Tunaoielewa CCM tumemuelewa Juma Nkamia, tumeshayaona matokeo

G Sam wewe sio tu unaielewa CCM, unaielewa pia emokrasia na kutambua nguvu zake. Unafshamu fika watu wakiamua hakuna wa kuzuia.

Hoja ya wananchi itawasilishwa bungeni na muwakilishi wa wananchi, mbunge.Wabunge, ambao ni wawakilishi wa wananchi watafanya maamuzi kwa niaba ya wananchi. Demokrasia imefuata mkondo wake.

Ikifanyika hivyo kutakuwa kuna kosa hapo? Mapungufu yepi yatajuwepo?
 
Uko sahihi sana mkuu,ila nikukosoe kidogo,sio ajenda ya WanaCCM wote,ni ajenda ya wanachama wachache wenye maslahi na mkulu,lakin kwa kuwa wanaCCM wengi ni waoga na hivyo kuwa wagumu kutoa maamuzi,hiyo hoja itapita tu!! Miaka saba ileeeeeeeeeeee!!!
 
Binafsi sioni tatizo ktk hilo.

Binafsi sijaona manufaa ya demokrasi zaidi ya maangamizi.

Napenda mabadiliko na haya ni mabadiliko.

Ni uchoyo tu ndio unaotuletea hili gubu na njia nzuri kufanikisha hili ni kwa wabunge pia waongezewe miaka hadi 7, madiwani pia.

Hivi anaeongezewa ni rais kama taasisi au magufuli kama magufuli.

Uzoefu ni kwamba kipindi cha miaka 5 haitoshi. Kwani Mwaka wa kwanza unachukua uzoefu, Mwaka wa 2,3 unafanya kazi Mwaka wa NNE unashtuka na unaanza kampeni ya term mpya. Mwaka wa 5 ni hakuna kazi ni maandalizi kwa ajili ya kampeni ya awamu ya pili
Miaka kumi ya Kikwete maendeleo makubwa yameonekana nchi nzima.

Maisha ya watu yameboreshwa na nyumba za nyasi zilipungua nchi nzima.
Mnataka kutupeleka wapi?
Mbona nyie watawala miaka miwili inawatosha kujenga familia zenu?
Iweje miaka mitano isitoshe wakati hamtumii fedha zenu?

Eti anachukua uzoefu.
Nchi inaendeshwa kwa mipango.
Kubadili mifumo kila siku ndio janga kubwa la nchi maskini mana hazina mifumo imara zaidi ya kuendeshwa na mtu mmoja.

Nchi sio nyumba ya mtu.
Kuna misingi inayopaswa ifuatwe.
Na huu udhaifu unatumiwa na CCM kurubuni wananchi na kuwalaghai.
Hata kama atakaa miaka mia lakini apigiwe kura kula baada ya miaka mitano.
Hata Nyerere kipindi chake alipigia kura kila baada ya miaka 5 pamoja na kuwa palikua na chama kimoja.

Huu upuuzi wa kuongezewa muda unashabikiwa na wateule zaidi.
Kama mnataka badi tafuteni maoni ya wananchi muunga she na katiba ya warioba.
Kwa nini wanasiasa mnajali sana matumbo yenu kuliko mustakabali wa nchi?
Hapa kilichoangaliwa ni siasa tu na uchaguzi lakini amani ya nchi haiangaliwi kwa undani, umoja wa kitaifa haujadiliwi zaidi ya ubinafsi wa kuongezewa madaraka na kutaka kuvunja katiba.

Tuna katiba ya warioba iliyoadisisiwa na wananchi sasa tunataka kuiweka pembeni ili tuhangaike kufurahisha watu wasiozidi kumi kwenye nchi ya watu mil.40.

Wekeni uhuru wa kujadili haya mambo kwa wazi na kuyapatia majibu ya wazi.

