Tunaodate na wanaume ambao hawajatusua bado

Tunaodate na wanaume ambao hawajatusua bado

jamani naombe mtupe moyo na maneno ya faraja ili kuvumilia changamoto kwa sisi ambao tunadate na wanaume ambao hawajatusua bado.

wa kwangu nimemaliza nae chuo,wote tunasaka ajira na pia tunaangalia na upande wa pili.

kuna wakati kama mwanamke unapata vishawishi kutoka kwa wanaume wenye pesa zao lakini unapiga moyo konde tu na kusali mana ukimwangalia mwenzako ndo hivo unampenda na kanafsi kanakusuta flani ukiwaza kufanya hivo.

wakati mwingine unakaa na kuwaza mh isije kua nakosa bahati

pia unaweza skia shuhuda za wanaume kibao walokuja kuwatenda wanawake zao baada kupata vijifedha kidogo.

nb: simanishi kwamba ni tegemezi no ila unakuta wote mmechalala maskini ya Mungu hakuna hata wa kumpiga tafu mwenzie

pia kwa mwenye shuhuda aweke hapa, ambae alimvumilia mwanaume wake since hana kitu na wakaend up pamoja as mke na mume hadi leo
Mama Hata Roman empire haikujengwa siku moja,shikamaneni hivyo hivyo,
Pili,mdogo wangu kwenye maisha,hakuna garantii,yaani uwezi kujua kwa uhakika,kama hapo ilipo umepatia,au umeramba galasa,kitu pekee kwenye maisha chenye uhakika wa kutokea ni Kifo tu,
Mambo mengine,ni Ku take risk tu,na bila Ku "take risk" uwezi Fanya chochote maishani,
Na kumbuka,maamuzi unayoyafanya sasa HV,kuhusu nyanja yoyote ya maisha,mapenzi,kazi,elimu,yana mchango mkubwa mahari utakapo kuwa kesho,
Trust your self Girl!!! Go with ur gut fillings
 
Poleni jamani kudate mwanaume asie na kazi ni changamoto
 
hiyo mada ilikua changamsha genge mkuu,hakuna mwanamke asiyetongozwa
Inabidi sometimes uwe realistic mana hata sasa hivi watu wata dhani ni changamsha genge.
Ok ngoja tuendelee kuburudika
 
Na wanaume tuwe makini ukiona mdada anaanza kuulizia kazi yako saana ujue anakupigia hesabu...utashangaa umepewa mimba tu
 
jamani naombe mtupe moyo na maneno ya faraja ili kuvumilia changamoto kwa sisi ambao tunadate na wanaume ambao hawajatusua bado.

wa kwangu nimemaliza nae chuo,wote tunasaka ajira na pia tunaangalia na upande wa pili.

kuna wakati kama mwanamke unapata vishawishi kutoka kwa wanaume wenye pesa zao lakini unapiga moyo konde tu na kusali mana ukimwangalia mwenzako ndo hivo unampenda na kanafsi kanakusuta flani ukiwaza kufanya hivo.

wakati mwingine unakaa na kuwaza mh isije kua nakosa bahati

pia unaweza skia shuhuda za wanaume kibao walokuja kuwatenda wanawake zao baada kupata vijifedha kidogo.

nb: simanishi kwamba ni tegemezi no ila unakuta wote mmechalala maskini ya Mungu hakuna hata wa kumpiga tafu mwenzie

pia kwa mwenye shuhuda aweke hapa, ambae alimvumilia mwanaume wake since hana kitu na wakaend up pamoja as mke na mume hadi leo
Asikuongopee mtu hakuna formula mahususi kwenye hilo. Hii ni pata potea (probability). Kuja kuwa mke na mume kuna factors nyingi sana na nyingine ni confounders kama vile pesa, dini, elimu, uzuri, ukaribu na umbali, kabila, tabia, elimu, aina ya kazi, ushawishi wa wazazi, umbile, afya, mihemko, ulaghai, ushawishi, lazima za wazazi na ndugu, usafi, mapishi, ujuzi wa kitandani, ahadi kabambe, familia ya mtu, bahati, nyota, nk. Vyote hivi vinaweza kuleta mageuzi kwenye mapenzi wakati wowote. Atakayekuwa mume wako ni yule atakayeonyesha juhudi na maendeleo ya wazi na haraka ya kuelekea kwenye kufunga ndoa na wewe yaani kujitambulisha, kuvalishana pete, kutoa mahari, vikao, tarehe ya matukio na kuoana. Siku zote ni lazima uone progress ikipigwa kuelekea kufunga ndoa sio maneno maneno tu ya kila siku.
 
Back
Top Bottom