Tundu Lissu afunguka bungeni

[anafaQUOTE=Mabulangati;4232671]Hivi hotuba ya kambi ya upinzani inaandaliwa na mtu mmoja mwenye influence anu inaandaliwa na jopo maalumu la kambi ya upinzani? Je Bajeti hiyohiyo inaweza kutumika wakiwa madarakani? Nauliza hivi kwakuwa sijona chochote alichosema Lisu nimesikia makelele yaliyoambatana na nguvu nyingi hadi kaharibu kipasa sauti na meza yenyewe akahamia kwa mwingine. Zaidi ya hapo sijaona kitu kama bajeti ila tu kuishambulia serikali kana kwamba nya kampeni. Kaaaazi kwelikweli.Tunachezewa akili kwa stali ya kipropaganda[/QUOTE]

Mkuu umenikera sana.Nakusikitikia.Hotuba imewekwa hapa na makamanda.Badala ya kubainisha udhaifu wa hotuba,kama unavyoelekea kuamini,wewe unaleta mizaha.Kwa hadhi,heshima na nafasi ya JF,ulipaswa , unapaswa na daima utapaswa kuweka fikra mbadala .Pambanisha hoja.
Nimepuuza mchango wako dhaifu.Liwalo na Liwe.

Hivi magazeti ya Tanzania yanatatizo gani hasa? Au ni ufinyu wa watu kuelewa role ya media? Hivi mbona tunaona sehemu mbalimbali duniani viongozi wakiwajibika kwa yale yaliyoandikwa magazetini? Magazeti ya Tanzania yana nini hasa? Tubadilike bana. Rwanda watu wamekula mvua kwa kile walicho-publish. Such is the power of media. Kama gazeti halisemi ukweli kwanini serikali iendekeze u-ndugai (mpaka sasa sijamwelewa) kupuuza wakati sheria zinazo-govern media zipo? Kumbe basi kuna haja gani ya kusoma magazeti wakati kila kinachoandikwa hakipaswi kuaminiwa? Hebu nissaidieni wadau. Hii ni kero yangu namba moja kati ya kero mbili nilizonazo.

Viongozi wa Serikali ya ccm wanaamini kwamba habari za 'kweli' katika magazeti ni zile zinazowasifia tu. Hata kama sifa hizo ni za kipuuzi.

Tusiwalaumu sana, somo la uwajibikaji walipata sifuri wote.
 
Tuna mtaji wa kura za masikini,wakulima wanawake na wasiosoma. Tuone kama nyinyi mtaingia Ikulu na kura za wanafunzi wa vyuo

Kama kuna makosa makubwa mnayofanya katika chama chenu (ccm) basi ni kufikiri kuwa bado ccm ina ushawishi vijijini. Yawezekana hujawahi kutembelea sehemu kubwa ya Tanzania, mikoani na vijijini. Fanyeni utafiti muone kama bado wananchi wanawaamini.

Ukweli ni kwamba nchi ilishaondoka mikononi mwa ccm tangu 2010, nguvu ya dola ndo imeendelea kuwaweka madarakani. Hata hivyo nayo imeanza kuwaacha.
 
Yes jamaa alizungumza sana akiitaka serikali itoe majibu,niliangalia mwanzo hadi mwisho ,ila huwa najiuliza kuna faida gani kuzungumza kiasi kile ,ni kweli majibu yanapatikana ? Ni kweli baada ya majibu kuna utekelezaji ,ikiwa serikali imeyakubali au haina majibu ni nini faida ipatikanayo pale bungeni ?

Wazo langu ni kuiweka ile risala ya mheshimiwa na kuisoma kwenye mikutano ya hadhara kwa nguvu zaidi na sauti kuu , mbona itakuwa haina wasiwasi na itawagusa wananchi na watazidi kushawishika na kujenga na kuweka matumaini kwa CDM pia itawavutia wale ambao bado hawajaamua waende wapi.