Kuongezewa hao akina baba na akina mama za watu miaka mingi ya kututawala wenyewe kama vile wao ni miungu haitakaa iwezekane kwenye nchi hii labda wakaongeze mikataba ya ndoa zao na familia zao sio Tanganyika na Zanzibar.
Kuna mmoja miaka zaidi ya 16 makamu wa Rais ,mika 10 rais lakini bado wanaibuka watu wanataka aongezewe Muda wa kuwa Rais.
Hii hata kwa Mungu ni dhambi.
Ni ulevi wa madaraka.
Wakina Kagame wametokea misituni kama manyani mpaka wakawa maraisi lakini kwa Tanzania watu wametokea kwenye uwaziri kuwa maraisi. Wamshukuru Mungu kwa sababu wako pale kwa sababu ya umoja na amani yetu sio ubabe wao.

Tumuogope Mungu.
Yote yatapita.
Nyerere angeng'ang'ania leo akiwa kavurini asingetajwa kwa heshima kubwa na kuenziwa kwa vizazi vyote.
 
Matokeo yanasema kuwa hatimaye rais Magufuli ataongoza hadi 2022. Tumeshaona wanataka nini, nani anasukuma hili na kwa nini?

Haya ni matokeo ya ushawishi wa rafiki yetu kipenzi Paul Kagame.

Rais Magufuli amefanana na Kagame pengine kwa kila kitu! one man show, ukaliukali (Kagame aliwahi kupiga mtu hadharani, nadhani hii haitakuwa habari ya kushtukiza kama yule naye atafanya hivyo! Anawaita wapumbavu, anawachana kama alivyoenda nao bandarini, akiwa nao ikulu anawapa makavu kwa hasira). Pia kwenye kuuminya upinzani wanafanana.

Magufuli wala alikuwa hana mpango wa kupeleka reli Rwanda haraka hivyo. Safari ya Kagame ya siku moja imemfanya hata Magufuli akasema "Kwa kile kipande cha kule Nzasa kuelekea Kigali tutaangalia tunachangiana vipi. Tunachangiana? Kwanza hatuhitaji kufanya biashara na wanyarwanda maana tunawajua!

Swala la miaka saba kamwe halitengani na Magufuli! Ni aina ya kiongozi wa miaka saba na hilo litatekelezwa. Ndiyo maana aliwapigia simu kina Kafulila na Lowassa warudi CCM, Lissu aliwekewa target yake Mungu akaepusha, wengi wameminywa ili hilo litakapoletwa hadharani lipite kiulaini.

Miaka saba siyo ajenda ya Juma Nkamia bali ni ajenda ya CCM. Isingekuwa ajenda ya CCM basi Nkamia angeshaonywa hadharani. Kule Zanzibar tayari wameshaisema. Hivyo ilishajadiliwa sirini na itatekelezwa. Dodoma pale Magufuli atadumu sana. Tunaanza na miaka saba baadaye tunaondoa ukomo wa kugombea. Ndiyo aina ya uongozi wa kula nyama za watu! Utaanza na damu, utachagua baadhi ya maeneo utaendelea kunogewa na hatimaye utaupenda mwili mzima wa binadamu.

Tuko naye! Tukimshindwa basi hatuna jinsi zaidi ya kuvumilia liende. Kama huzioni dalili za mtu kutawala maisha (Siyo miaka saba maana ni kianzio tu cha kumla binadamu) Basi unahitaji miwani!

Hiyo miaka saba anayoitaman ana uhakika gani na sekunde iliyopo mbele yake!? Asizan wanaokufa ni wakosaji, nae anaweza kufa saa na wakati wowote, aondoke na ndoto yake ya kutukandamiza. Hiyo miaka saba hapana, wala haifai!!!
 
Tunataka maendeleo. kama maendeleo yanakuja kwa style hiyo Basi atawale milele. Democrasia bila uchumi na maendeleo ni sawa na jehanamu. Go Magu we support you.

