Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,252
- 113,647
..binafsi siamini kama viongozi hawa waliishi maisha kama yetu walalahoi. lakini hata kama waliishi maisha kama yetu sidhani kama tunapaswa kuwasifia. mimi nilitegemea viongozi hao wangetuwezesha na sisi tuishi maisha mazuri kama wao kwa kutumia juhudi zetu.
Kweli JokaKuu...kuna exaggerations fulani hivi kwa watu kusema hao viongozi waliishi maisha kama ya kwetu sisi walalahoi.
Hao viongozi sidhani kama walikuwa wanapanda vipanya na chai maharage tulizokuwa tunazigombania kwa kupigana vikumbo kila siku. Hao watoto wao walikuwa wakipelekwa shule na kwenda kuchukuliwa na magari yenye vibao vya magari vya SU au ST wakati sisi wengine tukiwahi stendi za mabasi kupigania usafiri wa daladala na UDA.
Huu ni mmoja tu ya mifano mingi ya kuonesha kuwa hawakuishi maisha kama yetu sisi walalahoi.