Tunawadanganya wanawake kwa hoja ya 50 kwa 50

Tunawadanganya wanawake kwa hoja ya 50 kwa 50

Prof Phraoh AI

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
1,268
Reaction score
2,310
Kuna hii stori kila siku inapigiwa kelele mitandaoni, kwenye redio na tv, mashuleni n.k kwamba mwanamke na mwanaume wawe sawa, 50 kwa 50, kwenye kila jambo hadi kwenye uongozi.

kwamba Wanataka kuwe na mazingira ya kuwasukuma wanawake wawe viongozi. tena tuwatengenezee hayo mazingira.

Lakini swali ni moja — kama mtu hadi utengenezewe mazingira ndipo uwe kiongozi, je atakuwa kiongozi wa kweli? Maana kiongozi wa kweli anatokea kwa kusimama mwenyewe, kujisukuma mwenyewe na kuongoza hata bila kusukumwa na mtu mwengine.

Hebu tujaribu hata kuchunguza nature, tuone kama hiyo equality ya 50 kwa 50 kama kweli ipo:

1. Kwa Simba:
Simba dume ndiye mfalme wa nyika. Yeye ndiye hulinda familia, ndiye mwenye nguvu. Jike ni hodari kwenye kuwinda, lakini haiongozi kundi.

2. Kwa kuku:
Jogoo ndiye anayewika na kutangaza alfajiri. hata juki wakiwa wanapigana Jogoo akiingilia kila mmoja anasimama. Mtetea ana nafasi yake ya kulea, lakini sio wa mbele kwenye uongozi.

3. Kwa ng’ombe:
Dume ndiye wa kufanya kazi kubwa kulima, kuvuta mizigo wa kuongoza kundi, na wa kuheshimiwa.

4. Kwa ndege wa porini:
Tai au mwewe — ni dume hupigania nafasi ya kuwa mkuu wa familia. Hakuna kupewa nafasi, ni nguvu na ujasiri huamua.

5. Kwa nyuki:
Ingawa kuna Malkia wa nyuki, kazi nzito zote — ulinzi, kutafuta chakula, kujenga etc hufanywa na dume wa nyuki nyuki wengine.

6. Kwa tembo:
Tembo dume husafiri na kuongoza familia. Majike hushirikiana kulea watoto, lakini kwenye uongozi wa misafara mikubwa, ni dume huheshimiwa.
Uumbaji tu wa kila kitu unatambua jinsia ya kiume kama kiongozi

tukirudi kwenye Mwanzo wa kila kitu — Biblia.
Katika Mwanzo 2:7 Mungu alimuumba Adamu kutoka mavumbi. Kisha Mwanzo 2:21-22 akaumba mwanamke kutoka ubavuni mwa mwanaume si kutoka kichwani ili amtawale, wala kutoka miguuni ili akanyagwe, bali ubavuni ili awe "msaidizi wa kufanana naye."

Hii inaonesha wazi:
Mwanaume aliumbwa kuongoza. Mwanamke aliumbwa kusaidia.

Hiyo siyo kejeli kwa mwanamke. Ni nafasi ya heshima kubwa mno, lakini tofauti na ya mwanaume.

Leo tukisema wanaume na wanawake ni sawa kila jambo, tunavuruga mpangilio wa Mungu na wa nature. Tunatoa mwanamke kwenye nafasi yake ya kipekee, na tunamvisha mzigo ambao si wake.

Uongozi wa kweli hauji kwa huruma — unakuja kwa uwezo. Na kama uwezo huo haupo kwenye nature yako, utateseka tu kwa kuupigania.

Ndio maana hata mtaani au nyumbani mama anaheshimiwa, lakini baba anasikilizwa. Heshima ni ya wote, lakini nafasi si sawa.

hoja ya 50 kwa 50 ikifanikiwa ndo itakua mwanzo wa specie ya binadamu kupotea mwenye dunia ( nature hai support hivyo )

kila mtu ana umuhimu wake kwenye nafasi yake

wanawake wataingia period, pia watabeba ujauzito, watanyonyesha, hawana nguvu hata kimwili hata kuhimili mambo makubwa ya kisaikilojia, a kuna ula de wapo vizuri ili kua msaidizi wa wanaume


vya kuandika ni vingi na haviishi ila wanawake wasi tamani 50 kwa 50, kwanza hawawezi niazima wapiganiwe wanaenda against nature. kwenda against nature ni mbaya sana
 
Back
Top Bottom