Tundu 'Frankenstein' Lissu

Tundu 'Frankenstein' Lissu

..inategemea.

..wako watu waliowahi kupata majeraha vitani na wakatibiwa na kurudi tena vitani.

..hata dereva anaweza kuendesha tena gari bila matatizo. Mimi binafsi niliwahi kupata ajali ya gari kupinduka lakini kesho yake niliendesha gari lingine.

..lakini pia wapo ambao ajali na mikasa hawatia uoga. Kwa mfano yuko bwana mmoja alipata msukosuko ktk helikopta na sasa inasemekana hapendi usafiri wa anga.
[B]JokaKuu[/B], wapo watu wanadhani kaibuka tu wakati huu wa dikteta uchwara...hawafahamu historia ya Lissu na misukosuko aliyopitia hata kabla ya kujiingiza kwenye siasa. Hawafahamu Kikwete alimjulia wapi [B]Tundu Lissu[/B] hadi kufikia kutoa kauli ya heri Dr. Slaa aupate Urais kuliko Mh. Tundu Lissu kuukwaa Ubunge. Wakti anatamka hivyo Mh. Lissu ndio alikuwa anagombea Ubunge kwa mara ya kwanza.

Mkapa alimshughulika Lissu mara nyingi katika utawala wake na wakati huo alikuwa mwanaharakati tu na si Mbunge. Alikamatwa, akaswekwa ndani na akafunguliwa mashtaka lakini Mkapa hakuweza kumnyamazisha Lissu. Kikwete naye alihangaika na Lissu wee lakini mwisho wa siku hakufanikiwa kumnyamazisha Lissu. Wangapi wanakumbuka siku Lissu alipodhalilishwa na Polisi baada ya kuachiwa na Mahakama?

tundu%2Blissu.jpg

Tundu Lissu akionyesha shati lake lilivyochanwa na polisi
baada ya kumpa kichapo akiwa nje ya Mahakama
ya Wilaya ya Tarime, baada ya kupata dhamana.

Waliopanga shambulio kwa Mh. Tundu Lissu walijua njia iko moja tu ya kumnyamazisha nayo ni kumtoa uhai. Leo anatokea limbukeni mwingine anamfananisha na dubwana akijitetea eti alikuwa anatumia tu metaphor, metaphor my foot. Does he even know the meaning of the word? Kuna wengine yawezekana wamesoma lakini kuelimika ni sufuri na ndiyo maana wanakimbilia kutukana hovyo bila haya.

You cannot make an implicit, implied, or hidden comparison between Mh. Tundu Antiphas Lissu and an evil monster unless you have a sick mind!
 
Tatizo ni kwamba hata wakimuua Lissu wataibuka wengine wenye hulka na mrengo kama wake wataendelea kumwendesha bwana mkubwa,historia inatufunza kuwa unaweza kuuwa mtu lakini huwezi kuuwa wazo/idea/itikadi.muda utakuwa hakimu wa hili
 
You cannot make an implicit, implied, or hidden comparison between Mh. Tundu Antiphas Lissu and an evil monster unless you have a sick mind!

Well, I just did and I don't have a sick mind.

The only one sick here is probably you with your Alzheimer's!
 
Well, I just did and I don't have a sick mind.
Would you know it if you had one? Let me tell you something dude, your denial here confirms it. Your reaction proves beyond any doubt that you do have a sick mind.
 
Would you know it if you had one? Let me tell you something dude, your denial here confirms it. Your reaction proves beyond any doubt that you do have a sick mind.
Only one who is sick here is you.

Only two who are in denial are you and your friend JokaKuu.

Go get some help Mr. Curmudgeon.
 
Kwanza kesi alizofunguliwa si kesi uchwara. Ni kesi za kumfunga jela kama mahakama za Tanzania zisingeingiliwa na siasa. Hata serikali yenyewe inaonekana kama ina wasiwasi wa kulaumiwa kufunga wapinzani. Truth be told kuna viongozi wa wapinzani wengi ambao wangekuwa jela saa hizi katika nchi ambazo mahakama zake haziangalii makunyanzi ya uso.

Pili Lissu hakuwa kipenzi cha watanzania wote. Wengi wameweka chuki chini na kumuhurumia kwa misingi ya ubinadamu.

