Tunamkumbuka Mzee Rashid M. Kawawa - Simba wa Vita

Inaelekea hata hotuba za Mwalimu ulikuwa husikilizi wewe

And speaking of Greatness what was so great about Rashidi?

Come on man, najua sasa hivi Taifa liko sedated na kutaka kumfanya Rashidi Mtakatifu ili hali alikuwa na madhaifu kama binadamu mwingine.

Editorials za magazeti ya leo ni aibu tupu.

Kawawa's greatness hinged on his patriotism, honesty and intergrity some of the qualities which you GT and your benefactors will strive for eternity to acquire!! Wewe na handlers wako ni wezi na mafisadi hamuwezi kujilinganisha na Simba wa Vita!! Sasa hivi project yenu wewe na comprador wenzio ni January Makamba, mnampromote ili aje kuwa conduit yenu ya kutuibia a' la mzee wake na sisi wadanganyika tutawashtukia mpaka hapo atakapoondoka na mfadhili wake; ubunge wa Lushoto atausikia kwenye bomba tu!!!
 
Jasusi,

..but i dont think it would make much difference whether ppl were mauled by lions in Rufiji or Mwibara. the main point here is that the government put its own ppl in harms way. hata kama huko walikoishi b4, lion attacks were a common thing bado nalazimika kuamini kwamba the government should have relocated them to areas which were safe.

..halafu jibu alilotoa Mzee Rashidi Kawawa alipopewa taarifa za wananchi kutafunwa na simba halikuwa zuri hata kidogo. sioni kama lina tofauti na yale ya kusema "bora tule nyasi", " they can go to hell ," au " kila mtu abebe msalaba wake "

JokaKuu,
Kumbuka kwamba Kawawa alikuwa kama ana 'nuksi' fulani hivi akawa analundikiwa kila aina ya lawama hata kwa makosa ambayo si yake. Operation vijiji kama watendaji wa ngazi ya Mikoa na Wilaya wangelitekeleza wajibu wao ipasavyo kwa maelekezo waliyokuwa wamepewa na wananchi wange-respond kama ambavyo ilitegemewa leo tungelikuwa tunazumgumzia maendeleo makubwa yaliyoletwa na vijiji. But alas, wakatokea watu wenye mawazo kama ya huyo Rugarasomebody ambao kwao mambo mengi yenye manufaa yaliyokuwa yakibuniwa na viongozi ambao hawakuwa na madigirii, yalionekana ni mabaya kwa wale waliojiona wamesoma zaidi and that they know better.

Waliofuatilia Operation Vijiji kwa makini wataelewa kwamba hakuna maelekezo yoyote yaliyotolewa ya kuwapeleka wananchi katikati ya misitu wakaliwe na simba. Maelekezo yalilenga katika kuwapeleka kwenye sehemu ambazo tayari watu walikuwa wakiishi lakini kukiwa na maeneo makubwa ya kuweza kupanua na kuendeleza shughuli za kilimo na kuwaweka wananchi pamoja ili waweze kupata kwa urahisi huduma zingine za maendeleo kama shule na zahanati, barabara etc.
 
Jasusi,

..sasa hayo majibu ya "Simba wa Vita" kwamba wananchi kutafunwa na "Simba wala Watu" unayachukulia vipi?

..hivi majibu hayo ni careless and insensitive sawa na yale mengine kama "wananchi tule nyasi" au "they can go to hell " au " kila mtu abebe msalaba wake"?

NB:

..tatizo ninaloliona hapa ni waandishi wa habari kumpa sifa nyingine ambazo siyo zake.

Hilo jina la "Simba wa Vita" huyo Rugarasomebody ametunga tu wala halikuanzia kwenye Operation vijiji!! Na siamini kabisa kwamba Kawawa aliweza kutoa jibu kama hilo ni uzushi kama ule wa "Kawawa funika kikombe'!
 
Boramaisha,

..binafsi nasubiri waandishi wenye upeo kama Jenerali Ulimwengu watupe wasifu wa huyu Mzee wetu na mchango wake.

..hata ukiwasikiliza jamaa wa FRELIMO na NRA wamefanya kazi nzuri ktk kuelezea kazi na michango yake kuliko waandishi wetu uchwara.

..Kawawa hakuwa mtu wa kawaida huyu. Kumbuka akiwa na umri wa miaka 35 tayari alikuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika. kabla ya hapo alishashiriki ktk harakati za uhuru na kujitoa ktk mambo ya kishujaa kabisa.

..ninachokataa mimi ni ile hali ya kujaribu kutuaminisha wananchi kwamba Rashidi Kawawa alikuwa masikini. naamini hiyo siyo kweli kwasababu anayo pensheni nono, matunzo, na huduma 24/7 alizokuwa akipatiwa na serikali kutokana na kodi ya wananchi.

