Tunasherekea uhuru wa nchi ambayo haipo kwa sasa

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,667
1,566
Leo tunasheherekea sikukuu ya uhuru wa Tanganyika. Nchi ambayo imekufa baada ya nchi hiyo kuungana na Zanzibar 1964.

Hakuna bendera ya Tanganyika hata bendera inayopepea leo ni ni bendera ya Tanzania na si Tanganyika.

Kwanini kupoteza pesa zote hizi kusheherekea kitu ambacho hakipo!?

Kwanini tusingefanya kama mwaka jana?

Kwanini tusiue sherehe za uhuru wa nchi zote mbili yaani Zanzibar na Tanganyika kisha tukawa na siku moja tu kubwa ya uhuru ambayo ni 26 April?
 
Ni Taifa la Wanafiki tu duniani ndilo liwezalo kuadhimisha "birthday ya marehemu Tanganyika". Kama tumeikataa Tanganyika na kuiua kupitia koti la muungano,iweje tuendelee kupoteza fedha za umma kufanya maadhimisho ya kitu kisichokuwepo na bado wapumbavu wakashangilia?

Napendekeza katika maadhimisho hayo kuandaliwe na tuzo ya kujipongeza kwa kuwa Taifa la watu wasio waaminifu duniani.
 
Kinachonifurahisha leo ni kuona waliovaa sare za chama hapa uwanjani ni wachache sana kuliko miaka iliyopita.
 
Kinachonifurahisha leo ni kuona waliovaa sare za chama hapa uwanjani ni wachache sana kuliko miaka iliyopita.



Watakimbiliaje kuvaa sare wakati sare hizo hazina msaada wowote katika maisha yao ya kila siku?Wote tunaisoma namba,hakuna anayepata upendeleo wa maisha kwa kuvaa sare za CCM,kale kawimbo ka CCM mbele kwa mbele kamegeuka mjeledi wa miiba juu ya miili yao.
 
Mkuu tawa nakupongeza kwa ufikiri wako.
Hakika hili ni swali ambalo watu wengi wamejiuliza lakini wanaogopa kuzungumza wazi wazi mbele za watu
 
Mkuu tawa nakupongeza kwa ufikiri wako.
Hakika hili ni swali ambalo watu wengi wamejiuliza lakini wanaogopa kuzungumza wazi wazi mbele za watu
Huo ndiyo unafiki wenyewe mkuu mfizigo. Naona na rais wa nchi jirani ya Zanzibar amehudhuria pia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom