Uchaguzi 2020 Tundu A.M. Lissu: Mgombea Urais wa upinzani machachari zaidi kuwahi kutokea katika chaguzi zote chini ya mfumo wa vyama vingi kurudi 1992


..Tundu Lissu siyo mwanasiasa.

..He is a Human Rights activist who happened to be a lawyer and a legislator.

..Hicho ndicho kitu ambacho watu wengi wanao-deal na Tundu Lissu hawakielewi.

..Mtu wa namna hiyo siyo rahisi kumkuta ana makando-kando yanayowaandama wanasiasa.

..Pia siyo rahisi kushindana naye kwasababu harakati za kupigania haki ni kama WITO wa maisha yake.

..Wanaoweza kushindana na Tundu Lissu ni wanaharakati wenzake wa haki za binadamu na utawala wa sheria.
 
Hakika tupongeze vyama vya upinzani na wale wote walioshiriki kuimarisha upinzani tangu 1992 bila kuterereka, Bila kusahau viongozi wa chama kimoja kilichokuwepo kukubali hats kama ni kwa shingo upande.Naona kila mwaka wa uchaguzi kuna hatua kubwa inapigwa, na tunaona sura tofauti na bora zaidi kuanzia Mrema hadi sasa kwa Lisu na wengine, Suala la kuwa na vyama mbadala vyenye sera bora kwenye nchi ni jambo la baraka na la afya kwa taifa lolote lenye kiu ya kupata maendeleo ya haraka na dhabiti .Chama tawala kinapokosa mdadala wake huwa na, kiburi ,kujisahau na kuongoza kwa mazoea, huku kikifanya maamuzi bila kufikiri kwa kina matokea yake. Tunatamani kama taifa kila chama kiwe mdadala wa kingine ,hoja na sera zishindanishwe majukwaani , mwisho sisi tuàmue tunaenda na chama gani kwa miaka 5,kisiwepo chama cheñye uhakika wa kushinda %100 kabla uchaguzi
 

Unalenga kutaka kutoa hoja gani hapa Bwana Magembe?

Kwamba, so long as Magufuli professionally (japo profesheni ina utata na kuhojiwa sana) ni mwalimu - mwanasayansi ya korosho na kemia ni mzuri sana kutatua matatizo kama kiongozi?

Hapa binafsi sikubaliani na wewe kwa ushahidi ulio dhahiri kabisa. Labda awe mwanasayansi mwingine....

Lakini kwa John Pombe Magufuli, ni mwanasiasa mwenye taaluma ya sayansi (japo mashaka juu ya taaluma yake ni makubwa) amesha prove failure kote kitaaluma na kiuongozi....!
 
Hongera kwa chapisho. Ushawishi unaendelea ili wengi wamigie kura ya ndio. Binafsi nimeanza kumpenda alivyoshiriki kuandaa ile list of shame! Na pia jina lake ni lake tu
 
Ongezea na hii: ....mgombea urais aliyekuja na nuksi ya kuambulia wabunge 4 tu kwa chama chake na kupata kura kiduchu kuwahi kutokea single digit 7% ya kura za urais!

Ongeza na hii: Mgombea aliyefanikisha kuushawishi umma wa watanzania kujitokeza barabarani nchi nzima kudai matokeo halisi ya kuiondoa CCM rasmi madarakani, huku wapambe njaa wa Jiwe wakidondoka kwa pressure na wengi kukamtwa wakijaribu kutorokea nje ya nchi.
 
na anatoa historia ambazo huwa ni mpya masikioni

sikujua Serengeti ilianzishwa mwaka 1951

sikukujua vita ya ujinga, umaskini na maradhani ilianzishwa mwaka 1958

nimesikia jana Serengeti kwa Tundu Lissu
 
V
Very good analysis.
 
