Tunapendana, tatizo ni umri na dini, naombeni ushauri

Tunapendana, tatizo ni umri na dini, naombeni ushauri

nilishawahi kumtakaa mkaka mmoja kisa tu kwenye L anaweka R na vise versa.
Hata hamu ya kuchangia imeisha.
 
Wewe ni mwanaume huyo mchumba kakuzidi miaka mitano Ok...No comment!!

Hivi unawajua vizuri mabinti au unakurupuka tu? lazima a-pretend kuwa anakupenda kwa dh
 
mnatakiwa mkae na muangalie mambo ya msingi kwanza kwenu na baadae..
umri si tatizo sana japo hukuweka wazi umri wenu maana isije ikawa ke kashafikisha /kazidi 40 .. kumbuka kuna suala la kutengeneza familia yenye misingi au mtazamo fulani kiimani , hivyo mnapaswa kujadili watoto watafuata imani ipi japo kwa makubaliano hayo inabidi upande mmoja ulidhie iman ya upande mwingine na kuhakikisha anatoa ushirikiano hasa kwa watoto katika imani moja
 
tatizo nawaza wazazi wangu watanielewa? na wazazi wake je c wataniona mtoto?

Kwahyo ww ndo utaenda kuwaambia hao wazazi kuwa umemzidi umri binti?
Watakuona mdogo!!?wanapima kwa macho?

Hapo labda uniambie suala la imani kweli hapo usifanye kosa
 
Kwahyo ww ndo utaenda kuwaambia hao wazazi kuwa umemzidi umri binti?
Watakuona mdogo!!?wanapima kwa macho?

Hapo labda uniambie suala la imani kweli hapo usifanye kosa

kiuhalisia unapopeleka taarifa kuhusu uchumba maswali ya umri, muda wa uhusiano , anakotokea (kabila /uenyeji wa mchumba), imani etc pia utakapompeleka kwenu au wewe kwenda kwao watamwangalia na kuweza kuona ukomavu wa mwili / kukadiria umri

hivyo ni vyema uelezee haya masuala kwa utaratibu uone nini mtazamo wao kabla hujamfikisha mhusika au wewe kwenda huko .. kwa kifupi mazingira yenu lazima yawe wazi toka mwanzo ili isisumbue baadae
 
Kwa umri sio tatizo mmepishana kidogo sana, ila kwa dini mmpishana mno..!! Nakushauri utafute chaguo lingine, hata wazazi wako watakupa ushauri kama huu huu.
 
Kwahyo ww ndo utaenda kuwaambia hao wazazi kuwa umemzidi umri binti?
Watakuona mdogo!!?wanapima kwa macho?

Hapo labda uniambie suala la imani kweli hapo usifanye kosa

Dada angu miaka mitano unaona kidogo? Na umri wangu naweza kuoa mtoto wa miaka 24 lakini kijana mwenye 26 simshauri aoe mdada mwenye 31...tofauti ni kubwa mno..! Tena mno..!
Tofauti ya imani ndio kabisa sasa...bora hata wangekuwa wakristo iwe shida ya kimadhehebu..mmh..muislam na mkristo mie sijashauri bado..!
 
Dada angu miaka mitano unaona kidogo? Na umri wangu naweza kuoa mtoto wa miaka 24 lakini kijana mwenye 26 simshauri aoe mdada mwenye 31...tofauti ni kubwa mno..! Tena mno..!
Tofauti ya imani ndio kabisa sasa...bora hata wangekuwa wakristo iwe shida ya kimadhehebu..mmh..muislam na mkristo mie sijashauri bado..!

Hata mi kwenye imani simshauri
Bt unri sio issue to mi...
Coz nimeona ambao wako hivyo wanaishi poa tu
 
Suala lako naweza kukujibu hivi katika utaratibu wa kanisa hasa kanisa katoliki inakubalika muumini mkatoliki kufunga ndoa na mtu asiye muumini mkatoliki kama vile muislamu au mkristo wa madhehebu mengine. Ndoa za aina hiyo zinaitwa ndoa mseto, masharti yake ni kwamba inabidi zifungwe katika kanisa katoliki. Hivyo inawezekana kwa muislamu kuoana na mkristo hasa mkatoliki kwa kufuata utaratibu huo na baada ya ndoa kila mmoja akaendelea na imani yake. Hivyo basi mnaweza kushauriana na wazazi wenu ili muone kama mnaweza kufanya hivyo.

Pili ni kwamba suala la dini linachukua sura ya pekee kama imani yako ndiyo inayoongoza maisha yako yaani kila jambo unalofanya ni lazima lipate kwanza tafsiri ya kiimani, hapo kuwa na mtu wa imani tofauti na yako inaleta tatizo kubwa sana. Lakini kama maisha yako hayapo shaped na imani yako basi unaweza kuishi na mtu wa imani nyingine bila tatizo lolote. Hivyo kama imani yako ndio inayokuongoza kwa kile jambo basi nakushauri fuata utaratibu mwingine, yaani au mmoja wenu abadili dini na kumfuata mwenzake au kila mmoja akatafute mwenzi mwingine.
 
Usijaribu kabisa kuendelea na huo uhusiano.Nina uzoefu na suala kama lako....baadae mtashindwa tu.
Achaneni mapema kwa amani kila mtu akapate anayemstahili
 
we nawe si nimeona uzi wako una mchumba wa miezi minne umelala nae tu simu zako akujibu
unampelekaje sasa
 
kama pesa anayo, mambo yote yatakuwa sawa tu....zawadi kwa wazazi, huwa wanalainika! all the best my friend
 
Nina mpenzi ambae ananipenda sana nami pia nampenda kwani ananijari sana, ila amenizidi miaka 5 na tupo dini tofauti yeye ni mkristo na wazazi wake wameishika sana dini, mimi ni muislam vile vile wazazi wangu wameishika dini sana.

Kudhihirisha kuwa ananipenda mara kwa mara ananisisitiza mimi nikajitambulishe kwao kisha nimpeleke na kwetu.Mimi nampenda sana ila sitaki kukurupuka kwani taswira inaonesha wazazi wetu hawatokubariana na sisi kulingana na tofauti zetu.

WanaJF tafadhari naomba mnishauri katika hili nimechanganyikiwa mwenzenu na binti sipendi nimkose
.

Life expectancy ya mwanaume ni aproximately 75 yrs
Na mwanamke ni 81 yrs no worries mtazeeka pamoja.
Umri sio ishu. Dini mmoja wenu akubali kubadili tu!
 
Life expectancy ya mwanaume ni aproximately 75 yrs
Na mwanamke ni 81 yrs no worries mtazeeka pamoja.
Umri sio ishu. Dini mmoja wenu akubali kubadili tu!
asante ila alisha nibwaga nashukuru kwa mawazo yako mazuri
 
Back
Top Bottom