Tatu Lissu sio mwiba kwa CCM tu hata kwa wapinzani. Hasa wale wanaotegemea kupata uraisi. Akiwa unfit kugombea uraisi kuna watakaotoa machozi ya mamba katika wapinzani.

Kabla ya hili tukio umaarufu wa Lissu ulichafuka sana katika suala la bombadia na Acacia.

Akirudi akiendelea na alipoachia atapambana na upinzani ule ule uliofikia kumtoa uzalendo.
 
Zile kamata kamata zisizo na kichwa wala miguu dhidi ya Tundu Lissu na zile kesi uchwara zote zilizofunguliwa dhidi yake naamini ndizo zilizompandisha chati huyo bwana katika huu utawala wa awamu ya tano.

Mara nyingi kama si zote hizo kamata kamata zilitokea baada ya yeye kutoa maneno makali dhidi ya serikali na rais.

Kuna nyakati alikuwa yupo sahihi na nyakati zingine alikuwa mzushi tu. Kwa mfano, aliposema nchi inaendeshwa kwa misingi ya kikabila na kikanda, huo ulikuwa ni uzushi tu. Zilikuwa ni propaganda tu.

Uzushi na propaganda kwenye siasa ni jambo la kawaida sana na la kutegemewa kuwepo. Mwanasiasa asiyezusha, asiyetia chumvi, na asiyepiga propaganda atakuwa kakosea fani.

Sasa mimi naamini hii serikali inafanya makosa sana katika kuwakamata na kuwafungulia mashitaka watu wanaoipinga na kuikosoa. Hizo kesi wanazofunguliwa ni vichekesho mtupu.

Katika kukosea kwao huko, naamini serikali imeunda lidubwana [monster] ambalo kuanzia sasa kwenda mbele itakuwa vigumu kulidhibiti. Lidubwana hili nalifananisha na lile lidubwana la kwenye filamu ya Frankenstein.

Lidubwana hilo ndo Tundu Lissu. Hebu fikiria haya:

Jamaa keshaonyesha kuwa haogopi kuikosoa serikali wala kumsema vibaya rais [mambo ambayo ni ya kawaida sana kwenye demokrasia na ambayo yanahimizwa kufanyika].

Uthubutu na ujasiri wake huo ndo umepelekea yeye kukamatwa kamatwa na kufunguliwa vi kesi uchwara.

Uthubutu na ujasiri huo huo ndo si ajabu umepelekea yeye kushambuliwa kwa risasi kwa lengo la kutaka kumuua. Sijui kwa uhakika ni nani anayehusika na hilo shambulio.

Sasa pata picha atapopona na kurejea tena nchini na kuendelea na harakati zake pale alipoishia!

Serikali itamfanya nini huyu mtu? Wataendelea kumsumbua na hizo kamata kamata zao na kumfungulia hivyo vi kesi uchwara mtu ambaye tayari ana huruma za umma kwa ujumla wake kutokana na yale yaliyomtokea?

Sioni utamkamataje na kumfunga mtu ambaye kanusurika kuuwawa namna ile. Akili yangu inaniambia hata dhamiri yako, kama ni safi, basi itakusuta tu.

Hakika hii serikali ya awamu ya tano ilibugi stepu katika namna ya kumkabili Lissu na sasa amekuwa lidubwana ambaye anaweza asidhibitike tena.

Ni muda tu ndo utaotueleza.....

Katika Maeneo ambayo Mh. Tundu Lissu alipiga propaganda nyepesi ni Kwenye Suala la Ukabila na Ukanda!
JPM hazingatii sana Ukabila na Ukanda.Ingelikuwa hivyo basi nusu ya serikali wangejaa washosha!
 
Naamini Lissu atarudi kuendeleza harakati zake! He was born to do that
 
  • Thanks
Reactions: SDG
BLUE/SAMAWATI: hatokuwa tundu lissu yule ingawa anaweza kujaribujaribu lakini hatokuwa na kujiamini kulikopitiliza....kuna wakati inaweza kutokea akawa anadhani anasikia mlio wa bunduki bungeni na kustuka kumbe ni makofi ya wabunge wenzake ....ondoa hofu kabisa mkuu.

RED/NYEKUNDU: magufuli haonekani kuwa na huruma kama hiyo....akilikoroga atakamatwa kama kawa. mark my words!

KIJANI/GREEN: hiyo ni kweli kwani tiba pekee ya mtu anayekutania ni kukaa kimya na kucheka. kwa kufanya hivyo utakuwa umeliepuka lengo lake la kukukasirisha na hatokuwa na nguvu ya kuendelea sana!!!
Magifuli ana huruma sana,hajamkamata hata waziri au kiongoz yeyote alotutia hasara kwenye madini,ikiwemo yule alokwapua almas ya USD MIL 200.
Na anasema hao wazee muwaache wapumzike
 
Katika Maeneo ambayo Mh. Tundu Lissu alipiga propaganda nyepesi ni Kwenye Suala la Ukabila na Ukanda!
JPM hazingatii sana Ukabila na Ukanda.Ingelikuwa hivyo basi nusu ya serikali wangejaa washosha!

Home first
 
Kikwete mwanasiasa mwenzao ndiyo aliwaweza vizuri tu,alikuwa anawaita ikulu anawapa chai basi mchezo umekwisha.
 
Yake yakianza kubwagwa ataufyata tu.. nafikiri kwake kuna ile kuachiwa na kuangaliwa huku hajui wajuayo.. na hawezi kupata cheo anachotaka hadi wenzake wakubali(ndio maana wanatendeana majanga yanayoendelea kusisukumia kama vile ni serikali). naona ataendelea kupiga mdomo tuuuuu na kuishia alipo.. akitokea kupewa cheo makombora yatarushwa pwaaaaaa..
Kalale mkuu
 
..inategemea.

..wako watu waliowahi kupata majeraha vitani na wakatibiwa na kurudi tena vitani.

..hata dereva anaweza kuendesha tena gari bila matatizo. Mimi binafsi niliwahi kupata ajali ya gari kupinduka lakini kesho yake niliendesha gari lingine.

..lakini pia wapo ambao ajali na mikasa hawatia uoga. Kwa mfano yuko bwana mmoja alipata msukosuko ktk helikopta na sasa inasemekana hapendi usafiri wa anga.
Usilinganishe tukio hili na matukio ya ajali za kawaida za barabarani au angani hata kama ajali hzo huua mamia ya watu kwa mkupuo kila siku.

Hili tukio ni kitu kingine kabisa. Ona Nape alivyoathirika kwa kuoneshwa mtutu tu wa bunduki, tena bunduki yenyewe ni wa ka bastola tu. Nape wa leo si yule tunayemjua. He has completely transformed, sababu si kutimuliwa uwaziri bali kunyooshewa mtutu wa bastola. Nape wa zamani hatunaye tena duniani.
 
Inahitaji HOJA kukabiliana na Lisu, nje ya hapo ni matumizi ya nguvu na mabavu. Aachwe aikosoe serikali, wamjibu kwa hoja.......
 
Ataendesha harakati zake kwenye wheelchair
Hata kama ni kwenye wheelchair the fact remains that you could not implement your evil plans and deeds simply because Mr God did not approve them. So watch out guys
 
Kwanza kabisa huyo jamaa siyo wa kurudi leo wala kesho na hata akirudi kila kitu kwisha habari yake, kuna kiwango cha risaisi ambazo mwili wa Binadamu unaweza kuhimili, kupigwa risasi zote hizo siyo mchezo, huyo kwanza hata akifanya press conf. mtu akibamiza mlango tu kwa bahati mbaya atazimia atafikiri ni hitman wamemjia tena,

Kama ulishawahi kupigwa risasi au hata kukoswa tu unaweza kuelewa ninachomaanisha, hivyo ukiniuliza mimi huyo Tundu Lisu ndiyo basi tena its over, kwani sidhani hata kama ataweza kutembea tena, achilia bali hata tu kuinuka, atabakia jina tu kwa wafuasi wake kama vile Marando &Co., kwa kifupi they fvcked the guy up forever man, whoever shut him!
Wapumbavu kabisa!
 
Kama kawaida yako: Prophet of Doom!!
 
Back
Top Bottom