Yale ndio mambo ya kuzungumzwa kwenye mikutano ya hadhara ili kuujulisha umma wa WaTanganyika wapate kubadili muelekeo wa wapi pa kuipeleka kura yao.
 
Hivi wakuu wa mikoa/wilaya ambao pia ni wabunge wanalipwa mishahara yote miwili? Na wanapokuwa bungeni nani anafanya kazi zao mkoani/wilayani? Na kwanini kulundika madaraka kwa mtu mmoja?

Huwa wanatakiwa kuchagua mshahara mmoja aidha wa ubnge au wa ukuu wa mkoa/u-DC
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hawa watu walioko upande wa serikali (AG na Spika), wasitumie Nyundo ya CCM a.k.a Nguvu ya Hoja, kuzima hoja badala yake watumie Hoja ya Nguvu kuuonesha umma kasoro zilizomo katika hotuba ya Lissu.
 
Kama kuna makosa makubwa mnayofanya katika chama chenu (ccm) basi ni kufikiri kuwa bado ccm ina ushawishi vijijini. Yawezekana hujawahi kutembelea sehemu kubwa ya Tanzania, mikoani na vijijini. Fanyeni utafiti muone kama bado wananchi wanawaamini.

Ukweli ni kwamba nchi ilishaondoka mikononi mwa ccm tangu 2010, nguvu ya dola ndo imeendelea kuwaweka madarakani. Hata hivyo nayo imeanza kuwaacha.

Wewe utakuwa haijui Tanzania bora ukaachana nayo kabisa. Dili na siasa za kwenu Uganda si unajiita mtoto wa Mbale bila shaka uko ndio kwenu
 
Sio kosa lako ni mataptap unayofakamia!

Chama Daima Mipasho mnakataa nini we usikii mipasho ya viongozi wenu bungeni na magazetini? Sisi CCM tunafanya kazi kwenda mbele.

Dr Slaa juzi kawaimbia mipasho mara sitokwenda polisi mwenye kajipeleka kama si mipasho ni nini? Bado na nyinyi mle matapishi yake maana yeye keshayala, kazi mnayo mbayuwayu chadema

Kwa bahati mbaya sinywi pombe wala kufuta sigara bora ukaja na hoja inayopinga kuwa CDM sio chama cha mipasho na sio kumzihaki mwenzio. Tena nakuambieni kejeri zenu hazitonikimbiza bali zinanipaka mafuta.
 
Hivi wakuu wa mikoa/wilaya ambao pia ni wabunge wanalipwa mishahara yote miwili? Na wanapokuwa bungeni nani anafanya kazi zao mkoani/wilayani? Na kwanini kulundika madaraka kwa mtu mmoja?
Swali lako ni zuri na la muhimu sana, lakini sio sehemu yake anzisha thread tuchangie ndugu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
afu huyu Mama Stella Matomato ni FUNDI MCHUNDO, the anajiita na majuha magamba wote wanamuita Engineer,pambaf...
 
Tuna mtaji wa kura za masikini,wakulima wanawake na wasiosoma. Tuone kama nyinyi mtaingia Ikulu na kura za wanafunzi wa vyuo
Hao watu unawaongelea wako kimanzichana, msoga, lindi kisiju na utete.
Mtaji mwingine?
 
Hao watu unawaongelea wako kimanzichana, msoga, lindi kisiju na utete.
Mtaji mwingine?

Kama unakumbukumbu za historia ya Tanzania basi utakubaliana nami kuwa ukanda wa pwani ndio ulioanza vuguvugu za kudai uhuru. Huo ukanda wenu wa kaskazini wala haukuwa na mpango wa kudai uhuru nashangaa sasa mnaibuka eti mna uchungu na Tanzania . Usikubali kudanganyika kijana
 
na ndo huo ukanda ndo bado unasubiri kukombolewa.
Ukombozi utawafika sooon.
Mwisho wao wa kunywa minazi kama chai wajongea
 
Back
Top Bottom