Tunategemea CCM waje na Katibu Mkuu mwenye nguvu ya ushawishi au waendelee kuwekeza kwenye tume na dola?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Hali ilivyo nchini kuna njia mbili yakuamua siasa za 2024 hadi 2025. Njia ya kwanza ni chama cha mapinduzi kuweka kwenye safu yake viongozi wenye ushawishi kwa jamii. Kwa mtazamo wangu hakuna jina la katibu mkuu linaweza likawa na ushawishi kuliko jina la makamu mwenyekiti bara Ndugu Kinana. Kinana pamoja na ukongwe wake amekataliwa kwenye siasa za jukwaani, je ni nani anayekuja na nguvu ya umma zaidi?

Alikuja Mwenezi wao wakiamini binadamu wamesau uovu wao lakini watu wamemkataa......amekwenda Zanzibar hakuna mwenye muda naye....amefanya tamasha lakini bado gia zimegoma.

Tumeona hapa namna panavyopigwa chapuo Sabaya apewe uteuzi.....hawa wanaopiga hizi Ramli wanalenga kunufaika na ukatili na unyama wa watu hawa.

Njia pekee iliyobaki kwa CCM nikuwekeza kwenye mambo yafuatayo:
1. Kuwapandisha vyeo maafisa na askari wa vyombo vya dola.

2. Kuwaongezea maslahi watumishi wa vyombo vya dola katika bajeti zijazo

3. Kufanya uteuzi wa watendaji kutoka kwenye dola kwenda kuongoza halmashauri na majiji nchini.

4. Kuongeza kasi kutatua kero za wananchi

5. Kuwatengeneza viongozi wa upinzani mwenye kuipigia kampeni CCM kama ambavyo ambavyo tumeona kwenye maoni ya tume

6. Kuwavuta viongozi wa dini na mila watoe matamko yakuunga mkono serikali.

Pamoja na yote bado upigaji kura utafanywa na wachache
 
Back
Top Bottom