Kha! Kuna mtu jana kaanza style za makonda za kujilizaliza mbele za watu.
 
na anatoa historia ambazo huwa ni mpya masikioni

sikujua Serengeti ilianzishwa mwaka 1951

sikukujua vita ya ujinga, umaskini na maradhani ilianzishwa mwaka 1958

nimesikia jana Serengeti kwa Tundu Lissu
Ukimsikiliza TL unaweza ukaandika Thesisi yako na maprof wakaipitisha bila kipingamizi. Anatoa Elimu nadra sana.
 
24 Sep 2020
Nabii Mwingira Asema Tundu Lissu Ni Miujiza Ya Mungu


Hotuba hii ya Nabii Josephat Mwingira sio tu inaibua tafakuri kuhusu Tundu Lissu alivyosalimika katika jaribio kubwa kabisa dhidi ya uhai wake, lakini sasa sio tu ni mzima bali pia anawania urais 2020 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , bali pia inawezekana kuwa ishara ya awali ya viongozi wa dini waliokuwa karibu na Magufuli "kumkimbia".

Source : chahali media
 
Watu wa namna hii uzaliwa kwa Nadra sana na kwa kusudi maalum.
itapita karne kadhaa kuja kupatikana kichwa kama hiki ndani ya mipaka ya Tanzania.
Waweza kulinganisha na wale marais wa kwanza wa mataifa ya Afrika walio zipigania na kuzikomboa nchi zao kutoka kwa wakoloni
 

Kwani hao kina Magufuli wako wangapi. Hivi angekuwa hakandamizi demokrasia na kufumbia macho watu kutekwa ovyo na kuwaongezea watu mishahara kuimarisha sekta binafsi kwa kupunguza kodi zisizo za lazima na kuacha kuwa katili wakati wa maafa, watanzania si wangekuwa wanamfurahia kila anakoenda. Lakini amechagua kuwaumiza watanzania kwakuwa hakuna cha kumfanya inabidi sasa apambane na hali yake mimi kula yangu kwa Lissu
 
29 September 2020
Karatu, Tanzania

Kampeni za Urais TunduLissu2020 leo mjini Karatu

 
Ongezea na hii: ....mgombea urais aliyekuja na nuksi ya kuambulia wabunge 4 tu kwa chama chake na kupata kura kiduchu kuwahi kutokea single digit 7% ya kura za urais!
Mzee baba kwani kura zimeshapigwa na matokeo kutangazwa?😂😂😂
Eti ongezea na hili... Yaani hata kama ni utabiri, umefeli kabisa maana umeshindwa kuhusisha yaliyopita na yaliyopo kupredict yajayo😉
 
29 September 2020
Makuyuni Arusha,
Tanzania

Tundu Lissu azidi kutoa elimu ya uchaguzi ulio Haki na Huru kwa polisi
 
Ukimsikiliza TL unaweza ukaandika Thesisi yako na maprof wakaipitisha bila kipingamizi. Anatoa Elimu nadra sana.

sikujua kabisa kwamba muswada wa matumizi ya sent tano ya serikali ni lazima kwanza upigwe saini na Rais!

yani huwezi kupata kisima cha maji popote nchini cha hela ya kodi bila pendekezo la Rais!
 
sikujua kabisa kwamba muswada wa matumizi ya sent tano ya serikali ni lazima kwanza upigwe saini na Rais!

yani huwezi kupata kisima cha maji popote nchini hela ya kodi bila pendekezo la Rais!
Ndio Maana anasema ukichagua upinzani hupati hata bomba la maji
 
Toka kuanza kwa utaratibu wa vyama vingi mnamo mwaka 1995 Tanzania haijawahi kupata candidate wa uraisi mwenye uwezo mkubwa wa kiakili na maono kama Tundu Lissu. Tukiwa nchi yenye kuchagua candidate na sera za chama CHADEMA ndio direction. Mwalimu wa chemistry Vs Mwanasheria Nguli haiwezi kuwa discussion
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…