Tunaposema hakuna ukabila huku tukiendelea kuulizana kabila ni suala la ajabu sana

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,878
Wewe ni kabila gani! Hii ni moja kati ya vitu ambavyo Nyerere alijaribu ku-discourage ili kuua ukabila, intermarriages na system ya uongozi ilifanya kuuweka ukabila mbali na sisi ili tuweze kuishi kama Watanzania na sio kama watu wa kabila fulani hali ambayo ni hatarishi kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla wake.

Hali imekuwa tofauti kwa miaka yetu, kwa kuwa swali la wewe ni kabila gani, kwa sasa ni swala la kawaida sana, haswa kwenye taasisi za serikali. Sioni umuhimu wa kumuuliza mtu kabila wakati wa usajili wowote huko serikalini, zaidi hii inakuza ukabila.

NSSF, NIDA, POLISI na maeneo mengine wamekuwa na kawaida ya kuuliza kabila la mtu. Lakini kabila la mtu linaendana vipi na huduma mabayo mtu husika anapaswa kupatiwa. Tumekimbia kivuli tunaenda kukutana na kiumbe mwenyewe kabisa.

Tunaposema hakuna ukabila huku tukiendelea kuulizana kabila ni suala la ajabu sana.

Ukabila hauanzii wala hauishii kwa hizi kauli mbili tatu za vingozi kuhusu kundi Fulani la watu. Zaidi ni kuwa tunakasirika tu kauli zikiwa mbaya kwenye makundi yetu.

Ukabila upo!

Salaam.
 
Watu wanashangaa kuona mchaga hapendi Rushwa-Mtu flani.

Mengi ndie mchaga pekee aliyekua anasaidia walemavu-Governor wa dar
 
Back
Top Bottom