~*~ Tunawaudhi ~*~

kama wewe ni muislam huwa unakwenda msikitini kufanya nini wakati Quran imeandikwa zaidi ya miaka 1500 iliyopita kuna jipya kwenye Quran? Na kama wewe ni Mkristo huwa unakwenda Kanisani kufanya nini wakati yesu alishapaa kwenda mbinguni zaidi ya miaka 2000 iliyopita, lipi jipya unalolifuata au kulitafuta kanisani? Tuache unafiki kila maslahi ya mafisadi yanapoguswa kwa kujifanya hakuna "jipya!

is it even worth it me answering you ? NO, it aint !
 
Kuna wanufaika wa ufisadi humu, hivyo tegemea lolote la kuspeculate kutoka kwao.....
 
Kuna wanufaika wa ufisadi humu, hivyo tegemea lolote la kuspeculate kutoka kwao.....

kama wapo, basi nao ni mafisadi vile vile.... Mzee Msanii nafikiri ukianza kuwataja itakuwa vizuri sana kwa taifa ili tuone hiyo link inaanza wapi na kuishia wapi, kuanzia kwa wanaochezesha huo ufisadi hadi kwa hao wanaonufaika nao.!

Shukrani !
 
kwi kwi kwi,

huyu kweli ni bi saddam husein.
Mkuu umewakomesha hadi wametokomea kabisa?

nimeipenda signature yao "tumpe kikwete hadi 2010 asafishe chama! kweli ukistaajabu ya firauni utaona ya Joji Kichaka, hivi hcho chama kinawahusu nini watanzania wasio wanachama wake? kwa nini asisafishe serikali yake iliyojaa mafisadi? Yesu Kristo aliwahi kusema "Mtawatambua kwa matendo yao"
 
Ndiyo Tunawaudhi!!

Wanakaa chini na kujiuliza kwanini tunawafuata fuata! Wanakereka tunapoandika na kuwajadili na wanaona tunawaandama pasipo sababu ya msingi. Wanachukia na wangekuwa na uwezo wangesha tubamiza kama mtu anavyobamiza nzi ukutani!

Tumekuwa kwao kero isiyokoma, wasumbufu waliotumwa, na watu wenye wivu na maendeleo "yao". Wanakasirika na kununa, wanachukia na kuchukizwa! Tukipita wanatema mate pembeni, na tukiwasalimia hadharani wananyosha mkono kibahili! Wameudhika!!

Tumewaudhi kwa sababu suala la EPA lilitakiwa limalizwe kimya kimya, na sakata la Richmond lilikuwa limeshatolewa "maelezo". Tumewaudhi kwa sababu suala la Kiwira linamhusu "Rais Mstaafu" ambaye tuliambiewa tumuache "mzee wetu astaafu kwa amani". Wameudhika, na tena wamekereka.

Tumewaudhi kwa sababu tumeenndelea kuwahoji hata baada ya kuambiwa mtu kafa; Na tunaendelea kuwaudhi kwa sababu inaonekana tumekuwa watukutu tusiosikia, hatuelewi majibu yao na zaidi ya yote tumekuwa kama luba tumewang'ang'ania kwenye miguu yao ikimbiliayo maovu na ifanyayo haraka kuharibu!

Ndugu zangu, tumewaudhi na tunaendelea kuwakera; wakikaa ofisini kusaini mikataba mipya wanafikiria mara mbili sasa; wakitangaza tenda wanaulizana kama kuna maslahi binafsi yaliyofichwa; Wamebaki wenyewe kushukiana na kuhisiana ubaya na sasa wanazungukana kama watoto wanaocheza "kioo kioo"! Ajulikani nani hasa kakivunja! Wamebakia kuulizana huku wengine wamejificha "tiari bado"?!

Ndio wanakerwa na uwepo wetu, wanachukizwa na uthubutu wetu, wangelikuwa na uwezo kama wa paka kumrukia panya wangedaka mawazo yetu, kuyararua na kuyaweka kiporo ili wayachezee kesho yake! Wangekuwa na uwezo wangetukwapua kama kinyonga akwapuavyo vipepeo na kutubamiza kwenye ndimi zao za moto, na kufumba vinywa vyao kwa ghafla kama mamba wafanyavyo pembezoni mwa Rufiji!

