Habarini!!
Huu msemo sio mgeni kwako na kwangu hata mimi nilikua nikikua huku nausikia na Sasa nimeamini kuwa kupenda ni Mara moja tu
Nimekuwa kwenye mahusiano hapo nyuma lakini sijawahi kupenda, sijawahi kumlilia mwanaume kwa lolote wala sijawahi kuomba msamaha nadhani mfumo jike ulinitawala sikuwa na hisia na yeyote nilie wahi kuwa nae
Maisha yamebadilika Sasa ndipo nikagundua kuwa kwasasa nimependa kweli nimekuwa mdogo Kama piriton mwenye machozi yasiyoisha nikikosea na napenda kwa dhati haijalishi nini
Je ni kweli nawewe kwa upande wako imekutokea hii kwamba umewahi kupenda mara1 tofauti na Mara nyingine zote? Hata kwa wenye wapenzi wengi yupo mmoja ambae ndie unique unaemuhusudu??
Nipeni uzoefu
Nawasilisha