Tunakusanya Kero ambazo ungependa zisemewe Bungeni na Nje ya Bunge na Viongozi wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
Wakuu habari! Nimatumaini yangu kuwa tunaendelea vizuri na majukumu yetu ya kila Siku.

Nimeamua kuanzisha Uzi huu kwa lengo la kukuza ya kero,maoni,ushauri na chochote toka kwenu ili tuweze kuyasimamia ndani na nje ya Bunge.Kwa kutambua kuwa wanaJF wamesambaa kila mahali,maofisini,mashuleni,mitaani,majumbani na huko kote kuna kero mbalimbali zinazohitaji attention ya Serikali lakini mambo hayaendi na ungpenda kuona suala hilo linafanyiwa Kazi na hivyo unapendekeza Kambi ya Upinzani izibebe na kuzisimamia. Basi tafadhali toa kero,maoni,ushauri au hata mapendekezo yako hapa.

Tafadhali kero ziwe za kijamii na sio za mtu binafsi.

Natanguliza Shukrani zangu za dhati kwa Ushirikiano wenu.

Wenu katika Ujenzi wa Taifa
Regia Mtema
 
Anza na hili la Nyumba za Umma waliojiuzia bei rahisi Vigogo wa serikali na wafanyabiashara wakubwa tena kwa bei rahisi,chonde chonde anza na hilo kwani lina-effect uchumi wa nchi na tumeona viongozi wa serikali wanakaa hotelin na kua na ofisi hoteli coz nyumba za kukaa hawana kwa sababu mafisadi wamejiuzia,hili mliwekee priority ya kwanza tunahitaji nyumba zote zirudishwe serikalini na sio kua za watu binasfi
 
Kero kubwa sana kwa sasa ni hii ya nyie Wabunge kujiongezea maslahi peke yenu, huku shule hazina madawati, wala maabara!

Mna raha gani na hizo hela wakati wanaowazunguka wanaomboleza na kuteseka kwa mlo mmoja?..Au kwa vile mnaishi masaki na Mbezi Beach, hivo mnahisi majirani mlio nao pale ndivyo Watanzania wote walivyo?

Futeni hizo posho ziende kusaidia mambo yanayokera wananchi!...Kero hii naitoa tu, siamini kama utaifikisha mahala husika!
 
Mifuko ya hifadhi hasa NSSF wahakikishe kuwa wanachama wao wanafaidika na michango wanayoitoa kwa kuwapatia mikopo, siyo kupeleka mabilioni ya wanachama wake kwa watu ambao wala hawajui pesa hizo zimetoka wapi, mfano kwa nini wafanyabiashara binafsi wanapewa mikopo na nssf lakini mwanachama hapewi?

Kwanini mabilioni ya wanachama yanapelekwa kwenye miradi hasa ya majengo wakati wanachama hawafaidiki? Hatutaki majibu ya longolongo kwani tumekuwa tukiahidiwa kwa zaidi ya miaka mi5 sasa wakati hatuoni utekelezaji.

Tunahitaji kufaidika na michango yetu sasa badala ya kusubiri "pensheni" ambayo unalipwa kiduuuuuchu miaka michache kabla ya kufa.
 
Kero zangu kubwa ni:
-Uwekezaji kwenye SIASA. WAnasiasa kulipana kama akina Lionel Messi, Rihana,...
-Kale ka utaratibu kalikoko kwenye KATIBA za vyama vyetu vya SIASA ka kufukuzana uanachama na Katiba yetu ya JMT.
-VITI MAALUM vya UBUNGE na vile 10 vya Rais.
-Idadi kubwa ya majimbo ya uchaguzi. kila Halmashauri/Manispaa/Mji/Makundi maalum yawe na Mbunge mmoja.
-Teuzi zisizothibitishwa na zisizo na kikomo zinazofanywa na Rais.
 
Kero yangu Kubwa ni huu Ujenzi wa barabara za jiji ambao hauzingatii usanifu wa aina yoyote!!

Barabara zinajengwa bila usimamizi na kusababisha kuharibika baada ya muda Mfupi sana!! Barabara kama hizi unakuta zinatumia pesa Nyingi ambazo hazina manufaa!! Mfano barabara ya Kigogo first inn Kuja Mburahati hadi Kagera!! Ujenzi wa barabara hii Uligarimu Hela Nyingi ila wakati wa ujenzi nilikuwa napita ila kulikuwa hakuna usimamizi wa aina yoyote!! Hivyo Mkandarasi alikuwa anaweka udongo Mzuri Juu ya marundo ya Taka yaliyokuwepo Tangu enzi ya barabara ikiwepo kipindi Haina Lami!! Sasa ile barabara imekuwa ni Mashimo Matupu!! Full Kuharibika!!

