Tunakusanya Kero ambazo ungependa zisemewe Bungeni na Nje ya Bunge na Viongozi wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Zifuatazo ni kero ambazo ningependwa zisemwe bungeni
  • Wafanyakazi kutoka nje wasiokidhi viwango ukilinganisha na watanzania katika sekta ya madini
  • Viongozi wa nchi kutibiwa au kufanyiwa uchunguzi wa afya nje ya nchi hata kwa magonjwa madogo badala ya kutibiwa na madaktari wetu
 
Dada Regina Natanguliza Shukrani zangu kwako kwa kuanzisha site hii, Vile vile Nampongeza Mh Dk magufuli kwa Bajeti yake

Aliyoisoma wiki hii Bungeni Lakini Kero yangu kwa wizara hii Ni hili la Mizani ya kupima Uzito unaobebwa Na magari makubwa
Hainiingii Akilini Kwa mfano Sasa hivi katika jiji La Dar-es-salaam kuna Miradi Miwili Mikubwa Ya Barabara ambayo ni Mwenge _ Tegeta Na BRT project yaani mabasi yaendayo kasi ambayo Inaazia Kimara Mpaka Feri.

Sasa Basi Hizi Barabara Zinajengwa kwa Udongo Na mchanga Na hawa wakandarasi wote wameamua kuwaachia wazawa
wafanye kazi ya kuleta hayo Materials kwa magari ya Watanzania ili pesa ibaki Ndani Ya Tanzania Na Materials hizi Hauwezi kukadiria uzito wake Halisi Cha kushangaza hawa watendaji wa Tonroads Dar_es-salaam wanaacha magari yapite Toka Boko Na Bunju Na materials yaharibu Barabara wakati wanamzani Ambao Ni Mobile

Wanakuja kuwavizia Mwenge Na Kobil mlimani City Kwa nini wasiwafuate Kule Boko Na Bunju Ambako Magari Yanatokea kwenye Barabara ya vumbi Kuingia Kwenye Lami Ili kuzuia Uharibifu Mkubwa Kwa Barabara ambazo Zinatengenezwa kwa mabilioni ya shilingi? Hapo kwa akili za kawaida tu Kuna Dalili za hawa watendaji kutafuta mwanya wa kupata Rushwa

Kama sikosei mh Dk Magufuli aliwahi kusema bungeni kwamba Mizani Yote Tanzania Ilitumia Bilion 5 wakati wao walikusanya Bilioni 4 huo ndiyo wizi ambao Dk magufuli anatakiwa asiufumbie macho atafute njia ya kuwapunguzia hawa
watu wa mizani wasipate mwanya wa kujipatia rushwa Kirahisi kama hawa wa Mzani unaotembea hawana sababu ya kuvizia haya magari mbele ya safari wakati boko au bunju sio mbali na vile vile wanawe wakayapima haya magari na kuweka Alama yasipakie Zaidi ile alama Then wakikamata Tipper limepakia zaidi ya ile alama Ndiyo lilipe Faini

Maana mimi Niliwafutilia hawa jamaa kwa kila gari walilolikamata bila wao kunijua walikuwa wanachukua pesa zisizo na risti kati ya 200,000 na 600,000 waliyakamata magari 60 kwa muda wa masaa 4 hivyo walio aminiwa katika ule mzani wa
kutembea sio waaminifu wako kwa ajili ya manufaa yao zaid hizo ndizo kero kwa wenye mattiper ya mchanga.

Naomba kuwakisha.
Dk Kambiulaya
 
Kwanza niwapongeze wabunge wote wa CHADEMA na wale wa upinzani kwa kazi nzuri bungeni.
Kero yangu ni juu ya Idara ya Maji Manispaa ya Morogoro. Imekuwa ikikataa kutuunganisha maji kwenye maeneo ya Kola B kwa singizio kuwa kuna mpango uliofadhiliwa na mashirika ya nje wa kusogeza bomba kubwa karibu na nyumba za watu. Ahadi hii ni ya zaidi ya miaka 3 sasa tangu nianze kuisikia mwaka 2010. Bomba linalotakiwa kuwekwa ni la umbali wa mita kati ya 500 na 700 tu lakini cha ajabu mwaka huu mwanzoni walikuja wakaweka bomba kama mita 200 tu kisha wakasema pesa za mradi zimeisha.
Kero kubwa kwetu ni maji huku na wao wameshakataa kutuunganisha hata pale tunapotaka kugharamia kila kitu ili kuyapata maji toka bomba lao lilipoishia. Kwa utaratibu huu, tunapata taabu sana kwani inabidi uvizie kwa baadhi ya watu ambao waliruhusiwa kabla ya mwaka 2010 kuvuta maji kutoka mita 600 lilipokuwa linaishia bomba kubwa kwa wakati huo. Kwa sasa bomba limekaribia na wengine ni limetukaribia kama mita 150 tu lakini ukienda ofisi ya maji utaambia hawaunganishi wateja mpaka mradi uliofadhiliwa ukamilike.
Kibaya zaidi ni kuwa kuna baadhi ya watu akiwemo Mkuu wa mkoa mmoja wanaunganishiwa maji. Kero tupu.
Inauma sana kudharauliwa na kubaguliwa kiasi hiki.
 
