Tunakusanya Kero ambazo ungependa zisemewe Bungeni na Nje ya Bunge na Viongozi wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Ndugu wabunge..Mimi nina mengi sana yakusema ila leo natoa hoja moja tu.

1.Tanzanite gemstone kwasasa hazisafirishwi nje ya nchi hadi ziwe processed hapa hapa Tanzania, Tanzaniteone Mining walikuwa wana export Tanzanite with Zero VAT, sasa Tanzanite inauzwa nje ikiwa tayari iko processed..Inakuwaje hawa jamaa wana export Tanzanite with zero VAT hadi leo??

2.Wakati wa campaign..Raisi aliahidi kuto kutoa leseni Mpya kwa Tanzaniteone mining LTD.. Leseni ime- expire toka mwaka jana..Je waziri wa madini anaweza kuteleza Tanzaniteone mining wanachimba madini kwa leseni gani hadi leo?? na kama bado hawajapewa leseni..Serikali inampango bado wakumpa Leseni mpya huyu mwekezaji??

3.Tunaomba waziri wa mambo ya ndani atueleze inakuwaje kampuni hii ina wageni zaidi ya 60 expatriate wakati kuna watanzania wanaoweza kufanya hizo kazi??

4.Kuna mfanyakazi mmoja wa security hapa Tanzanite one mining anaitwa COLLIN..alimuua mtanzania akakaa gerezani kwa mwaka akaachiliwa akarudi south africa...Chakushangaza huyu collin amerudi hapa Tanzania nakupewa working permit tena...hamna sheria yakuzua uuaji wa raia na bado mtu anapewa tena working permmitt...

5..Naomba mwendelezo..
 
Mimi kero yangu ni maji na ufisadi uliofanyika katika Wilaya Same kijiji cha Vumari.Hawa wanajiita TASAFU walikuja eti wanaboresha miundo mbinu ya maji.walidai wanajenga visima 2 vipya vya maji.Hatimaye wakakarabati tu vilivyokuwepo hawakujenga hata kimoja ,hela za kujenga visima zikaingia tumboni mwa wajanja.Badala yakuboresha miundo minu wakaiharibu hadi sasa watu wa vijiji vya vumari wanahangaika na maji.Yani ile maji ambayo tulikuwa tunapata kwa siku kwa masaa manne yanatoka kabla ya TASAFU, leo tunapata kwa wiki maratatu.Mbunge yupo huko dodoma amepumzika huku tunateseka.Ila silaha yetu 2015.
 
Yaani mimi ndiyo nasikia kama Laurence masha yupo kwenye Nyumba ya serikari mpaka hii leo Basi
Tanzania hatuna Viongozi tuna wahuni wanaopeana vitu vya uma hawa ni wahujumu uchumi mfukuze kwenye hiyo nyumba ya uma vinginevyo uma utamfukuza
 
MImi naliongelea hili la tenda za kutengenezea Barabara nakuombeni Tafuteni Njia nyingine ya upatikanaji wa wakandarasi
wa hizi barabara zinazojengwa abazo nyingi zinajengwa na wachina kuna siku nilikuwa naongea na maboss wa juu kabisa wa kampuni za kichina zilizoko hapa nchini kwa kazi hizo walinieleza hivi unaweza kutupeleka Ikulu tupate mtu aliye karibu na Raisi kwani Huyu mrema anachukua kwetu percent kubwa mno kwa kila project tunampatia ya kwake perent 4% mpaka 7% je hatuoni kama tunapoteza pesa nyingi kwa njia hiyo? na makampuni alinitajia 1.CHICO 2.SINO HYDRO 3.CRJE. NAKUOMBENI SANA WAHESHIMIWA WABUNGE ANGALIENI NAMNA YA KUMPATA CONTRACTOR VINGINEVYO BARABARA ZITUSUMBUA MPAKA MWISHO WA DUNIA
 
Mh. mimi nina kero kuhusu suala zima la ubarishaji wananchi na wanachama wa cdm kwa sababu toka ututoke kumekuwa na poor information supply kokote uliko (najua hauko nasi kimwili ila kiroho uko nasi)tunakuomba utusaidie kwa hili. Mfano kumekuwa na wimbi la viongozi waandamizi wa Chama kutoa taarifa nusunusu kuhusu mambo muhimu yanayohusu maendeleo ya chama. tukianza na ziara inayoendelea ya katibu mkuu wa chama kweli kumekuwa na uzito wa hali ya juu kuhusu uhabarishaji. Taarifa inatolewa lakini baada ya hapo hakuna mwendelezo.
 
