Tunaofatilia Sultan tukutane hapa

Inasemekana ni true story ilitokea hivyo, Sultana Hurett Mke wa Mfalme alikuwa na chuki kubwa na waziri mkuu Ibrahimu Pasha ,hivyo alijaribu fitina nyingi akosane na Mfalme Suleiman. Nadhani alichangia sana kuanguka kwa himaya hiyo ya Ottoman.

Kifo cha pasha kilichangia? Au mke wa sultan alichangia kuanguka kwa himaya hio?
 
Sio itakuwa kahasiwa ni kweli kahasiwa, yeye, gula, kilaza, urojo ndio kanuni za harem yao.

Inachoniboa tamthilia mtunzi amependelea sana hurrem japo ni Sterling amechezesha kama asieshindwa. Alafu anamchezesha pasha kama zumbukuku kwenye maamuzi ya kila simu ya maisha wakati huo huo anamchezesha kama mwenye akili nyingi sana katika utawala na ndie amemsaidia Suleiman kufika aliko.

Kwa mfano, juzi hurem kamuwekea majambazi wamuue lakini kafika kwa sultan hamwambii ukweli. Sawa tukubali anaona suleman asikii aambiliki kwann asimuombe Rafiki yake waweke mtego ajue sura halisi ya Hurem. Hapo ndipo inaboa japo ndio kufanikiwa kwa mwandishi kutuudhi.
Ila kumbuka ile ni storia ya kweli iliyowahi kutokea sio kwamba eti hurrem kapendelewa hapana ndivyo ilivyokuwa kwenye maisha ya kweli
 
Sultan imefikia patamu, Je Mfalme Suleiman yupo Salama!? Sultana Hurrem usiemtaka anakuja.
 
prezidaa wa uturuki anataman saana kuirudisha ottoman lkn moja kati ya majirani zake wa karibu vichwa ngumu ni urusi na israel
 
Kifo cha pasha kilichangia? Au mke wa sultan alichangia kuanguka kwa himaya hio?
Kifo Ibrahim Pasha, kilichangiwa sehemu kubwa na fitina Sultana Hurrem,akitamani apandikize waziri mkuu mtii kwake. Pengo Ibrahim Pasha limepunguza amani Familia ya mfalme pia utawala pia.
 
Back
Top Bottom