Kero yangu kuu ni swala la huduma mahospitalini ....jamani naomba nieleweke hivi..inaniuma sana ninapoona mwanadamu mwenzangu anateseka hali alipojisikia udhoofu alikimvilia Hospitali kwakuwa ndiko sehemu pekee inayoleta matimaini ya uhai wetu...mimi naomba swala la kuboresha mazingira ya Hospitali zetu kwa maana ya vifaa au vitendea kazi lipigiwe kelele za kutosha bungeni...tumeona madakitari wakigoma kudai hayo pia lakini sasa ilivyowekwa na serekali yetu ni ushawishi kwetu wanainchi tuelewe kuwa madakitari wanataka mishahara mikubwa lakini hili la ubovu wa vitendea kazi vya kumwezesha dakitari afanye kazi yake vyema haliongelewi...mimi naomba kwanza serekali itatue yale madai wanayodai madakitari yanayogusa jamii moja kwa moja halafu hilo la mishahara lishughulikiwe polepole
 
Kero zangu ni the Workers Compensation Act 2002. Soma Chapter 263 utusaidie. Wako wananchi wengi wanalia kuhusu Act hiyo inayotumiwa na Labour. Iweje mtu aumie na kulemaa akiwa kazini alipwe 108,000/= zitamsaidia nini? Dr Lissu Tundu uko wapi utusaidie sisi wanyonge?
 
Sidhani kama uko kwa ajili ya kuwasaidia watanzania wote, nakama ndivyo hebu tatua kero hii ya wananchi walio wengi, Sensa ndo hiyo iko kwenye kona inasogea wananchi wa tanznia hasa waislamu wanasema hawata hesabiwa mpaka kipengele cha dini kiwekwe kwenye dodoso, unaweza ukashanga kwanini udini? Lakini fikiria takwimu zilizo tolewa na catholic church kwamba wakristo ni wengi tanzania hili linawakera, Napia kama serikali haina dini na haihitaji kujua takwimu za watu kidini kwanini inahesabu nyumba za ibada yaani misikiti na makanisa?, Kama chadema chama cha wananchi hii nikero izungumzeni.
 
TUNAOMBA , JAMAN ITAKAPOFIKA , KUJADILI BUDGET YA WIZARA YA SAYANSI NA TECHNOLOJIA NA MAWASILIANO,
1. WAZIRI AELEZE KIASI KILICHOTUMIKA KUJENGA MAJENGO YA HOSTEL YA WANAFUNZI TAASISI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA (mist). kunauchakachuaj hapo.
2. je maeneo ambayo chuo hicho(mist) kina chukua kwa wananchi ni lini kitalipa fidia, na kama selikali haina uwezo wa kuwalipa wananchi hao ni kwann isiruhusu , waendelee na ujenz katika maeneo yao.
3. eneo la chuo cha mist inaonekana ni kubwa , lakini nilini selikali itaendeleza ujenzi katika kupanua chuo hicho, huku kinatakiwa kuwa chuo kikuu, na bado kina endelea kutumia majengo na miundo mbinu ya zamani (1985) enzi za mrusi , kikiwa kinaitwa MTC, MPAKA SASA MIST NA KISHA KITAKUWA MUST? IDADI YA WANAFUNZI INAONGEZEKA?
4. JE PESA ZILIZOGAIWA KWA WAFANYAKAZI NA WAKUU WA IDARA WA CHUO HICHO ZILITOKA WAPI? NA INASEMEKANA WAKUU WA VITENGO IDARA NA TAASIS WALIKULA PAREFU, HUKU SERIKALI INADAIWA NA WAFANYAKAZI WA CHUO HICHO ZIKIWEMO PESA ZA RIKIZO N,K
 
Tena hawa wa kusoma na kuandika "Mheshimiwa spika naunga mkono hoja aslimia mia miaaaaa" kumbe hamna kitu kichwani anaona kama akipinga anaweza kuulizwa sababu za kutounga mkono hoja hivyo anajiwahi.

