Kwa yeyote mwenye taarifa, au mwenye uwezo wa kutusaidia, asubuhi ya leo, Jumapili, Oktoba 3, 2010, kwenye eneo la maegesho ya magari nje ya Kigango cha Mt. Thomas Moore, Ally Sykes Close, Mbezi Beach, takriban saa 4 za asubuhi, wakati misa ikiendelea, gari aina ya Suzuki Swift iliyokuwa kwenye eneo hilo ilivunjwa kioo cha nyuma na mlango wa nyuma kufunguliwa, hatimaye kuwezesha baadhi ya vitu vilivyokuwamo ndani yake kuchukuliwa na mtu au watu wasiojulikana.
Kwako wewe uliyechukua vitu hivyo, tunajua kwamba labda utadhani kwamba huu ni mtego. La hasha. Tunachotaka ni vitu hivyo kurejeshwa kwani ni hasara kubwa sana kwetu. Tupo tayari kukuzawadia kwa ushirikiano wako, kwani hatuna muda wa kwenda kufungua kesi Polisi au Mahakamani, kwani tuna uhakika kwamba kwa njia hii HATUTAFANIKIWA. Tunachokuomba ni uaminifu wako na imani yako, kwamba, hatutachukua hatua zozote za kisheria.
Tafadhali turejeshee vitu vyote vilivyokuwamo ndani ya gari, tuko tayari kukupa kiasi kizuri cha pesa kama shukrani yetu kwako. Muda wa kuomba upya kadi ya benki ya CRDB, kutafuta kitambulisho kipya cha kazi, kutafuta kadi ya mpiga-kura huku zikiwa imebaki siku chache sana kabla ya Uchaguzi Mkuu, na hii ni muhimu zaidi, kumbukumbu za namba za simu na picha zilizopo kwenye simu za mkononi (ambazo thamani yake haihesabiki), vyote hatuna muda wa kufuatilia, ni hasara kwetu.
Tunajua kwamba ni dhiki ndiyo inayokusumbua, na kwamba, unaona kwamba hiyo ndiyo njia sahihi kwako kujipatia chochote. Hatuwezi kukuhukumu kwa kuwa maskini!
Tafadhali wasiliana nasi kwa namba za simu 0715-019119 na/au 0786-019019, ili tuweze kukutana nawe na kurejeshewa vitu hivyo.
Asante.
Familia ya Bw. na Bibi Aziz Losika Mongi
P.S. Ni bora tukayamaliza kati yetu kuliko kupelekana Polisi, ambapo hatutapata muafaka!