Nashauri mifuko ya jamii kama NSSF, PPF, nk wewekeze kwa kujenga nyumba za walimu mijini na vijijini ambako hali ni mbaya kimaisha na kusababisha elimu kushuka kutokana na walimu kukata tamaa kunakosababishwa na mazingira mabovu y kazi
 
R.i.p regia sina uhakika kama hii page uliyo ianzisha kwa nia njema bila kujua kuwa februar ungekufa kama kuna mwana mbunge yeyote anaipitiaga lakini sio mbaya hili wazo lako litadumu milele mpaka kieleweke dada regia Mungu aendele kukuweka hapo peponi ulipo
 
kwanini viongozi wa ccm,awataki kumpigia kura mizengo.nakati hali inajulikana,chadema komaeni hadi mwisho kitaelewaka 2.
 
Mimi ni muajiriwa wa kampuni inayofuata sheria zote za kazi. Ninaposimuliwa unyanyasaji unaofanywa na baathi ya waajiri eti kwa sababu wana mkono mrefu waserikali inauma sana. Naizungumzia St. Matthew’s secondary school (mkuranga-coastal region) kongowe mkuranga. Yaani nilielezewa ikaniuma sana. Shule hii imeajiri degree levels wengi sana lakini haifuati sheria za uajiri. watu wanafanya kazi miaka kadhaa kwa mikataba ya penceli. Hivi juzi kuna dada mmoja alikuwa mjamzito tangia mwezi wa tano wakaanza kumsumanga, oo wewe ni mjamzito na hujaolewa kwa hiyo umejifukuzisha kazi mwenyewe. mwingine amejifungua akiwa maternity leave akakutana na phone call ya redundance. hamna cha kukatwa kodi, hamna kujiunga na mifuko ya hifadhi. mishahara yenyewe wanapewa mkononi ili kukwepa kodi. kama kuna mwandishi yeyote wa habari, mwanasheria au kiongozi wa serikali mkereketwa naomba afuatilie hii sule.
 
Mimi ni muajiriwa wa kampuni inayofuata sheria zote za kazi. Ninaposimuliwa unyanyasaji unaofanywa na baathi ya waajiri eti kwa sababu wana mkono mrefu waserikali inauma sana. Naizungumzia St. Matthew’s secondary school (mkuranga-coastal region) kongowe mkuranga. Yaani nilielezewa ikaniuma sana. Shule hii imeajiri degree levels wengi sana lakini haifuati sheria za uajiri. watu wanafanya kazi miaka kadhaa kwa mikataba ya penceli. Hivi juzi kuna dada mmoja alikuwa mjamzito tangia mwezi wa tano wakaanza kumsumanga, oo wewe ni mjamzito na hujaolewa kwa hiyo umejifukuzisha kazi mwenyewe. mwingine amejifungua akiwa maternity leave akakutana na phone call ya redundance. hamna cha kukatwa kodi, hamna kujiunga na mifuko ya hifadhi. mishahara yenyewe wanapewa mkononi ili kukwepa kodi. kama kuna mwandishi yeyote wa habari, mwanasheria au kiongozi wa serikali mkereketwa naomba afuatilie hii sule.
 
mimi naumia sana kuona ninakatwa kodi halafu sioni ya kukatwa kwangu kodi,, hivi kwanini hawa NSSF na wengine kama PPF, PSPF, watumie hiyo hela tunayokatwa kodi kuwajengea hao wafanyakazi hata nyumba basi manake ukisema uisubiri uikusanye ukistaafu ni kwa asilimia kubwa hakutakua na uwezekano wa kuzipata zote... inauma sana basi walau watujengee hata barabar na kuboresha miundo mbinu,,,, halafu ni haki yetu pia kila mwisho wa mwaka kupata some returns kutoka haya mashirika ya pensheni sasa kwanini huwa hatulipwi,, mimi ninaumizwa sana na utaratibu usioeleweka wa hii nchi....
 