HARUFU KALI YA TUMBAKU KWA WAKAZI NA WAPITA NJIA ENEO LA KIWANDA/OFISI ZA SIGARA

Eneo hilo lina harufu kali sana na nina uhakika kuwa ina madhara kwa wananchi na zaidi wale wasiojihusisha kabisa na kiwanda hiko kama wapita njia. Je serikali ina lifahamu hilo na ina mpango gani? mimi huwa napita tu kwenye daladala lakini napata tabu tukifika eneo hilo.
 
JAMANI KERO YANGU KUBWA NI KWA WIZARA YA ELIMU.sisi walimu tulioajiriwa kwa leseni.tulikuwa tunalipwa 80% ya mshahara wa diploma ambao kisheria haturuhusiwi kukatwa kodi lakini cha ajabu serikali imeamua kutukata bila taarifa na kinyume na tarabu zetu za ajira kwani hatupaswikukatwa.pia unapajiendeleza experience yetu haizingatiwi.tunaomba msaada wenu wabunge wakati huu wa bajeti.maisha magumu jamani.
 
kuna mkuu wa idara ya serikali mja huko mbinga ruvuma anaifanya idara ya uhamiaji kama mali yake unapoenda kufata huduma anajiamulia vtu anavyotaka yy akiamua kukunyima huduma anakunyima tutamchoka hebu ifatilieni gari ya serikali anapeleka shamba kwa kazi zake binafc aliangusha gari akienda kwenye mambo yake binafc mumfatitilie huyo
 
mimi kero yangu ni ktk kujiendela kielimu upande wa nursing km mtu ana certificate anataka kusoma diploma anaangaliwa ufaulu wake wa fm 4 je hii inahaja gani kwanini yasiangaliwematokeyake ya mwisho wakati anamaliza masomo ya nursing certificate kweli wizara inatukwaza kwa hilo itafanya watu wengi wasisome jamani hata viwango vya D vikubaliwe C tutazipata wapi tungekuwa na uwezo huo si tungeanza na degree moja kwa moja kwa moja
 
Hata kama ni RIP mimi naendelea kuchangia, Regia alikuwa na mawazo sahihi kwa habarii ya ukusanyaji kero.....tumempoteza mbubge na ambaye angekuwa Waziri mteule wa Maendeleo ya Jamii
 
Kwanini tuwaambie wabunge wa chadema pekee na sisi wafuasi wa CUF tunaruhusiwa kuwaambia wabunge we2?
 
Napenda viongozi wangu wa CDM wakalisemee hili:WAALIMU wanapelekwa vijijini kwenye shule za kata lakini inapofika mwalimu huyu anataka kwenda likizo anaambiwa atalipwa kwa viwango vya SUMATRA na ikumbukwe sumatra hawajapanga viwango vya kwenda na kutoka kwenye vijiji,na unakuta nauli ya kutoka kijijini hadi mjini inafika mpaka Tsh 12,000/=kufika wilayani,sasa mwalimu huyu ana watoto na mizigo,kwa kweli ni shida tupu.imejitokeza KATIKA wilaya ya BUKOMBE
 
kero yangu ni iyo ya viongozi kusema kwamba ppf itoe mafao ndani ya miaka 55 ya mwajiri kustafu.asa ataitumiaje na vijana wengi wa sasa ni vigumu kufikia hiyo miaka na nibora wangekuwa wanatoa kutokana na mkataba kati ya mwajiriwa na mwajili wake kuisha ili aendelee kuifanyia matumizi wengine ya kumjenga kiuchumi.wafikishie ayo
 
KERO YANGU NI ' THE WORKERS COMPENSATION ACT 2002" INAYOTUMIKA SASA. Kipengele cha 7: Ukipata ulemavu wa kudumu kazini sheria inasema ulipwe mishahara yako kwa miezi 54 lakini kiasi hicho cha pesa kisizidi 108,000 na kisipungue 2,000. Kwa kweli ni sheria inayokandamiza sana mfanyakazi aliyepata matatizo. Sheria hiyo ilirekebishwa mwaka 2002 lakini kipengele hicho ni cha sheria ya 1966.
 
Kero yangu ni Zitto! wanabodi anapoteza stepu za M4C kila wakati anakuja na ishu za kugawa chama na iwekwe wazi ni anamahusiano na TISS na kibaraka wa Jack Nzoka
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom