Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Sokoine ni kiongozi aliyetukuka wenye upeo, mchapakazi, mzalendo, mwadilifu, mwenye utu, asiyependa dhuluma ,uonevu ,mpenda haki asiye kuwa na makuu. Huwezi kumlinganisha EL na Sokoine kwani ni sawa na kumlinganisha Mungu na shetani.

Huku kwema mapya ya huku ni madini mliyoacha kwa sasa wenye nayo wamekuja kuyachukua maka na udongo wanabeba, wanyama pori kama twiga siku hizi wamekuwa na tabia kama mwewe wameruka hadi uarabuni na sasa itabidi tuwe tunafunga safari kwenda kuatizama huko uarabuni ila nauli itakuwa shida, mlima Kilimanjaro theluji imeisha inasemekana Mungu wa Wachagga naye amechoka kuona madhambi yao kama uzinzi, wizi, ufugaji wa majini na kukata miti hovyo so ametimka na blanketi lake ila wakirudisha miti atarudi.

Vile viwanda mlivyojenga na mwl vililiwa na mchwa mpaka kwenye mashina havioti tena ila jirani yetu Kenya alipiga dawa so vya kwake vinaendelea kuzaa na kwa sasa wameleta maoteo machache wakapanda hapa Bongo. Kuhusu maadui watatu Umaskini, Ujinga na Maradhi kwa sasa wamezidi hakika tuombee baya zaidi kuna adui mwingine ameongezeka anaitwa Ufisadi.

Huyu ni hatari kuliko hao maadui wengine amezama kwenye serikali hadi kwenye familia zetu.Anapiga bingo mbaya ni bilion kwa bilion nafkiri anaukoo na BILL GATES.Chama chetu cha kijani kilikuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi kwa sasa ni chama cha wafanyabiashara na wenye nazo ka michael jackson masikini wenzio niwashika pembe tu. Kama inawezekana njoo uje utunusuru baba ushirikiane na akina Mwanyembe, Slaa, Lisu,Sita, Butiku na Dogo janja kuinusuru hii nchi.Siku hata binti yako Namelock naye amekimbia vijiji vya ujamaa eti mambo yote yapo mjengoni kijijini kiangazi noma anataka ale vya kurosti pale monduli maziwa yamekuwa ni kama almasi.

Usisahau kumweleza baba wa taifa kwamba huku udini,matabaka tumeanza kuupalilia so akisia asishangae ila mwambie taratibu asijepatwa na mshtuko wa moyo.pumziko jema baba yetu
 
Kuna watu bado wanadiliki kusema eti LOWASA ni mchapaka kazi kama sokoine..inashangaza huyu fisadi kufananishwa na mzalendo huyu.inatia hasira sana
 
1938 Born in Monduli, Tanzania

1948-1958 Primary and Secondary Education, Monduli and Umbwe

1961 Joined Tanganyika African National Union (TANU)

1962-1963 Took studies in Administration, Federal Republic of Germany

1963 District Executive Officer, Masai District

1965 Elected to the National Assembly - Member of Parliament for Masai Constituency

1967 Deputy Minister of Communication, Transportation and Labour

1970 Minister of State, Vice President’s Office

1972 Minister of Defence and National Service

1975 Elected to the National Assembly - Member of Parliament for Monduli

1977 Member of the Central Committee of the ruling party Chama Cha Mapinduzi (CCM)

1977 - 1981 Prime Minister of the United Republic of Tanzania

1983-1984 Prime Minister for the second time

1984 April Passed away in a tragic car accident

Kutokana na wasifu na utendaji wake kazi nathubutu kusema kuwa shule si kipimo cha uteandaji, Moringe alikuwa na shule ndogo lakini aliwatingisha na kuwanyima usingizi watu waliokwenda shule.

daima tutamkumbuka sokoine


Hakika tutamkukumbuka daima yote Hayati Edward M. Sokoine!
Copy kwa Kyoma popote pale alipo!
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu bado wanadiliki kusema eti LOWASA ni mchapaka kazi kama sokoine..inashangaza huyu fisadi kufananishwa na mzalendo huyu.inatia hasira sana


Wacha tu mkuu Mi cjui member wengine wanashindwa kutofautisha usingizi na kifo Mi sijui kwa kweli.
Wanamfananisha Ngoyai na Moringe?
 
R.I.P baba yetu!! Nilisoma kitabu kimoja nikiwa darasa la sita 1997 kilichoeleza safar ya Moringe mpaka kifo chake niliumia sn.kwakweli waswahili wanasema "kizur hakidumu" lkn kiukwel Sokoine alistahili kudumu...naumia sn lkn maumivu nilonayo juu ya mtumishi bora huyu hayataondoa ukwel kwamba Moringe alizmika km mshumaa na hatainuka tena ktk USO wa dunia mpaka Yesu arudi!!
 
Mlale pema peponi...!
Mmeondoka viongozi wetu...mmeiacha nchi imevamiwa na viongozi mchwa, mafisadi, wapenda anasa, wanyang'anyi, walafi, wauaji, watekaji, waovu, na wasio mcha Mungu....! Tunakuomba Mwenyezi Mungu uliokoe taifa la Tanzania na Afrika yote...
 
Hakika jamani Mungu hebu tuletee viongozi wanaofanana nao jamani!
 
Walah! kama Nyerere akifufuka lazima afe mara ya pili maana tanzania aliyoiacha sio hii. imekua shamba la bibi.
 
Tulikupenda mungu alikupenda zaidi.

Walikuua Mungu ameshawaondoa na wao duniani.

Mungu akulinde akupe rehema zake akusamehe makosa yako baba yetu, mzee wetu, ndugu yetu.
 
Back
Top Bottom