G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Matokeo yanasema kuwa hatimaye rais Magufuli ataongoza hadi 2022. Tumeshaona wanataka nini, nani anasukuma hili na kwa nini?
Haya ni matokeo ya ushawishi wa rafiki yetu kipenzi Paul Kagame.
Rais Magufuli amefanana na Kagame pengine kwa kila kitu! one man show, ukaliukali (Kagame aliwahi kupiga mtu hadharani, nadhani hii haitakuwa habari ya kushtukiza kama yule naye atafanya hivyo! Anawaita wapumbavu, anawachana kama alivyoenda nao bandarini, akiwa nao ikulu anawapa makavu kwa hasira). Pia kwenye kuuminya upinzani wanafanana.
Magufuli wala alikuwa hana mpango wa kupeleka reli Rwanda haraka hivyo. Safari ya Kagame ya siku moja imemfanya hata Magufuli akasema "Kwa kile kipande cha kule Nzasa kuelekea Kigali tutaangalia tunachangiana vipi. Tunachangiana? Kwanza hatuhitaji kufanya biashara na wanyarwanda maana tunawajua!
Swala la miaka saba kamwe halitengani na Magufuli! Ni aina ya kiongozi wa miaka saba na hilo litatekelezwa. Ndiyo maana aliwapigia simu kina Kafulila na Lowassa warudi CCM, Lissu aliwekewa target yake Mungu akaepusha, wengi wameminywa ili hilo litakapoletwa hadharani lipite kiulaini.
Miaka saba siyo ajenda ya Juma Nkamia bali ni ajenda ya CCM. Isingekuwa ajenda ya CCM basi Nkamia angeshaonywa hadharani. Kule Zanzibar tayari wameshaisema. Hivyo ilishajadiliwa sirini na itatekelezwa. Dodoma pale Magufuli atadumu sana. Tunaanza na miaka saba baadaye tunaondoa ukomo wa kugombea. Ndiyo aina ya uongozi wa kula nyama za watu! Utaanza na damu, utachagua baadhi ya maeneo utaendelea kunogewa na hatimaye utaupenda mwili mzima wa binadamu.
Tuko naye! Tukimshindwa basi hatuna jinsi zaidi ya kuvumilia liende. Kama huzioni dalili za mtu kutawala maisha (Siyo miaka saba maana ni kianzio tu cha kumla binadamu) Basi unahitaji miwani!