X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,791
- 15,016
Nina mpenzi ambae ananipenda sana nami pia nampenda kwani ananijari sana, ila amenizidi miaka 5 na tupo dini tofauti yeye ni mkristo na wazazi wake wameishika sana dini, mimi ni muislam vile vile wazazi wangu wameishika dini sana.
Kudhihirisha kuwa ananipenda mara kwa mara ananisisitiza mimi nikajitambulishe kwao kisha nimpeleke na kwetu.Mimi nampenda sana ila sitaki kukurupuka kwani taswira inaonesha wazazi wetu hawatokubariana na sisi kulingana na tofauti zetu.
WanaJF tafadhari naomba mnishauri katika hili nimechanganyikiwa mwenzenu na binti sipendi nimkose.