tbc ni wanafiki wakubwaWananchi watanzania tumezoea kuhabarishwa kupitia hiki chombo cha UMMA hasa taarifa ya habari kila saa mbili jioni. Leo vipi mnatuonesha mafisadi na wezi wanavyo kula matunda ya uhuru wa nchi yetu.Astagaflah kwahiyo mmeona kufanya hivyo MODS NAJUA NAWEZA PEWA BAN KWA HILI NITAKALOSEMA Serikali na viongozi wake ni wapumbavu,wajinga,manyani,******* tena saanaa am ready for any thing.
Wanajamvi mnapoweka Uzi humu kuhusu habari mlizoona ktk TV au kusikia ktk Redio jaribuni kuweka/kuandika Habari yenyewe inahusu nini kwa kirefu na undani ili wale ambao hatuna idea nasi mtuhabarishe.
Kuna watu humu tunaandika tukiwa nje ya TZ, wapo ambao hawaangalii TBC kabisa,
Kwa ufupi ni kwamba Prince Charles na mkewe wako hapa tz kwa ziara ya siku mbili, sasa JK amewaandalia chakula cha jioni pale ikulu. Wanacholalamikia hapa wanaJF ni kile kitendo cha TV ya taifa kukatisha vipindi(ikiwemo taarifa ya habari ya saa mbili usiku) na kuonesha kinachoendelea pale ukumbini.
Mimi pia hiki kitendo kimenihuzunisha sana, kwa mantiki kwamba hakuna habari/tukio lolote la maana lililokuwa linaendelea pale ukumbini.
Mi nadhani ilitosha tu sisi kujua kwamba amekuja nchini na mh. jk amemwandalia chakula cha jioni kupitia taarifa mbalimbali za habari; na sio kutupotezea muda wetu kuangalia tukio zima.
This is sometimes funny, mchana msafara wake umefunga barabara, usiku amefunga vipindi kwenye TV. Kilichokuwa kinatia kichefuchefu zaidi, ni jinsi vigogo walivyokuwa wanaonekana wakitumbua mapochopocho pale ukumbini huku wavuja jasho wengi wakiwa hawana hakika ya kupata hata huo mlo mmoja wa usiku huu.
Ile ilikuwa ni dhifa ya "Kitaifa" ulitaka isitangazwe na TV ya Taifa? Unanchekesha, hizo taarifa za habari zinakwisha? lakini ni mara ngapi unapata wageni kama yule hapa?
Ile ilikuwa ni dhifa ya "Kitaifa" ulitaka isitangazwe na TV ya Taifa? Unanchekesha, hizo taarifa za habari zinakwisha? lakini ni mara ngapi unapata wageni kama yule hapa?
JK hajaalikwa dhifa ya kitaifa? Aliwahi kuwa live kwenye nchi ipi? Au yeye ni inferior prezdaa?