Tunaoielewa CCM tumemuelewa Juma Nkamia, tumeshayaona matokeo

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,879
Matokeo yanasema kuwa hatimaye rais Magufuli ataongoza hadi 2022. Tumeshaona wanataka nini, nani anasukuma hili na kwa nini?

Haya ni matokeo ya ushawishi wa rafiki yetu kipenzi Paul Kagame.

Rais Magufuli amefanana na Kagame pengine kwa kila kitu! one man show, ukaliukali (Kagame aliwahi kupiga mtu hadharani, nadhani hii haitakuwa habari ya kushtukiza kama yule naye atafanya hivyo! Anawaita wapumbavu, anawachana kama alivyoenda nao bandarini, akiwa nao ikulu anawapa makavu kwa hasira). Pia kwenye kuuminya upinzani wanafanana.

Magufuli wala alikuwa hana mpango wa kupeleka reli Rwanda haraka hivyo. Safari ya Kagame ya siku moja imemfanya hata Magufuli akasema "Kwa kile kipande cha kule Nzasa kuelekea Kigali tutaangalia tunachangiana vipi. Tunachangiana? Kwanza hatuhitaji kufanya biashara na wanyarwanda maana tunawajua!

Swala la miaka saba kamwe halitengani na Magufuli! Ni aina ya kiongozi wa miaka saba na hilo litatekelezwa. Ndiyo maana aliwapigia simu kina Kafulila na Lowassa warudi CCM, Lissu aliwekewa target yake Mungu akaepusha, wengi wameminywa ili hilo litakapoletwa hadharani lipite kiulaini.

Miaka saba siyo ajenda ya Juma Nkamia bali ni ajenda ya CCM. Isingekuwa ajenda ya CCM basi Nkamia angeshaonywa hadharani. Kule Zanzibar tayari wameshaisema. Hivyo ilishajadiliwa sirini na itatekelezwa. Dodoma pale Magufuli atadumu sana. Tunaanza na miaka saba baadaye tunaondoa ukomo wa kugombea. Ndiyo aina ya uongozi wa kula nyama za watu! Utaanza na damu, utachagua baadhi ya maeneo utaendelea kunogewa na hatimaye utaupenda mwili mzima wa binadamu.

Tuko naye! Tukimshindwa basi hatuna jinsi zaidi ya kuvumilia liende. Kama huzioni dalili za mtu kutawala maisha (Siyo miaka saba maana ni kianzio tu cha kumla binadamu) Basi unahitaji miwani!
 
Democracy,anaesema mitano yupo sahihi, anaesema kumi yupo sahihi,anaesema Saba pia yupo sahihi,
Si ndio Democracy?
Wananchi ndio waliamua iwe mitano,wakaweka kwenye katiba katika wakati wao,kama wananchi wa sasa wanaona kunafaa kuwepo na mabadiliko iwepo referendum tu...
Democracy inatabia ya kuheshimu ata maoni ya wachache....mifano hai ipo.
 
Matokeo yanasema kuwa hatimaye rais Magufuli ataongoza hadi 2022. Tumeshaona wanataka nini, nani anasukuma hili na kwa nini?

Haya ni matokeo ya ushawishi wa rafiki yetu kipenzi Paul Kagame. ...
G Sam, kuwa jasiri na kutamka wazi kuwa una chuki na Magufuli na siyo Urais wake! Labda nikuulize Ni kwa nini utawala wa Rais ni miaka mitano mitano? Na ni nani alifanya maamuzi hayo?
 
Huenda siku ambayo Tanzania mtaacha kuhangaika, kumshambulia na kumchukia Rais wa Rwanda Paul Kagame ndiyo ikawa mwanzo wenu mzuri wa kuanza kuwa na Maendeleo yenu hasa ya Kiuchumi na Kijamii. Kinachonisikitisha huyo Rais Kagame mnayehangaika nae Yeye nchi yake kila siku inapiga hatua na si ajabu hata muda si mrefu ikaja kuipita Tanzania lakini Tanzania bado inapiga tu ' mark time ' Kimaendeleo huku mkiwa mmewekeza katika Majungu, Chuki, Unafiki, Husuda, Uswahili na Fitna.

Badilikeni bado hamjachelewa!
 
G Sam, kuwa jasiri na kutamka wazi kuwa una chuki na Magufuli na siyo Urais wake! Labda nikuulize Ni kwa nini utawala wa Rais ni miaka mitano mitano? Na ni nani alifanya maamuzi hayo?
Mhm!, There we go. Safabu inayo halalisha 5 ita halalisha 7, 10,...ufalme
 
Democracy,anaesema mitano yupo sahihi, anaesema kumi yupo sahihi,anaesema Saba pia yupo sahihi,
Si ndio Democracy?
Wananchi ndio waliamua iwe mitano,wakaweka kwenye katiba katika wakati wao,kama wananchi wa sasa wanaona kunafaa kuwepo na mabadiliko iwepo referendum tu...
Democracy inatabia ya kuheshimu ata maoni ya wachache....mifano hai ipo.

TUnapochukua maoni ya wachache badala ya maoni ya weingi hiyo sio demokrasia.
 
Maadam haishi nyumbani kwangu aendelee na frastresheni zake atakavyo
 
Democracy,anaesema mitano yupo sahihi, anaesema kumi yupo sahihi,anaesema Saba pia yupo sahihi,
Si ndio Democracy?
Wananchi ndio waliamua iwe mitano,wakaweka kwenye katiba katika wakati wao,kama wananchi wa sasa wanaona kunafaa kuwepo na mabadiliko iwepo referendum tu...
Democracy inatbia ya
kuheshimu ata maoni ya
wachache....mifano hai ipo.[/
QUOTE]

Mkuu watanzania tulitoa maoni yetu kwenye tume ya Sinde Warioba tena kwa uhuru kabisa mbona hatukuona pendekezo hili la miaka 7 hii inayofanyika sasa ni uchochezi!
 
Back
Top Bottom