Ina uma sana kitendo cha serikari kuwanyanyasa walimu kisaikolojia walio jiendeleza kufikia shahada ,hasa kwa kitendo cha kuwazuia kupandishwa ngazi za mishahara na badala yake kuwapa vyeo vya kwenye makaratasi na kuwahamishia sekondari walio kuwa msingi bila malipo yoyote.Hili limefanyika jijini MBEYA 2010 na 2011
 
ninapenda kuliongelea swala la watu kuuawa bila sbb za msingi naishangaa nchi hii iliyona aman na utulive ...eti kuna viongozi wa majeshi ya ulinzi na usalama...wanafanya nini ...TAFAKARI CHEDEMA NDO WAMEKUA POLICE SS KUFATILIA HAKI ZA WANANCHI NA MALI ZAO...JE HII NA KAZI YA CHADEMA LKN NI KWA SBB YA JESHI LA POLICE KUA WAZEMBEEE....TAFADHARI HILI LIFIKE MBELE YA BUNGE NA HAKI ZIFANYOKE JUU YA WAUAJIII....SI KUA WANASHIKILIA KESI AMBAZO HAZINA MAANA NA KUDAI RUSHWA....TUUUUUUUUUUUUUUUUU
 
KERO YANGU NYINGINE:

Wazawa kupewa title deeds zisizozidi miaka 33 na wageni kupewa miaka 99. Ukweli ni kuwa hata kizazi kimoja hakipiti na umiliki wako unakatika. Ina maana kuwa huwezi hata kumrithisha mtot wako nyumba. Hii italeta vita nchi hii kama vile vita vya kugombea uhuru vya Zimbabwe.

Kwa nini tunatenda yale ambayo tuliyakataa wakati wa ukoloni?
 
1. Serikali kutokuwa na VIPAUMBELE sahihi (mfano: kununua mashangingi kwa mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa mikoa, n.k. badala ya kujenga hospitali, shule, barabara nzuri).
2. Miji yetu kujengwa pasipo kufuata master plan yeyote (hivi moto ukitokea Kariakoo, Fire Brigade watapita wapi kwenda kuuzima? Ukitaka kumwelekeza ndugu akutembelee kule unakoishi Kigilagila ama Yombo ama Kawe ama wapi sijui, unamwelekezaje wakati hakuna mitaa inayo make sense?)
3. Miji yetu kuwa michafu as if hakuna authorities wa kuondoa uchafu na pia kuweka sheria za kuwafanya watu wazingatie usafi.
4. Umeme usio na hakika, hata baada ya miaka 50 ya uhuru.
5. Mazingira yasiyo rafiki kwa private sector na hivyo kupelekea ukosefu wa ajira.
 
tunaomba chadema ipitie ruvuma, lindi, mtwara huko bado elimu ya uraia bado so please kuna kura zetu nyingi sana kutoka kwa vijana wengi kule ni wapinzani ila hawana chama.
 
Wakazi wa Kigamboni tunajiuliza tulimkosea nini Mwenyezi Mungu? Mimi nimezaliwa na kukulia Gezaulole, nilikuwa nimejiandaa kuanza kujenga nyumba yangu na sasa ni zaidi ya miaka minne tangu tuzuiliwe kujenga. Pia, haturuhusiwi kuuza maeneo yetu, eti kuna mipango ya kujenga mji. Tutasubiri mpaka lini? Serikali imetusahau kabisa. Wa kututetea hatuna, CHADEMA tuteteeni jamani.
 
hebu pambaneni na hili la mzazi kulipa pesa ya majengo kila mwaka zinaenda wapi na kujenga nini kujaza matumbo ya watu tu na nchi inajiweza kwa kila jambo wanabanwa wadogo wakubwa wanaogelea na mabilioni
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom