Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,694
- 40,720
Ndiyo Tunawaudhi!!
Wanakaa chini na kujiuliza kwanini tunawafuata fuata! Wanakereka tunapoandika na kuwajadili na wanaona tunawaandama pasipo sababu ya msingi. Wanachukia na wangekuwa na uwezo wangesha tubamiza kama mtu anavyobamiza nzi ukutani!
Tumekuwa kwao kero isiyokoma, wasumbufu waliotumwa, na watu wenye wivu na maendeleo "yao". Wanakasirika na kununa, wanachukia na kuchukizwa! Tukipita wanatema mate pembeni, na tukiwasalimia hadharani wananyosha mkono kibahili! Wameudhika!!
Tumewaudhi kwa sababu suala la EPA lilitakiwa limalizwe kimya kimya, na sakata la Richmond lilikuwa limeshatolewa "maelezo". Tumewaudhi kwa sababu suala la Kiwira linamhusu "Rais Mstaafu" ambaye tuliambiewa tumuache "mzee wetu astaafu kwa amani". Wameudhika, na tena wamekereka.
Tumewaudhi kwa sababu tumeenndelea kuwahoji hata baada ya kuambiwa mtu kafa; Na tunaendelea kuwaudhi kwa sababu inaonekana tumekuwa watukutu tusiosikia, hatuelewi majibu yao na zaidi ya yote tumekuwa kama luba tumewang'ang'ania kwenye miguu yao ikimbiliayo maovu na ifanyayo haraka kuharibu!
Ndugu zangu, tumewaudhi na tunaendelea kuwakera; wakikaa ofisini kusaini mikataba mipya wanafikiria mara mbili sasa; wakitangaza tenda wanaulizana kama kuna maslahi binafsi yaliyofichwa; Wamebaki wenyewe kushukiana na kuhisiana ubaya na sasa wanazungukana kama watoto wanaocheza "kioo kioo"! Ajulikani nani hasa kakivunja! Wamebakia kuulizana huku wengine wamejificha "tiari bado"?!
Ndio wanakerwa na uwepo wetu, wanachukizwa na uthubutu wetu, wangelikuwa na uwezo kama wa paka kumrukia panya wangedaka mawazo yetu, kuyararua na kuyaweka kiporo ili wayachezee kesho yake! Wangekuwa na uwezo wangetukwapua kama kinyonga akwapuavyo vipepeo na kutubamiza kwenye ndimi zao za moto, na kufumba vinywa vyao kwa ghafla kama mamba wafanyavyo pembezoni mwa Rufiji!
Wanajiuliza kwanini tunawafuatafuata, kwanini hatuwaachi wafanye "kazi", kwanini tunafuatilia matendo na maneno yao wakati wao ndio "viongozi"? Wanashangaa kwanini wakisema mambo ya "vijisenti" kauli zao zinakuzwa kama kwa baragumu! Hawaelewi, wamebakia kuchukizwa na kukerwa!
Ndiposa, sisi sote tunaitwa kufanya uamuzi; aidha kusalimu amri na kuwaacha wapumue kidogo? au kukaza uzi ule ule. Tuna uamuzi wa kukubali maelezo yao ya juu juu au kuendelea kuwachimba kwa maswali ya ziada; tuna uamuzi wa aidha kuwaonea huruma kwa sababu familia zao na jamaa zao wamefadhaishwa na kufedheheshwa au kuendelea kwa sababu kwa maamuzi yao wametufadhaisha na kutufedhehesha sisi kama taifa! Tukubali majibu yao ya awali na turidhike?
Tunaitwa kufanya uamuzi; kujipanga mstari na kupiga makofi na kuwaimbia nyimbo za shangwe au kukaa kimya na kusubiri tuone wanachofanya nini ili tuamue sawasawa. Tunaitwa kufanya uamuzi wa kukubali kutawaliwa nao jinsi wapendavyo, au kuwalazimisha kutambua tunavyopenda kutawaliwa nao! Yes! Tunaoumauzi pia wa hata kuamua kama tunataka waendelee kututawala tena au hii ndiyo iwe ngwe ya mwisho kwao!
Kama wewe ni Mtanzania na mzalendo wa kweli, bila kujali hali yako ya maisha, elimu yako au nafasi yako ya kisiasa na kijamii, bila kujali kama wewe ni mfurukutwa au mkeretwa, bila kujali kama unafuata mrengo wa kulia au wa kushoto au kama itikadi yako ni ya kijamaa au ya kibepari; kama kweli una mapenzi na taifa lako, kama kweli unataka Tanzania ije kusimama kama Taifa la watu walio huru kweli na sawa; Taifa ambalo ndani yake kila mmoja ana nafasi sawa ya kufanikiwa; Taifa ambalo ndani yake wana na mabinti wake wanaona fahari kulitumikia na siyo kulitumia, kuliendeleza na sio kulitelekeza, kuliinua na siyo kulifumua! Taifa la kisasa, Taifa la Kiafrika, na Taifa ambalo kwa mafanikio na fahari litasimama katika jamii ya Mataifa ya ulimwengu!
Basi tunaitwa kufanya uamuzi, na uamuzi huo kwa hakika utakuwa ni wa kuwaudhi na kuwakera watu fulani fulani. Je uko tayari kuwaudhi mafisadi? Je uko tayari kuwakera waliokwiba fedha za Taifa letu? Je uko tayari kuwasumbua usiku kucha waliobaka raslimali za Taifa letu huku wanatuchekelea na kujilamba vinywa vyao huku wakipangusa ala zao?
Najua mimi niko tayari! sijui wewe.. lakini huko tunakokwenda, ni wale walio tayari kusimama peke yao na pweke ndio wataliinua Taifa letu na kulifanya liwe jinsi ile tulitamanivyo liwe! Stand up and be counted otherwise sit down and be forgotten!