Wanajiuliza kwanini tunawafuatafuata, kwanini hatuwaachi wafanye "kazi", kwanini tunafuatilia matendo na maneno yao wakati wao ndio "viongozi"? Wanashangaa kwanini wakisema mambo ya "vijisenti" kauli zao zinakuzwa kama kwa baragumu! Hawaelewi, wamebakia kuchukizwa na kukerwa!

Ndiposa, sisi sote tunaitwa kufanya uamuzi; aidha kusalimu amri na kuwaacha wapumue kidogo? au kukaza uzi ule ule. Tuna uamuzi wa kukubali maelezo yao ya juu juu au kuendelea kuwachimba kwa maswali ya ziada; tuna uamuzi wa aidha kuwaonea huruma kwa sababu familia zao na jamaa zao wamefadhaishwa na kufedheheshwa au kuendelea kwa sababu kwa maamuzi yao wametufadhaisha na kutufedhehesha sisi kama taifa! Tukubali majibu yao ya awali na turidhike?

Tunaitwa kufanya uamuzi; kujipanga mstari na kupiga makofi na kuwaimbia nyimbo za shangwe au kukaa kimya na kusubiri tuone wanachofanya nini ili tuamue sawasawa. Tunaitwa kufanya uamuzi wa kukubali kutawaliwa nao jinsi wapendavyo, au kuwalazimisha kutambua tunavyopenda kutawaliwa nao! Yes! Tunaoumauzi pia wa hata kuamua kama tunataka waendelee kututawala tena au hii ndiyo iwe ngwe ya mwisho kwao!

Kama wewe ni Mtanzania na mzalendo wa kweli, bila kujali hali yako ya maisha, elimu yako au nafasi yako ya kisiasa na kijamii, bila kujali kama wewe ni mfurukutwa au mkeretwa, bila kujali kama unafuata mrengo wa kulia au wa kushoto au kama itikadi yako ni ya kijamaa au ya kibepari; kama kweli una mapenzi na taifa lako, kama kweli unataka Tanzania ije kusimama kama Taifa la watu walio huru kweli na sawa; Taifa ambalo ndani yake kila mmoja ana nafasi sawa ya kufanikiwa; Taifa ambalo ndani yake wana na mabinti wake wanaona fahari kulitumikia na siyo kulitumia, kuliendeleza na sio kulitelekeza, kuliinua na siyo kulifumua! Taifa la kisasa, Taifa la Kiafrika, na Taifa ambalo kwa mafanikio na fahari litasimama katika jamii ya Mataifa ya ulimwengu!

Basi tunaitwa kufanya uamuzi, na uamuzi huo kwa hakika utakuwa ni wa kuwaudhi na kuwakera watu fulani fulani. Je uko tayari kuwaudhi mafisadi? Je uko tayari kuwakera waliokwiba fedha za Taifa letu? Je uko tayari kuwasumbua usiku kucha waliobaka raslimali za Taifa letu huku wanatuchekelea na kujilamba vinywa vyao huku wakipangusa ala zao?

Najua mimi niko tayari! sijui wewe.. lakini huko tunakokwenda, ni wale walio tayari kusimama peke yao na pweke ndio wataliinua Taifa letu na kulifanya liwe jinsi ile tulitamanivyo liwe! Stand up and be counted otherwise sit down and be forgotten!
Sawa mkuu.Maudhui yanatiririka vizuri, ila nadhani tunyooshe lugha sehemu ndogo sana kuhusu neno "aidha".Wataalamu wa BAKITA watusaidie.Neno hili lina maana ya "vilevile" au "pia";sio kama kwenye kiingereza ...either...or...
Sisi tuseme,"ama......au....."
 
sijakebehi, ila ninachosema ni kwamba, yooote aliyogusia HAMNA JIPYA, na kama unaandika kitu basi lazima uwe AIM ya kuandika, hadi hivi sasa sijaona chochote kipya, na kama solutions nadhani zilishatolewa before katika threads husika !

asante !