Harooo! Ukiona hivi basi ujue huyu jamaa anakula kuku kwa mrija maana yuko connected na anafaidi kutokana na mfumo uliopo!!

Go Magu I say Go, but kumbuka kuna katiba, kumbuka demokrasia ni muhimu.
Go Magu, just Go wengine waishi kama malaika, wengine kama mashetani.;):(o_O
 
Kama kweli tunataka Mheshimiwa sana awepo miaka saba kwa muhula mmoja, tufanye tathimini za kiuchumi na kisiasa kwa miaka miwili ya utawala wake. Je, ajira kwa watanzania zimeongezeka au zimepungua kutokana na kufungwa kwa baadhi ya kampuni? Uwekezaji kwa wajasiriamali wadogo wadogo ukoje na je kuna ahueni?
 
Kama Mzee akiongezewa muda wa kubaki kwenye power halii itakuwa ngumu na watu wengi sana watakuwa wakipotea ktk mazingira ya kutatanisha!
 
Umethibitisha umimi wako. Siye kila mwenye hoja tofauti na yako ni Lumunba. Uwe na mawazo mapana na chanya, ukikubali kusikiliza na kujadili mawazo ya mtu mwingine. Hiyo ndiyo demokrasia, pia ukomavu wa akili
Demokrasia ndani ya nchi ya ccm??
 
Lengo lao ni kuhakikisha ngosha anakuwa Rais wa maisha chini ya ccm. Huu ni mpango ulosukwa kwa kipindi kirefu.
Mtakoma kwani mlitaka Iweje. Majingamajinga nyie rais kalitolea ufafanuzi lakini bado mnamlisha maneno. Kupeleka SGR Rwanda ni matakwa ya kibiashara na pia ile nchi ni landlocked haina jinsi lazima Tanzania iihudumie kwa kuwezesha. Rwanda ni walipa kodi wetu hatuwezi kuwaacha. Hata DRC hatuwezi kuwaacha. Hata Burundi na Uganda. Mawazo yenu ya kiataahila mnaweza kimakalio tuuuuuu
 
Tunataka maendeleo. kama maendeleo yanakuja kwa style hiyo Basi atawale milele. Democrasia bila uchumi na maendeleo ni sawa na jehanamu. Go Magu we support you.
Halikadhalika uchumi bila Demokrasia, ni sawa na bomu lililotegwa, linasubiri sekunde tu zitimie ili lilipuke.
 
Mtakoma kwani mlitaka Iweje. Majingamajinga nyie rais kalitolea ufafanuzi lakini bado mnamlisha maneno. Kupeleka SGR Rwanda ni matakwa ya kibiashara na pia ile nchi ni landlocked haina jinsi lazima Tanzania iihudumie kwa kuwezesha. Rwanda ni walipa kodi wetu hatuwezi kuwaacha. Hata DRC hatuwezi kuwaacha. Hata Burundi na Uganda. Mawazo yenu ya kiataahila mnaweza kimakalio tuuuuuu
Muda utaongea, wewe tulia tu maana utalazimika kuja na utetezi mwingine.
 
CCM sio nyepesi hivyo mnavyodhani.

CCM ina demokrasia ya aina yake.

Rais mwenyewe ameshakanusha hadharani.
Kama rais amekanusha basi watanzania wamemwelewa sana.
Na bahati nzuri watanzania wengi wanampenda Magufuli lakini hawaipendi CCM.
Zoezi lolote litakalofanywa na CCM litaleta chuki na halitafanikiwa kwa kua tu lina hila nyuma yake na watanzania wanalijua hilo ndio maana unapowakutanisha CCM na Watanzania wanyonge basi ni lazima moto uwake mana haikubaliki labda kwa mabomu.

Zoezi la kubadili muda wa rais kukaa madarakani halitaungwa mkono na CCM kwani wanajua fika kuwa nguzo zao zitajitoa na jumba litaanguka.
Nguzo kuu ya CCM ni viongozi wa dini.

Hakuna viongozi wa dini watakaounga mkono mbinu hiyo ya kulipeleka Taifa kwenye maafa bila sababu.

Mkamia kwa mtizamo wa haraka haraka ni mtu wa ajabu na asiyejali mustakabali wa uhai wa watanzania zaidi ya kuona kuwa anakaa muda mrefu bungeni.
Dunia nzima kuna vurugu kutoka na tamaa ya watawala kukaa madarakani muda mrefu kwa kujiona kuwa mawazo yao ndiyo yanayofaa kufuatwa na kuminya uhuru wa wananchi kujadili na kuweka wazi utendaji wao.
Mkamia anataka kuliteketeza taifa hili ambalo waliopita waliepuka tamaa hiyo ya kuongeza muda.
Mkapa aliombwa sana lakini alikataa.
Na wakati Mkapa anaondoka upinzani ulikua umekaribia kufa kabisa ndio maana JK alipata kura 82% kutokana na jinsi Mkapa alivyokuwa ameiunganisha CCM kisiasa na pia uimara wa uchumi wa nchi. Hata hivyo suala la kuongezewa muda alilikataa kama alivyokataa Magufuli mwenyewe.

Kuna wapumbavu na Malofa wanaoilinganisha Rwanda na Tanzania (Tanganyika na Zanzibar)
Hii ni nchi ni Muungano wa nchi Mbili zilizokua na uhuru kamili.
Ina historia yake.
Ni nchi kubwa yenye makabila 125 makubwa yaliyokuwa na historia na watawala wake wa kitemi na himaya zake.
Sio kale kanchi ka Rwanda kenye vikabila viwili ambavyo kakabila kamoja kanamaliza kakabila kengine ili katawale milele. Sio kwa Tanzania. Ni huko huko kwa Kagame na historia zao za mauaji.

Tanzania hatuna historia ya kuua watu kwa dhulma kama Rwanda.
Tuna historia ya kutumua nguvu zetu na damu zetu kutetea haki na uhuru wa wanadamu popote duniani.
Sio Rwanda wanaotumia nguvu zao na damu zao kupora uhuru na haki za watu wengine kama wanavyofanya kule Kongo DRC.
Rwanda ni kanchi kaovu.
Rwanda ni kanchi ka kijambazi ,kanakoendesha uchumi wake kwa hila na wizi wa mali za wakongo.

Kuna wapumbavu na malofa wanashinda usiku na mchana kuidifia Rwanda bila kutambua kuwa wanasifia wahalifu na wezi wa Mali za wakongomani.
Tanzania chini ya viongozi wenye utu kama Mwalimu JKN tuliipiga Uganda na kuikalia kwa muda lakini hatukupora rasilimali zao.
Tuliwateka askari wa Libya lakini hatukuhitaji fedha zao kwa ajili ya kubadilisha maisha ya watu na fedha za Walibya,tulijali utu na heshma ya mwanadamu.
Tumewasaidia wakongomani kwa muda Mrefu lakini hatukupora madini yao kwa ajili ya kujenga uchumi wetu bali tulijali utu wa wakongomani.

Tungeamua kuivamia Kongona kupora madini yao tungeweza.

Ni aibu kubwa kulinganisha utajiri halali wa mfanyabiashara na utajiri haramu wa jambazi.

Kama kuna watu( Wapumbavu) wanaotaka kuilinganisha Tanzania na Rwanda kiuchumi basi ni Malofa.

Haina uchumi unaolingana na hata Jiji la Dsm wala Mkoa wa Mbeya.
Hii nchi ina Rasilimali nyingi sana.

Ukiwachukua watu wa Kilimanjaro pekee wana utajiri mkubwa kuliko nchi ya Rwanda.
Rwanda hakuna Tajiri hata mmoja kama Regnald Mengi. Hayupo.

