Tunatumikia ibada tusizozijua na bila kufahamu

Mmmh! Wabongo bwana kwa kutishana, eti nilihudhuria lakini sikutumia yani uende kuzimu halafu usile chakula cha huko kwahio uliwaambia umefunga au? Hivi hizi propaganda zitaishaga lini? Mara Taa moja ya Toyo ni ishara ya Freemasonry mara taa ya Treni hebu tuacheni tule raha bwana, utaratibu wa kuchoma nyama kila mahali pana uchomaji wake sasa ule uchomaji mzuri ndio unaigwa na watu wote kwahio huo wa ndafu ndio mzuri ndio maana tunaufuata. Na pia hivi kipande cha nyama choma utakiokotaje kwenye sahani bila uma au kitu chenye ncha kali?
 
tapatalk_1492858741785.jpeg
 
Ndomana nilikua najiuliza bila majibu... Kwanini mwaka 2017_2018 umeongoza kwa kukata keki za kuzaliwa et happy birth day!!!.. Sasa naanza kuunganisha doti kwa mwanga mdogo hapo juu.
 
Vipi mkiombea kabla ya kula?

Chakula ni ibada kamili yale mapmbezi ni sehemu au ishara ya kuanza ibada ya kulisha mwili. ... Kuna kitu wengi hatufanyi kushukuru kwa maombi baada ya kumaliza kula ambayo ni ishara ya kumaliza ibada
 
Unapofanya sherehe, epuka kufanya mambo ambayo yataambatana na ibada usizozijua. Andaa vyakula na vinywaji lakini vitumike kwa utaratibu. Usiache chembechembe za hofu na maswali yasiyoisha. Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunamseta na kumuabisha shetani.
 
Back
Top Bottom