Tunatengeneza mabwawa kwa ajili ya ufugaji wa samaki

Tunatengeneza mabwawa kwa ajili ya ufugaji wa samaki

29d787333a351dc044d09f3a504acfc0.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
Bwawa hili linachukua samaki wangapi na limegharimu kiasi gani?
 
Mkuu kwema? mnauza Pond liner?

Hivi kwa eneo la mita 30 X 20 wanaweza kaa samaki wangapi??
Kwema mkuu pond liner atuuzi ila kama unaitaji tunaweza kukutaftia,,
Kwa bwawa la mita 20×30 wanakaa kuanzia samaki elfu 6000 mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naombeni kuuliza kati ya ufugaji wa samaki na ufugaji wa kuku upi ni rahisi kufuga? Pia upi unafaida kubwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nime specialize kwenye ufugaji wa samaki sijui zaidi kuusu kuku,,ila nitakupa urahisi,ugumu(changamoto) na faida za ufugaji wa samaki;

1.Ugumu(changamoto) katika kufuga samaki
Zinatokea pale magonjwa yanapotokea kwa samaki,,na njia ya kuepuka ayo yasitokee ni kufanya maji yasichafuke(kubadilisha maji kwawakati)
2.kununua mbegu(vifaranga)visivyo weza kukua.
Suruhisho kwa hili ni kupata mbegu bora,,maana ukipata mbegu isiyokua unaweza kufuga kwa muda mrefu bila mafanikio
3.ujenzi wa bwawa..
Apa nisehem muhimu kuzingatiwa kabwa ya kuweka vifaranga vyako katika bwawa ni razima uakikishe au ujenge bwawa imara.

Hayo nimachache kwa upande wa ugumu(changamoto);:

URAISI KATIKA UFUGAJI SAMAKI
Ufugaji wasamaki unazingatiwa kwa mambo machache; mfano kulishwa,kubadilishiwa maji kwa wakati,hayo ni machache na muhimu ni rahisi kuyaudumia ukilinganisha na mifugo mingine.

FAIDA ZA UFUGAJI WA SAMAKI
Faida zimegawanyika katika makundi mbali mbali mfano;
1.kimazingira
2.kiuchumi
3.lishe
4.kiburudisho
Hizo ni baazi ya faida za ktk ufugaji samaki,,ila tunazingatia sana faida mbili,,kiuchumi,lishe

Kiuchumi: samaki anapato kubwa kwa miaka hii ya karibuni hii nikutokana na uhitaji wake mkubwa,,ukilinganisha na nyama za aina nyingine za mifugo mfano ng'ombe n.k

Lishe:; wana protein na madini mengine ambayo ni muhimu ktk maisha ya binadamu(ukuaji n.k)
Wanasayansi wanashauri kutumia samaki kama chanzo cha protein kuliko kutumia au kutafuta protein kutoka kwenye vyanzo vingine..
HAYO NI MACHACHE KUUSIANA NA UFUGAJI WA SAMAKI
 
fc1a288e37691e4611ac135e00d8d10a.jpg
ni vifaa na idadi ya vitu vinavyoitajika katika ujenzi wa bwawa kwa ukubwa wa mita 10*10
 
fc1a288e37691e4611ac135e00d8d10a.jpg
ni vifaa na idadi ya vitu vinavyoitajika katika ujenzi wa bwawa kwa ukubwa wa mita 10*10
Comrade
Nina Wazo la kufuga samaki katika eneo langu la makazi ambalo ni sqm 1695
Nataka nitumie eneo dogo la 10x10 m

Pia ktk kujenga nataka bwawa liwe limechimbwa
Yaani liwe usawa wa ardhi likitokea chini

Inawezekana????
 
Comrade
Nina Wazo la kufuga samaki katika eneo langu la makazi ambalo ni sqm 1695
Nataka nitumie eneo dogo la 10x10 m

Pia ktk kujenga nataka bwawa liwe limechimbwa
Yaani liwe usawa wa ardhi likitokea chini

Inawezekana????
Ndio mkuu inawezekana
 
Samaki kuanza kufugwa akiwa kifaranga mpk kuvunwa na kuliwa inachukua muda gani/miezi mingapi..??
 
Samaki kuanza kufugwa akiwa kifaranga mpk kuvunwa na kuliwa inachukua muda gani/miezi mingapi..??
Unaweza kuvuna samaki kuanzia miezi minne mpaka sita,,ikiwa umemlisha vizuri,umepata vifaranga vizuri,kumbadilishia maji kwawakati,umeweka vifaranga kulingana na ukubwa wa bwawa..ayo yanakuletea matokeo mazuri ktk ufugaji wako na utavuna kwawakati
 
ELIMU JUU YA VIFARANGA BORA NA MANUFAA YAKE(FAIDA)

Kwanza kuna aina mbili za vifaranga(kwa jinsia);katika ufugaji

1.Vifaranga vyenye jinsia tofauti(mixed sex) yaani jinsia ya kike na kiume.
Hawa Wapo kwaajiri yakuzariana ktk bwawa,
a).faida ya hawa ni kuongezeka ktk bwawa.
Angalizo;
Ufugaji huu unafaa kwa wale ambao wanamabwawa makubwa,mengi kwaajiri ya kuviamishia vifaranga vilivyo tayar ktk mabwawa mengine ili kuepusha msongamano na usumbufu baina yao(competition).
Wanaitaji chakula chakutosha,hewa,usafi wa maji ili kuweza kuwamudu ktk ukuaji wao vizuri.
Kwa bwawa dogo nitatizo sababu autoweza kutimiza ayo yote,hivyo awatokua vizuri hii kibiashara ni hasara.

2.Vifaranga vya jinsia moja(mono sex) hawa huwa ni vifaranga vyenye jinsia ya kiume(male).
Ni jinsia ya kiume sababu samaki aina ya sato wenye sex ya kiume wanakua zaidi ya female.Kabla ya vifaranga kuanza kuonyesha sex zao wanapatiwa chakula ambacho kina madawa yakuweza kuwabadilisha jinsia walionayo kwenda kuwa male sex
Faida ya vifaranga vya mono sex;
Kama nilivyo elezea apo mwanzo aina hii ya vifaranga Wapo kwaajiri ya kukua au kukuzwa,wanauwezo wakukua au kukuzwa ata kufikia nusu/kilo kwa samaki baada ya kukua
Angalizo: anaweza kukua kufikia uzito mkubwa kutegemea na muda uliomfuga,chakula,maji,mbegu(vifaranga) pamoja na wingi wao ktk bwawa hivi vikizingatiwa na kua ktk ubora basi utegemee kupata au kuvuna samaki wenye uzito mkubwa.
HAYO NI MACHACHE KUUSIANA NA AINA YA VIFARANGA NA FAIDA ZAKE
Ahsanteni..
 
KWA WALIOPO ARUSHA NA MOSHI VIFARANGA VYA SATO VINAPATIKANA KWA ULAISI SASA.
Nitofauti na kipindi cha nyuma watu wa kutoka arusha na moshi kununua vifaranga mbali na maeneo yao
 
Back
Top Bottom