Kada Mpinzani na wewe ni CHARACTER NGUMU KIKWELIKWELI, hongera kwa kusimama kama usimamavyo
 
me i think tunawafurahisha sana ndo maana hawajachukua any necessary step.kinyume na hilo..........THEY WOULD HAVE SILENCED US
 
We are just not doing enough hizi ni sawa na kupiga risasi hewani kumshtua adui au kumwogopesha hakuna kitu 'physical' kilichofanyika na tukafanikiwa ktk kuondoa uharamia huu wa mali zetu. Mi naungana na Geoff kuwa wanatuenjoy wakijua kuwa kelele zetu hazina madhara iwapo tu wkichoose kukaa kimya
 
Dua.. hakuna kitu kibaya kama mazoea. Mazoea ndiyo yaliyotufikisha hapa na kujaribu kubadili mawazo au mwelekeo watu hujikuta wanakabiliwa na changamoto ya kuachana na mazoea. Kwa wengine hilo ni unthinkable. Wanataka tufanye mambo vile vile na ni wepesi kukebehi ukweli hata ukiwakodolea macho.

Lakini yote ni sehemu ya mapambano ya fikra ambayo mwanzo wake ni kujiamini. Watanzania pole pole wameanza kujiamini na kutambua kuwa Taifa hili si la watu wachache (kama alivyosema mama Malecela) na ya kuwa kikundi cha watu wachache hawawezi hata kidogo kumiliki nchi nzima kana kwamba wanamshikia mtoto kitu halafu wanammegea kidogo kidogo.

Hivyo mawazo yanayotolewa na jamii kama JF, vyombo vya habari, taasisi huru na mashirika binafsi vimeanza kuwa kero. Na sasa tumefikia mahali mstari unaanza kuchorwa vizuri kabisa kati ya serikali na CCM kiasi kwamba CCM kama chama kimeanza kugawanyika ndani kwa ndani huku serikali ikijaribu kwa kila namna kutafuta nafasi yake katika Tanzania yetu mpya.

Haya ni mabadiliko ya lazima. Hivyo hata wale ambao wanachaguliwa au kuteuliwa kushika nafasi yoyote sasa wanajikuta wanapokea kwa wasiwasi kwa sababu wanajua darubini za watanzania na kurunzi zao zimeelekezwa kwao.

Inaelekea mimi na wewe tupo jukwaa moja ila nipo behind you for almost 2 years
 
nothing new ! yooooote yameongelewa kwenye threads lukuki humu, whats new ? NOTHING.... sasa propaganda kama kawaida ! haya wazee msifieni saddam hussein huyoooooooooooooo.....anakuja ! muimbieni nyimbo nzuri nzuri na mumtupie maua ili afurahi !

Nadhani hauko tayari kama sikosei ni moja ya watu ambao WANAUDHIKA.
 
ndio nipe info zote ! NIHAKIKISHE ! pesa yako ya box sina haja nayo ! lete ma-info hayo watu tumeki shua kama unalipa kodi, kama hulipi basi argument yako mdebwedo !

usiponipa hizo namba/info NAWE FISADI PIA !

We jamaa una matatizi hivi wote humu wapo ughaibuni? mbona mimi nipo Bongo? nsio mimi tu nazani wengi tupo bongo pia, Hivi unajua maana ya VAT? na kama unajua VAT kweli kuna mtu asiye lipa kodi nchi hii?
 
hii ina tofauti gani na mada uliyoandika wewe ?? kubali tu yote maisha, umetoa mada ya kuwaudhi viongozi lakini wewe ukiudhika basi inakuwa kitaanani,..........ebo, si ndio mada uliyotoa hiyo ! na wewe umeonyesha kuudhika kama mada yako inavyodai na hukujificha !

Sikujua kuwa hi mada inawahusu viongozi? kumbe? mimi nilijua inawahusu MAFISADI. Kumbe MAFISADI = VIONGOZI?
 
Back
Top Bottom