Tunamshukuru Rais kwa Kuongeza Muda wa Sensa

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Rais amewataka watu wote watakaoshindwa kuhesabiwa mpaka siku ya mwisho ya sensa, wapeleke taarifa zao kwa viongozi wa maeneo yao ndani ya siku saba ili taarifa zao zipelekwe panapohusika. Baada ya muda huo kupita wale watakaoshindwa kufanya hivyo watashughulikiwa.

Swali langu: Makarani walipangiwa maeneo yao kwa maana kila area ilikuwa covered. Kwanini hao makarani walioshindwa kuwafikia wananchi wasichukuliwe hatua?

Source: Hotuba Ya Rais
 
Washaughurikiwe kivipi? Watumie takwimu walizopata kwenye vitambulisho vya taifa! Aanze kushughuurikiwa yeye kwanza asiyechukua hatua!
 
dah hii inatisha sasa..................Hivi umeiuliza serikali yako ktk kpndi cha miaka kumi ya maandalizi ya sensa ilikuwa inaandaa nini? Ten yrs... Ten solid yrs of anticipation...............tunafanya uzembe hata ktk mambo ya muhimu, think.. upungufu wa vifaa, maofisa wa sensa kugoma, viongazi wa mitaa kugoma, waislamu kugoma kuhesabiwa?miaka kumi ya maandalizi then wht? Tafakari................Chukuwa hatua..................vua gamba.............vaa uzalendo......

SERIKALI LEGELEGE........................
 
Mbona hujamshukuru sasa?

Ahsante kwa kunikumbusha. Ahsante Mh.Rais. Sasa taaifa zangu zitaifikia Ofisi ya Takwimu kupitia kwa mwenyekiti wangu wa Kitongoji ambaye hakuwahi kuhitimu hata darasa la saba. Posho yake pia naamini atalipwa baada ya hali ya kifedha kuwa nzuri.
 
jamani nimesikia wimbo wa taifa ghafla nikamsikia kikwete anazungumza lakin sikupata nafasi ya kumsikliza kwa hyo mwenye taarifa sahii atujuze alikuwa anasemaje
 
Rais amewataka watu wote watakaoshindwa kuhesabiwa mpaka siku ya mwisho ya sensa, wapeleke taarifa zao kwa viongozi wa maeneo yao ndani ya siku saba ili taarifa zao zipelekwe panapohusika. Baada ya muda huo kupita wale watakaoshindwa kufanya hivyo watashughulikiwa.

Swali langu: Makarani walipangiwa maeneo yao kwa maana kila area ilikuwa covered. Kwanini hao makarani walioshindwa kuwafikia wananchi wasichukuliwe hatua?

Source: Hotuba Ya Rais

Nishughulikiwe kwa kosa gani? Hivi hawawezi kufanya mambo bila vitisho? Nilipanga kupeleka taharifa zangu lakini sitafanya hivyo, maana sijaona sababu iliyowafanya washindwe kuja kunihesabu.
 
Kesho nitakuwa nyumbani waje kunihesabu,ila saa tisa naenda kuangalia mechi
 
hata mm nimeuskia,ila nlikua bar,s unajua tena wauza mabaa wana alergy na hotuba?jamaa akabadili station bila hata kujua kilikua ni kitu gani.
 
Mimi nimepiga chaki mlangoni kwangu, na wengi wengine wamefanya hivyo, wana ushahidi gani kama sijahesabiwa? wakiona chaki wanapita.

Kwi kwi kwi teh teh teh!
 
Mbona sioni muda alioongeza? Kasema Kama kuna malalamiko yapelekwe kwa mjumbe ndani ya Siku Saba na sio kaongeza muda fanya edit ya post na hearding yako Mkuu..
 
Leo Rais wetu ameondoka kwenda Ethiopia kushiriki katika mazishi.

Kuna jamaa alianzisha thread hapa Akasema JK asipo enda Ethiopia apigwe ban for life.....Naona utabiri wake umetimia. Ivi aliudhuria mazishi ya waliokufa kwenye boti znz?
 
Huku kwetu huandikishwi hadi ulipe Mchango wa ujenzi wa soko wa Tsh15,000.

Hili zoezi linasimamiwa na Viongozi wetu wa Mtaa.
 
Back
Top Bottom