Rwanda hakuna mtu mmoja mwenye uwezo wa kumiliki Mabasi 100 ya ya SCANIA marcopolo.. Hayupo. Ni lazima ashirikiane na watawala na serikali mana hilo soko hawana.
Rwanda ni kama kupe na Tanzania ni ng'ombe. Huwezi kumlunganisha kupe na ng'ombe. Utakua ni ulofa.

Nchi hii ina rasilimali nyingi sana na kuziwekea mazingira ya kuzifikia kwa uhakika inahitaji fedha nyingi sana kwa hiyo kwa muda mfupi tu haiwezekani . Miundo mbinu inayojengwa Tanzania nzima kwa Rwanda ni kama wilaya ya mkoa mmoja tu wa Dsm wenye watu miioni 6 wanaopata umeme ,maji, afya, elimu ,na biashara.
Ukiilinganisha Rwanda na Tanzania ni lazima uweke mahaba pembeni utuambie kuwa barabara za lami na reli kwa nchi nzima ya Rwanda ni Km ngapi na Tanzania ni km ngapi!

Mfumo wa Kuganda madarakani unafaa na unatosha kuishia huko kwa hao wanaoendekeza ukabila huko Rwanda na sia Tanzania.

Mfumo wa Rwanda umejengwa juu ya misingi ya mafuvu na damu za watu.
Mfumo wa Tanzanua umejengwa juu ya hekima ,utu, umoja ,amani, ujamaa, undugu, upendo, hekima na busara za waasisi wetu.

Hatuwezi kuruhusu mufumo inayojengwa kwa damu iingie Tanzania.

Ili kiongozi yeyote aishi kama Kagame ni lazima awaangamize wale wenye ndoto za kweli za kuwa marais.
Hatutaki nchi yetu ielekee huko.
Atakuaja kutokea kiongozi mbovu halafu tutajuta sana.
Hatutaki kujuta bila sababu.
Kama rais tuliye naye anafanya vizuri basi atimize aliyaoahidi kwa katiba hii hii ndani ya muda wake akistaafu tutamuenzi kama kawaida na atapata thawabu yake kwa m
Mungu na uzuri hatuna tabia ya kuwachukia au kuwatukana wastaafu.
Nchi yetu imejengwa kwenye misingi hiyo ya kuwaheshimu wastaafu wetu.

Kwa hiyo wale wanaotaka kutuletea mifumo ya kuganda madarakani , mifumo miovu inayotawaliwa na ubabe ,ukabila ,udini ,ufamilia,urafiki na undugu watambue kuwa haitufai kabisa ,Mh.Rais wetu Mpendwa ameshakataa hadharani mara mbili.
Kwa hiyo mkamia aache kupinga kauli ya Rais.
Rais anaijua historia ya nchi hii vizuri kuliko hao wapambe wanaotizama matumbo yao tu .
Afadhali umewaelimisha hawa malofa kazi yao kumfitinisha rais wetu.kwanza Rwanda ina square kilomita 26,000 wakati mkoa wa shinyanga una kilomita za mraba 51,000 ni aibu kulinganisha TZ yenye square km 954,000 na kijiji cha Rwanda.. Kwa taarifa yao hao malofa ukubwa wa TZ ni ukubwa wa Kenya + Uganda +Burundi + Rwanda .Jumla yao haijaifikia TZ bado inawazidi kwa Square km 61,000.MalofA wajisomee siyo kushinda na keyboards bila ufahamu. Tanzania ni baba lao EAC
 
Democracy,anaesema mitano yupo sahihi, anaesema kumi yupo sahihi,anaesema Saba pia yupo sahihi,
Si ndio Democracy?
Wananchi ndio waliamua iwe mitano,wakaweka kwenye katiba katika wakati wao,kama wananchi wa sasa wanaona kunafaa kuwepo na mabadiliko iwepo referendum tu...
Democracy inatabia ya kuheshimu ata maoni ya wachache....mifano hai ipo.

eleza referendum ya vyama vingi 1992, nini matokeo yake na je yaliheshimika?
 
