Tunatengeneza mabwawa kwa ajili ya ufugaji wa samaki

Tunatengeneza mabwawa kwa ajili ya ufugaji wa samaki

Bwawa limeshakua tayari sasa ni Zoezi la kujaza maji,,
~Usiweke maji mpaka juu acha cm 30 au 40 toka kwenye 1.5m za kina Cha bwawa.
Hii itapunguza uwezekano wa kuingia wadudu hatari bwawani mfano.nyoka n.k

Itaongeza mawimbi katika bwawa ambayo ndio chanzo Cha uzalishaji wa hewa

Pia ni msaada mkubwa kwa samaki kutoka nje ya bwawa apa tunagusia kwa samaki wenye tabia ya kuruka mfano kambale.

Pia inapunguza hatari ya kuchukuliwa na ndege au wadudu wengine
IMG_20180922_172355.jpg
 
Weka wavu,,baada ya kuweka maji weka wavu juu ya bwawa hii ni kwasababu ya usalama kwa samaki toka kwa ndege,,wadudu na watu kuingia ndani ya bwawa
IMG_20180927_154414.jpg
 
Ni vizuri kuweka uzio au fensi kuzunguka bwawa au mabwawa kwa usalama zaidi,,au kutenganisha mabwawa na shughuri nyingine ambazo zinaweza sababisha hatari kwa samaki
 
Ni hatua ya kuweka vifaranga,
Weka vifaranga vyako vya samaki kwa utaratibu unaotakiwa ili wasiweze kufa,,
Chukua bag lako la vifaranga weka katika bwawa bila kulifungua,,likae kwa dakika 15 au 20 Kisha unalifungua na kuanza kuwaweka taratibu,,hii nikwaajiri ya kuwianisha au kulinganisha joto la maji ya kwenye bag la vifaranga na joto la maji ya bwawa,,ili samaki asione utofauti wowote
IMG_20180930_172821.jpg
 
Baada ya kuwaweka vifaranga katika bwawa sasa ni Zoezi la kulisha chakula,kubadilisha maji,,kuwapima samaki wako ukuaji wao Mara kwa Mara,,na mauzo baada ya kukua
IMG-20181003-WA0012.jpg
 
Mkuu mimi sitaki samaki wa biashara nataka nifuge samaki kwa ajili ya chakula changu tu mwenyewe na sina eneo kubwa mana ni kwangu eneo ambalo naweza kuweka bwawa ni 4×5 au 5×5 je linawezekana hilo
 
Mkuu mimi sitaki samaki wa biashara nataka nifuge samaki kwa ajili ya chakula changu tu mwenyewe na sina eneo kubwa mana ni kwangu eneo ambalo naweza kuweka bwawa ni 4×5 au 5×5 je linawezekana hilo
Ndio mkuu linawezekana,,
Unaweza Jenga la kutumia tofali,,unaweza kujenga kwa chuma na nylon (hili ni lakuamishika),,mabanzi na nylon (lakuamishika),, kuchimba na kuweka nylon n.k
 
Ndio mkuu linawezekana,,
Unaweza Jenga la kutumia tofali,,unaweza kujenga kwa chuma na nylon (hili ni lakuamishika),,mabanzi na nylon (lakuamishika),, kuchimba na kuweka nylon n.k
Sawa hilohilo naweza kuweka samaki wa kuzaliana ili wawe wanaongezeka
 
Sawa hilohilo naweza kuweka samaki wa kuzaliana ili wawe wanaongezeka
Kuweka samaki wa kuzaliana katika eneo dogo ni hatari Sana,,haishauriwi
Matokeo ya kuweka samaki wa kuzaliana ktk eneo dogo ni:
Samaki kukosa hewa
Kudumaa kwa uhaba wa chakula
Kupatwa na magonjwa kwa urahisi
Uchafu kuongezeka ktk bwawa
Ukiwa na bwawa kubwa ni rahisi kwa samaki wakuzaliana hayo yote ayatotokea
 
Ok ila kwa kufuga kiasi mana sio kuwaweka wengi. Mana wengne hatutumii nyama so ukifika wakati wa uvunaji ulaji utaongezeka
 
Ok ila kwa kufuga kiasi mana sio kuwaweka wengi. Mana wengne hatutumii nyama so ukifika wakati wa uvunaji ulaji utaongezeka
Yaah unaweza kuweka kiasi tu,, kuna viwango maalum ya kuweka samaki kwa Kila mita za mraba za bwawa mfano:
Bwawa la mita 5*10 weka sato kuanzia 500,,,kambale kuanzia 1000
Bwawa la mita 10*10 weka sato kuanzia 1000 na kambale kuanzia 1500
 
Pia unaweza kuweka samaki wengi kwa sehem ndogo ya bwawa ila kwa vigezo Kama:
~Uwe na mifumo ya kuongeza hewa kwa samaki
~uwe na mifumo ya kubadilisha maji Mara kwa Mara
~Chakula kiwe Bora
~vifaranga viwe Bora pia
Apo unaweza fuga samaki wengi kwa eneo dogo
 
Kuvua samaki kwa wavu(partial harvest)
IMG_20181027_132656.jpg
 
Uzalishaji wa vifaranga vya sato kupitia happa net
IMG_20180930_151354.jpg
 
Habari mkuu bwawa standard tu ni sh ngap kwa mkoa wa kilimanjaro kisiwani
Bwawa la kawaida au ufugaji wa kawaida wapo wanaoanza na kufuga samaki 1000 iwe Sato au kambale,,je unaitaji kujua gharama kwa ufugaji wa samaki idadi iyo?
 
Back
Top Bottom