Tunaogopa nini kuruhusu uraia pacha?

Tunaogopa nini kuruhusu uraia pacha?

Hizo nchi zaidi ya 50 zilizoruhusu zimepungukiwa nini!! Au uliwasikia wakilia na kulalamika!! Mkuu, uraia pacha una manufaa sana sana, refer Kenya n.k

Kenya unarefer kwa Lipi mkuu kibera au idadi kubwa ya watu wasio na ardhi. Wakenya wangapi wako tayari kufundisha kwa ujira ambao watanzania hawawezi kukubali.
 
Bila Shaka nyingi ni wale wa kutoka chama cha kijani wenye kauli mbiu ya 'zidumu fikra za mwenye kiti '

Ruhusuni uraia Pacha wabongo waje kuwekeza nyumbani,achaneni na mawazo yaliyofubaa hayo
Kuna fursa nyingi sana nje ya nchi, na zingine ili ufaidike zaidi na kuwezesha ndugu na jamaa zako pia wafaidike inakuwa rahisi kuchukua uraia wa hiyo nchi, bila kupoteza uraia wa nyumbani. Na pia kwa nyumbani, ili kuwekeza bila usumbufu au kumiliki arhi na mali zingine ni lazima uwe raia. Ndiyo maana diaspora wengi wanahitaji hiyo opportunity. Its a win-win situation
Ndugu yangu huko Tz wananchi bado wamefubazwa na mawazo ya siasa zile za kikomunisti... kupenda kufungia watu ndani wasipate fursa zilizopo nje na hata ku explore na kuzitumia kusupport maendeleo ya nchi zao , kwa sababu finyu za eti uraia pacha ni kuhatarisha usalama wa Taifa..... mara sasa waziri anasema hiyo haipo kwenye katiba sijui..( kwani katiba haiwezi rekebishwa kuruhusu hili).....yaani kwa mawazo hayo mgando bado naona Tz bado tuna safari ndefu kufikia kupata maendeleo endelevu aiseee....... tuendelee kula mtori, na nyama ziko chini..
 
kwa nini uone aibu ya kuwa mtanzania?
 
Sijui Tanzania tunaogopa nin kuruhusu uraia Pacha, Watanzania wengi huko ughaibuni wanataman kuwekeza Nchini kwao wengine wana vipaji vya mpira, Music, Riadha n.k wanataman wachezee kwenye nchi yao Tanzania..

Tunakwama wapi km Taifa kuruhusu uraia pacha, Unahisi nin kikwazo kwenye hili?
Nani anawazuia kuwekeza? Nani kawazuia kuchezea Yanga? Kama ana wazazi wake hapa, nani kamzuia kuja kuwatembelea na kuwajengea Masjid?
 
Wasioelewa umuhimu wa uraia pacha ni wale waliojifungia ndani ya nchi tu bila kutoka nje kujionea majirani wanaishije. (Lack Of Exposure)
Kwani kwenda Ulaya kumeanza leo? Nyerere alisoma wapi? Lipumba alisoma wapi? Samia alisoma wapi? Fr Pengo alisoma wapi? Kwa nini hawakubaki huko?
 
katika uraia wa nchi zoote hakuna raha kama kupata uraia wa United arab emirates hasa abudhabi, nimeishi huko mpaka wazungu wanakubali kuwa raia hao wana enjoy, kuna mtanzani mmoja raia wa emirates alikuwa jeshini alikuwa na cheo akastaafu ninafahamiana nae kila mwezi analipwa dirham elfu 90. nyumba kapewa bure watoto wanasoma bure kuanzia chekechea mpaka chuo nje ya nchi ni bure. matibabu nje ya nchi bure,
 
Hizi Kelele zote za uraia Pacha ni sababu ya kuwezeshwa kumiliki ardhi..

Hakuna kingine.

Serikali iendelee kubana hapo hapo.
No uraia Pacha.
Ardhi inamilikishwa na serikali, siyo kila anayekujwa kuonba ardhi huipata hata kama ni raia. Kuna wale ambao walichukua uraia wa nje wakati tayari wana ardhi Tanzania ama ya urithi au waliyopta kwa mujibu wa sheria kabla hawajahamia ughaibuni; watu hao waruhusiwa kuendelea kutumia ardhi hiyo kama watanzania wengine hasa pale inapokuwa wazi kuwa bado ardhi hiyo imekuwa inatumika kama ilivyopangwa.
 
Nani anawazuia kuwekeza? Nani kawazuia kuchezea Yanga? Kama ana wazazi wake hapa, nani kamzuia kuja kuwatembelea na kuwajengea Masjid?
Wanachoogopa ni vichwa vya uhakika kurudi Tanzania na kukualika vikawapora "circle" yao ya utawala na wakawa hawana uwezo wa kuwa "harass" na kuwafunga/goa wsapendavyo. Hakunza zaidi.

Tanzania ina vichwa vingi nje vyenye asili ya utawala na si utawala wa kugombea bali wa asili.

Hilo ni tishio kubwa sana na wanalijuwa hilo. Wanataka mali zao lakini hawataki hekima zao.
 
Bila Shaka nyingi ni wale wa kutoka chama cha kijani wenye kauli mbiu ya 'zidumu fikra za mwenye kiti '

Ruhusuni uraia Pacha wabongo waje kuwekeza nyumbani,achaneni na mawazo yaliyofubaa hayo
Kwanini wasiendelee kuwekeza hukohuko waliko? Je mbona Kuna wageni kibao wanawekeza bongo bila kuwa na huo uraia pacha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kwenda Ulaya kumeanza leo? Nyerere alisoma wapi? Lipumba alisoma wapi? Samia alisoma wapi? Fr Pengo alisoma wapi? Kwa nini hawakubaki huko?

kusoma na kuishi ni vitu tofauti
 
Chagueni Kama mnataka uraia pacha bila ardhi hata leo mnapata.

Wabongo wengi bado Ni wapumbavu, ukiacha ardhi watu watageuka wapangaji ndani ya nchi yao ndani ya SAA 24 tu.

Halafu wataanza kulaumu CCM

This might be true.
 
Bila Shaka nyingi ni wale wa kutoka chama cha kijani wenye kauli mbiu ya 'zidumu fikra za mwenye kiti '

Ruhusuni uraia Pacha wabongo waje kuwekeza nyumbani,achaneni na mawazo yaliyofubaa hayo
Kwani bila uraia pacha wanazuiwa kuwekeza??
 
Sijui Tanzania tunaogopa nin kuruhusu uraia Pacha, Watanzania wengi huko ughaibuni wanataman kuwekeza Nchini kwao wengine wana vipaji vya mpira, Music, Riadha n.k wanataman wachezee kwenye nchi yao Tanzania..

Tunakwama wapi km Taifa kuruhusu uraia pacha, Unahisi nin kikwazo kwenye hili?
Bangi imeshindikana sembuse uraia pacha?
 
Diaspora akili zao zipo fresh awaathiriki na moshi wa mwenge ccm inaogopa watawaamsha watz.
Uraia pacha ni ajenda ya Dunia haikwepeki, dunia inakwenda kuwa moja mbeleni huko mipaka itaondolewa Ili kuleta free movement ya watu baada ya watu wote duniani kuwekwa kwenye system moja. Tutaitwa global village dunia moja.
Makao makuu ya dini moja duniani yashajengwa, kwa ujio wa dini moja inayoitwa Chrislam.
Uraia pacha haikwepeki.
 
Umesha athirika sana kiakili kwasababu umechagua kusikia ujinga
 
Nani anawazuia kuwekeza? Nani kawazuia kuchezea Yanga? Kama ana wazazi wake hapa, nani kamzuia kuja kuwatembelea na kuwajengea Masjid?
Hiyo masjid imeingiaje hapo mdini wewe
 
Back
Top Bottom