mgeni wenu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2012
- 3,664
- 1,731
Kumbe mpo wengi msio na shukrani na msiotambua mambo bwelele ambayo Kikweye kawafanyia. Jamani karudisha 'chenji ya rada' hamshukuru?
Kumbe mpo wengi msio na shukrani na msiotambua mambo bwelele ambayo Kikwete kawafanyia. Jamani karudisha 'chenji ya rada' hamshukuru?
Ukweli wa mambo ni kuwa kawaida ya wananchi ni kulaumu pale serikali inapofanya makosa na si kazi yetu kusifia inapofanya vizuri kwa sababu kubwa moja, tulichagua serikali ili ifanye mazuri na si vinginevyo.
Shida ya Dk Kikwete na viongozi wengi wa ki-afrika(au dunia ya tatu?) ni kupenda kusifiwa kwa 'mazuri' waliyofanya na kukataa lawama kwa mabaya yao kwa kisingizio kuwa 'wameshauriwa vibaya na wasaidizi wao'. Sifa njema wapate wao lakini lawama wapate wasaidizi!!! Dk Kikwete ameangukia katika mtego huo kama wengi wengine kabla yake...Mh Mkapa, Shekhe Ali na Mwalimu Julius.
Katika mtego huo wamekataa kutambua na kukubali kuwa wao kama kichwa basi vyote lawama na sifa ni stahiki zao lakini wakipaswa kuzingatia kwamba kufanya uzuri ni wajibu usiohitaji sifa(isitoshe ni ahadi za kampeni zao siyo?) na upuuzi wao ni lazima uendane na lawama chungu tele.
Mfano wa uzembe na upuuzi wa kichwa ni pale kinapohitaji ushauri kutoka kwa kiganja ili kuufanya mwili utekeleze wajibu wake (soma: mkuu wa nchi kusubiri kamati kuu ya chama impe baraka za kuwashughulikia wezi na wabadhirifu wenye kujinasibu kuwa hawawajibiki kwa chama bali mkuu wa nchi kama mmoja wa watuhumiwa alivyonukuliwa na gazeti la mwananchi la jumatatu tarehe 30/04/2011).
Huo ni uzembe ambao hauwezi kusahaulika wala kusameheka na kwa kweli ni uzembe ambao umeigharimu sana serikali ya Dk Kikwete na hasa umaarufu wake binafsi na chama chake.
Pengine kama kuna kitu ambacho bwana mkubwa Kikwete tutamkumbuka na kwa kweli kimetufikisha hapa pa kusema pasi na woga ni kukuza uhuru wa kujieleza...pamoja na kejeli zake pale awali kama vile kelele za mbu hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi, kwa kweli nafuu ipo kinyume na ilivyokuwa wakati wa Mr ANBEM co-founder(mh Mkapa ukipenda muite Mr Kiwira), Mzee Ruksa au Mwalimu.
Walau sasa tunaongea kwa uhuru mkubwa tu...kwa hili pongezi Rais wangu, mheshimiwa, Dk, Luteni Kanali Mstaafu J.M. Kikwete.
Nawasilisha.
yeye anayo nyembamba!Suppose anastahili shukurani na hashukuriwi.
Yeye aligombea urais ili ashukuriwe?
Siye Kikwete huyu huyu anayesema uongozi unataka ngozi nene?
Kumbe mpo wengi msio na shukrani na msiotambua mambo bwelele ambayo Kikwete kawafanyia. Jamani karudisha 'chenji ya rada' hamshukuru?
Humjui Kikwete.
Laiti ungemjuwa usingeleta pumba ulizozileta.
Ni hotuba ipi aliyonung'umika kama utakavyo iwe?
Hotuba za Kikwete zote, ni fundisho kwa watu kama wewe wanaolalamika na kunung'unika kila siku lakini mnachonung'unika hakijulikani.
Hotuba aliyoongea na wazee kuhusu madaktari, licha ya kuwaelewesha kilichojiri, alitamba sana na hata kukejeli. Na mpaka leo tumeona madaktari ni kimya na wala hutowasikia tena wakilalamika. Huyo ndio JK.
Hotuba ya juzi umeona alivyowanyamazisha kwa kukurupuka na kudakia hoja kwa mafanikio ya jitihada zake.
Kikwete, hakupewa "favor" kuupata Urais kama ilivyokuwa kwa wote wa kabla yake. Kikwete alijuwa kabisa kuwa anataka awe Rais na alijipanga hivyo kwa miaka mingi sana na akaupata licha ya kuletewa mizengwe na Nyerere katika uhai wake.
Nakuona una haha kutafuta la kusema kuhusu Kikwete lakini ukweli ni kwamba hamumuwezi kabisa, kila afanyacho hufanya kwa maslahi ya wananchi na si ya kwake binafsi. Leo hii kikwete angekuwa na madudu japo asilimia 1 tu ya madudu ya Mkapa sijui kama angebaki kwenye Urais, maana mlivyomsakama si kidogo, lakini hamna zaidi ya kuzuwa tu na kutafuta kisichopo, mtatafuta sana lakini bure tu.