Muda utaongea, wewe tulia tu maana utalazimika kuja na utetezi mwingine.
Acha Magufuli awanyooshee mlizoea kuishi kwa kupiga mizinga ndugu zenu. Sasa hivi ni kazi tu.Tafuteni uzushi wooote lakini ngosha yuko kwenye mstari ulionyooshwa kwa rula
 
Matokeo yanasema kuwa hatimaye rais Magufuli ataongoza hadi 2022. Tumeshaona wanataka nini, nani anasukuma hili na kwa nini?

Haya ni matokeo ya ushawishi wa rafiki yetu kipenzi Paul Kagame.

Rais Magufuli amefanana na Kagame pengine kwa kila kitu! one man show, ukaliukali (Kagame aliwahi kupiga mtu hadharani, nadhani hii haitakuwa habari ya kushtukiza kama yule naye atafanya hivyo! Anawaita wapumbavu, anawachana kama alivyoenda nao bandarini, akiwa nao ikulu anawapa makavu kwa hasira). Pia kwenye kuuminya upinzani wanafanana.

Magufuli wala alikuwa hana mpango wa kupeleka reli Rwanda haraka hivyo. Safari ya Kagame ya siku moja imemfanya hata Magufuli akasema "Kwa kile kipande cha kule Nzasa kuelekea Kigali tutaangalia tunachangiana vipi. Tunachangiana? Kwanza hatuhitaji kufanya biashara na wanyarwanda maana tunawajua!

Swala la miaka saba kamwe halitengani na Magufuli! Ni aina ya kiongozi wa miaka saba na hilo litatekelezwa. Ndiyo maana aliwapigia simu kina Kafulila na Lowassa warudi CCM, Lissu aliwekewa target yake Mungu akaepusha, wengi wameminywa ili hilo litakapoletwa hadharani lipite kiulaini.

Miaka saba siyo ajenda ya Juma Nkamia bali ni ajenda ya CCM. Isingekuwa ajenda ya CCM basi Nkamia angeshaonywa hadharani. Kule Zanzibar tayari wameshaisema. Hivyo ilishajadiliwa sirini na itatekelezwa. Dodoma pale Magufuli atadumu sana. Tunaanza na miaka saba baadaye tunaondoa ukomo wa kugombea. Ndiyo aina ya uongozi wa kula nyama za watu! Utaanza na damu, utachagua baadhi ya maeneo utaendelea kunogewa na hatimaye utaupenda mwili mzima wa binadamu.

Tuko naye! Tukimshindwa basi hatuna jinsi zaidi ya kuvumilia liende. Kama huzioni dalili za mtu kutawala maisha (Siyo miaka saba maana ni kianzio tu cha kumla binadamu) Basi unahitaji miwani!
Katika hili Kikwete anapaswa kulaumiwa kwa kukubali jina la huyu jamaa kupitishwa kuwa mgombea. Hii dhambi na yeye itamuhusu.
 
Acha Magufuli awanyooshee mlizoea kuishi kwa kupiga mizinga ndugu zenu. Sasa hivi ni kazi tu.Tafuteni uzushi wooote lakini ngosha yuko kwenye mstari ulionyooshwa kwa rula
hakuna marefu yasiyo na ncha, ndio maana nikakwambia muda utaongea. Hata yule awanyooshaye wenzie hawezi wanyosha milele. Utafika wakati atafikia kikomo tu, na asipokuwa macho anaweza kuta na yeye zamu yake ya kunyooshwa inaingia.
 
Katika hili Kikwete anapaswa kulaumiwa kwa kukubali jina la huyu jamaa kupitishwa kuwa mgombea. Hii dhambi na yeye itamuhusu.
Kwani kikwete ndiyo alipitisha peke yake? Poleni kumbe hata utaratibu uliotumika hamjui. Viva JPM
 
Back
Top Bottom