeni majukumu yao yanatekelezwa na nani. Pia amedokeza suala la wanajeshi kuwa wakuu wa wilaya/mikoa ambao ni makada wa CCM kinyume na Katiba ya JMT.
(v) Suala Ulimboka: Ameanza kwa kuoanisha kauli ya "LIWALO NA LIWE" na kutekwa na hatimaye kuteswa kwa Dr. Ulimboka muda mfupi baadaye. Amewataja pia kwa majina watuhumiwa wa utekaji huo na ametaka maelezo ya Serikali.
Sorry! Ameeleza mengi siwezi kuyaandika yote hapa. Tafadhali mwenye hotuba yake atuwekee hapa tafadhali.