Humjui Kikwete, unamsikia tu na unamkisia, he is way too far ahead from your way of thinking. Wewe bado una fikra za kizamani sana, za wakati wa dhiki za chai kukorogwa kwa lawalawa badala ya sukari.
Mnajionea nafsi zenu wenyewe na ndio mpaka zinawafanya mnakuja kubwabwaja hapa hapa, ati "tunamuonea Kikwete", una ubavu upi wewe wa kumuonea Kikwete?
Humjui Kikwete1
He has failed to kick the ball to the net...he himself is the 1st problem...he is very unbelievable with what he promises...ataahidije kupunguza mfumuko wa bei wakati ameshindwa kutimiza ahadi zake za uchaguzi? Is that practical? Ameahidi mishahara kupanda wakati serikali yake inaishi kwa vimikopo vya barclays na wengine? Ameshindwa kuchukua wajibu wake kama aliyeteua na kudai anasupport bunge? Is he really serious? Anaogopa kila mtu! Hana priorities! Amekuwa situational leader...kazi kuchekacheka tu na kutafuta misiba iliko. Ameamua kuplay uswahili wakati taifa linaangamia. Kweli watz tulijiwekea mzigo...na haki ya nani hatuna rais...subiri baraza atakaloteua, utachoka na roho yako!
TatiZo ni kwamba aliamua
taasisi ya urais iwe mikononi mwa Familia yake,pia waliomzunguka
hawampi tathmini ya utawala wake,hiyo inamfanya akose kabisa uhakika na
akkifanyacho,naendelea tu kumpa moyo angalau ka muda alikobakiza
akatumie kuaga kila wilaya japo hata hajashukuru kwa kupewa kipindi cha
pili cha uongozi wake
Hapo kwenye red hapo....
Hotuba zake tatu za hivi karibuni zimejaa manung'uniko na malalamiko ya mtu ambaye haeleweki, hapendwi, hasifiwi au ambaye hashukuriwi. Hotuba yake kwa wazee wa CCM wa Dar-es-Salaam baada ya mgogoro wa madaktari na hotuba yake ya Mei Mosi mbele ya wafanyakazi kule Tanga zinatuonesha hisia za mtu ambaye wananchi wake inaonekana hawamshukuru vya kutosha.
Katika hotuba zote tatu Rais amejaribu kutuonesha ni jinsi gani amejitahidi kufanya mambo kadha wa kadha ambayo kwa kweli watu wangemshukuru kuwa ameyafanya lakini inaonekana hashukuriwi. Ni hotuba ambazo zimejaa "tenda wema nenda zako" nyingi. Madaktari hawamshukuru, wafanyakazi hawamshukuru, wapinzani hawamshukuru, na hata wana CCM wenzake yawezekana hawamshukuru. Lakini pia kwenye hotuba ile ya mambo ya nishati ambapo alisifia serikali yake kufanya mengi katika kuzalisha umeme nchini kuliko serikali zilizomtangulia nayo pia ilijaa kutokuwa appreciated.
Ndio sababu najiuliza ni kweli yawezekana Rais Kikwete anaona Watanzania hawamshukuru vya kutosha na kuappreciate vitu alivyovifanya? Ni kweli Kikwete amefanya makubwa sana ambayo anapaswa kushukuriwa kwayo? Ni kweli kwamba Watanzania wanambebesha lawama kwa kumuonea tu japo "amejitahidi" sana kufikia malengo mbalimbali kulinganisha na viongozi wengine waliomtangulia?
Kama ni kweli amefanya yote ambayo anadai amefanya ni kitu gani basi kinawafanya Watanzania wasiyaona mambo hayo na kumpatia pongezi zaidi kiasi kwamba badala ya kuongeza kura zake mwaka 2010 alizipunguzwa kwa asilimia 20 hivi? Kwamba pamoja na yote mazuri anajikuta anashinikizwa kuvunja baraza, utawala wake ukilaumiwa sana na wananchi wakiwa na kiu zaidi ya mabadiliko na uongozi. Tumeona juzi hata baadhi ya viongozi wa chama chake wakimuambia waziwazi kuwa "awe mkali kidogo".
Labda tujiulize swali la ugomvi zaidi - ni uongozi gani ambao Kikwete anapatia taifa kiasi kwamba anafanya mambo mengi mazuri lakini analaumiwa zaidi? Yaani, anafanya mambo ambayo anaamini ni makubwa lakini mbele ya wananchi yanaonekana kama 'hakunaga'?
Yawezekana, we are missing to recognize the genius in our midst? are we that blinded by whatever to the extent that we can not appreciate the work of superb and beloved leader? Ni matatizo ya sisi wananchi kutomtambua yeye au ni tatizo la yeye kutotambulika?