..nadhani pia hujanielewa kuhusu hii dhana ya fringe benefits za viongozi. ninachosema mimi ni kwamba viongozi waishe kwa kiasi. viongozi wa Tanzania wamekuwa ni mzigo mkubwa sana kwa walipa kodi. hivi inaingia akilini mwako kwa kiongozi mkuu mstaafu kujengewa nyumba na serikali na kukabidhiwa kuwa mali yake binafsi? yaani kuwa kiongozi mkuu nchi hii imekuwa nchi hii "pasipoti" ya kuishi kwa kodi ya wananchi maisha yako yote?

NB:

..operation Vijiji ilifeli na kuporomosha uchumi wa mikoa ya kusini. suala hilo halihitaji mjadala, na kila aliyehusika anastahili lawama kulingana na nafasi yake.
 
jokaKuu,
Hapana. Kawawa hakuwa maskini in the real sense of the word. Lakini hapo hapo Kawawa hakuwa na mahela waliyo nayo akina Lowassa, Rostum, Kikwete, Karamagi na Chenge. That is a big difference. Kwa mantiki hiyo hiyo, Nyerere naye hakuwa maskini. He lived a simple life and shunned a life of luxury. Hakuwaachia wanae urithi except for the shamba in Butiama and a few cents that come from loyalties of the books he published.
 
Jasusi,

..kwani wazazi wa watoto wa kawaida huwa wanaacha urithi gani?

..kwanini taifa liwe "guilty" kwasababu Mwalimu,Kawawa,Salim Salim,Warioba etc hawakuacha urithi kwa watoto wao?

..guys, viongozi wakuu wanaishi kwa kodi yetu tangu wanaingia ktk uongozi. kama hawakuacha urithi hayo ni masuala yao ya ndani.
 
Thank you for all who contributed to this post by displaying historical pics for our serious leader Kawawa and others the founder of Tanzania.

Mungu amweke mahali pema peponi, AMEN
 
Jasusi,

..kwani wazazi wa watoto wa kawaida huwa wanaacha urithi gani?

..kwanini taifa liwe "guilty" kwasababu Mwalimu,Kawawa,Salim Salim,Warioba etc hawakuacha urithi kwa watoto wao?

..guys, viongozi wakuu wanaishi kwa kodi yetu tangu wanaingia ktk uongozi. kama hawakuacha urithi hayo ni masuala yao ya ndani.
jokaKuu,
Inavyoonekana hujanielewa. Nilikuwa nafananisha viongozi wa zamani na viongozi wa sasa kuhusu utajiri/mali walizonazo. That's all.
 
Jasusi,

..ingekuwa vema ukawalinganisha hao viongozi wa zamani na wananchi waliowaongoza.

..kwa maoni yangu kuna disparity kubwa kati ya maisha ya viongozi wetu na mwananchi wa kawaida wa nchi hii.

..hali hiyo ilianza tangu zamani na sasa hivi inakuwa mbaya zaidi.

NB:

..unapozungumzia kiongozi masikini moja kwa moja nakwenda kwa watu kama Abel Mwanga.
 
Abel Mwanga alikuwa mbunge wangu. Alikufa maskini kabisa. Kuna wakati nilimkuta Musoma akitembea na viatu chakavu. Ilinisikitisha kabisa.
 
Jasusi,

..kuna kisa cha Nyerere na Kawawa kujificha wakati wa machafuko ya 1964. i hope kuna mtu ambaye alielezewa kisa hicho na Mwalimu au Kawawa.

..ingefaa wananchi waelezwe viongozi hawa walijificha wapi na vipi. Watanzania, wazalendo, waliofanikisha tukio hilo, na kuwasitiri viongozi hao wakati wa matatizo, wanapaswa kutambuliwa kutokana na mchango wao huo.
 
jokaKuu,
Nilisoma mahali kuwa walijificha Kigamboni. Kawawa ndiye aliyesisitiza Nyerere aondoke Ikulu wakati Nyerere alitaka kuwasubiri wanajeshi aka reason nao.
 
Jasusi,

..sasa unakuta kuna waandishi walipata nafasi ya kumhoji Mzee Kawawa lakini hawakumuuliza kabisa kuhusu kisa hicho.

..kwa kweli mambo kama hayo ndiyo ya ku-include kwenye eulogy ya Kawawa. pia huwezi kuacha mchango wake ktk mgomo wa mabasi ya dmt, na jinsi alivyomsaidia Mwalimu ktk ile kesi kabla ya uhuru.

..vilevile mchango wa Kawawa akiwa waziri wa ulinzi wakati wa vita vya Kagera na Uganda nao lazima upewe nafasi.

..kwa kweli waandishi wetu wamekuwa very shallow ktk kumuenzi Mzee Rashidi Mfaume Kawawa.
 
Yaani, we acha tu. Nilipokuwa Tanzania nilinunua kitabu Rashid Mfaume Kawawa kilichoandikwa na John Magotti. I was so mad. Yaani kimeandikwa ki TANU TANU vile, bila hata maswali ya undani wa hisia na maoni ya Kawawa katika matukio mbalimbali ya Tanzania. What waste!
 
Waache kwenda kuwahoji kina Beni kinyaia wapoteze mda na wazee? tatizo ni elimu feki
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom