Tunatumikia ibada tusizozijua na bila kufahamu

Tunatumikia ibada tusizozijua na bila kufahamu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,172
Reaction score
866,429
Naandika makala hii si kwa ajili ya kubeza mila na desturi za wengine au kukosoa utaratibu uliozoeleka kwenye matukio mengi ya furaha.

Naandika makala hii kuonyesha siri mbinu na mitego anoyotumia shetani kumuangamiza mwanadamu
Kwa kuweka wazi jinsi shetani anavyoturubuni na kumtumikia bila kujua itatusaidia kumkabili adui huyu dhidi ya maisha yetu na wapendwa wetu

SHEREHE NYINGI ZA KUKATA KEKI NA NDAFU NI IBADA ZA SHETANI

Niliwahi kuhudhuria ibada ya mashetani nje ya Tanzania, tendo moja kubwa na muhimu ni kula nyama nakunywa damu ya binadamu. Ni tendo la kikatili mno na lililojaa mateso kwa mhanga! Mimi sikula wala kunywa.

Vitu muhimu viwili hutumika kisu kikali na uma unaofanana na huu;
1434178931066.jpg

Angalia tendo la kukata keki watu hukusanyika kuimba kwa pamoja kwa sauti ya juu na furaha kisha mlengwa huchukua kisu kikali na kukata keki iliyoandaliwa kisha huchukua uma na kuanza kuwalisha watu! Unajiuliza kwanini uma kwanini kisu kwanini hili tendo hufanywa maalum na la kipekee? Tafakari.

Tendo la kukata NDAFU

Chakula ni ibada takatifu, chakula hakichezewi, chakula ni dawa na tiba kwa ajili ya mwili, ni kitu cha kipekee mno, ndio maana kina utaratibu wake wa kukila! Refer table manners.

Sasa inaleta sintofahamu pale mnyama anapochinjwa lakini nyama yake isitengenezwe kwa utaratibu wa kawaida bali kubanikwa na kuwekwa kama sanamu kisha nyama yale kuliwa kwa style ileile ya kisu na uma! Hii ni ibada ambayo haimbariki Mungu.

Unajisikiaje kula nyama katika mtindo ule? Tendo la kufanya haya na tendo lile linalofanyika kwenye ibada za kumuabudu shetani vinashabihiana sana sana.

Kwahiyo wapendwa, hata wale ambao wana sherehe mbalimbali leo, tafakarini kwa makini mtakapokuwa mnakata keki na ndafu kwa kisu kikali kisha kuwalisha watu ama kwa uma au stiki zenye ncha kali.

Unapofanya sherehe, epuka kufanya mambo ambayo yataambatana na ibada usizozijua. Andaa vyakula na vinywaji lakini vitumike kwa utaratibu. Usiache chembechembe za hofu na maswali yasiyoisha. Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunamseta na kumuabisha shetani.

Ni mtazamo tu lakini wenye uhalisia...!

Usinichukie.
 
Utafurahi........subiri..........

jumamosi njema wakati ushaniharibia.........nina mwaliko wa harusi na nimepania kula ndafu mpaka inisalimu........hii mada ungeileta j3..............

😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂🙊🙊🙊🙈🙈🙈🙈🏃🏃🏃🏃
 
Mshana Jr kwani kabla ya kuvumbuliwa vitu hivi tunavyotumia zamani walikuwa wanatumia nini? Hawakuwa wanabanika na kuoka?
Nijuavyo mimi hizi dini tumeletewa na wazungu na waarabu, before that our ancestors walikuwa wanaabudu nini?
Help me pleaseeeeeeeeee
 
Sahihi kabisa KOKUTONA tulibanika na kuoka lakini sio kwa staili ya ndafu
Ancestors wetu waliabudu miungu kulikuwa na mungu wa jua wa mwezi wa maji wa upepo wa mvua nk nk na wote hao walifanyiwa ibada za matambiko ambazo hata hivyo ni tofauti kabisa na hizi ibada za shetani
 
Last edited by a moderator:

Mungu anafurahishwa na matambiko?
 
mshana jr

* Huyo binadamu mlikuwa mnamuua wenyewe au mnachukua maiti sehemu nyingine?

* Kama ukali wa kisu ni hoja, inaonekana kisipokuwa kikali hamna 'ushetani'

* Watu hutumia kisu 'kikali' na uma au 'stiki zenye ncha kali' kula vyakula vingi sio keki na ndafu tu, hii mada iko too specific kulenga 'sherehe' zenye keki na ndafu tu.
 
Kwenye keki na ndafu kisu uma na siku hizi stiki ni ada, na ni tendo la kipekee tofauti na vyakula vingine ambavyo vina mbadala
Pata hii picha kuna sherehe yenye keki au pengine ndafu kikikosekana kisu na uma vyaweza zua zogo na hata mleta keki kushushiwa mzigo wa lawama...tafakari
 
Tunaweza kubisha tu kwa mazoea na bila tafakuri ya kiba lakini hivi vitu ni ibada kamili na yenye madhabahu kamili jaribu kuangalia vibebeo vya keki vitambaa na vikolombwezo vingine utaniambia
 
Kwaiyo kila kitu ni ushetani sasa,iyo keki ulitaka ikwate kwa kijiko ndo ionekana ni jambo la ki Mungu au,so far hata kuku anabanikwa na ndege wengine kilichokufanya uone kubanikwa kwa mbuzi ni ushetani ni nini
 
Back
Top Bottom