Tunaomba hawa manispaa ya Kinondoni ni Nini wanafanya ili waweze Kusimamia ubora wa Kazi na Usanifu wa Hizi barabara? Hadi Kero!! Ndugu Mbunge jitahidi kufuatilia hili, Kwani huyu Mkandarasi anaonekana ametuzidi Maarifa kwa kazi zake Mbovu!!

"Hari Sigh"
 
Kero kwangu kubwa ni hii:-
1.Je,serikali ime wekeza kwenye ujenzi wa hospitali huko india?
Kama ndio,kwanini ndugu zetu wanao ugua magonjwa makubwa hawa pelekwi
kwenye hiyo "hospitali yetu" ilhali nyie wabunge hata mkiugua malaria "mbili" mna kimbizwa huko?

2.Kama hatujawekeza huko,kwanini nyie wabunge mkienda kutibiwa hamrudi mkawa na hamu ya
kuona hospitali kama za huko india zikejengwa hapa?

3. 1 na 2 yanazaa swali la tatu,...kwanini serikali ina dharau taaluma za watanzania?
Juzi hapa madaktari wanafunzi walipo kua wanadai haki zao walipewa kisha waka timuliwa,...
Je,...wana mpango wa kutuletea wahindi waje kututibu au ?Maana hata hawa walio kua wana
kuangalia usoni tu na kukupa panadol wamewatimua ili tufe zaidi.

4. Kwanini uhuru wa kujieleza ume bakwa na serikali?
Ndo kusema demokrasia mda wake umeisha Tanzania na tunaelekea kwenye udikteta au?
Nasema hivi kwa sababu UDSM wanafunzi walifukuzwa bila makosa,viongozi wa wanafunzi waka fuatilia
nao wamepewa barua za "expulsion from the university" leo,...na tangazo limewekwa la vitisho kwamba
"hakuna haki ya kukusanyika popote pale",...hii ni tanzania kweli?

Aghr,nimechoka kuandika.
 
1. Kupungua uwajibikaji kwa upande wa serikali na kutumia kukomoa kama njia njia ya kutatua migogoro inayotokana na kutokuwajibika kwenyewe,mfano sakata la madaktari walio katika mafunzo-MNH,migogoro mbalimbali katika vyuo vikuuu

2.Kuadimika mara kwa mara kwa nishati ya mafuta pindi EWURA inaposhusha bei ya hiyo nishati

3.Mfumuko wa bei za bidhaa muhimu
 
nahisi kama umechanganya mada mkuu,hizo zako zingeelekezwa kwenye mabadiliko ya katiba!
Tuziseme sasa maana huenda KATIBA yenyewe isije mapema. Kero zingine ni:
-Ongezeko la kila mara la Mikoa , Wilaya, Tarafa, Kata na vijiji ambalo linaambatana na ongezeko la wakuu wake.
-Huduma mbaya kabisa za ELIMU, AFYA, MAHAKAMA, POLISI.
-Mfumuko mbaya kabisa wa gharama za maisha na anguko takatifu la shilingi yetu.
-Serikali kubwa na vyombo duni kabisa vya DOLA kama PCCB, UwT, EWURA,...
- Ongezeko la Watu matapeli, wezi, mafisadi wenye nguvu kabisa kuliko DOLA.
 
Regia, kwa miaka mingi sasa kila tunapopata matokeo ya mtihani (i.e STD 7, Form IV etc) utasikia wizara inasema kuwa baadhi ya wanafunzi wamefutiwa matokeo ya kwa sababu ya udanganyifu. Kwa maneno mengine watoto hao walipata mtihani. Je, nani amepewa jukumu la kusimamia hii mtihani ili isi-leak? Wizara imefanya nini kukomesha kabisa (sio kupunguza - kukomesha) huu ugonjwa?

Hatua kama ya kufukuza watoto/kuwafutia mtihani sio sahihi kwa sababu:
(a) wao sio chanzo cha ku-leak, hivyo ni sawa na ku-deal na matokeo badala ya chanzo cha tatizo
(b) kuwafutia mtihani kwa sababu ya uzembe wa 'security' ni kuwaonea kwa sababu jukumu la kuchunga mtihani ni la serikali,
(c) kuna hatari ya kuongezeka kwa vijana mtaani kwa sababu unapomfutia mtihani anakwenda wapi?
(d) Ni lini waziri au wakubwa toka wizara ya Elimu watawajibika kwa kutotunza mtihani ipasavyo? Ushahidi upo maana kitendo cha kuwafukuza watoto kwa madai ya kudanganya tafsiri yake ni kwamba wizara inakubali imeshindwa kutunza mtihani na hivyo ume-leak. Uwajibikaji muhimu. Kama waziri hawezi kusimamia mtihani ana umuhimu gani wa kuwepo ofisini?

Jambo jingenie, Serikali imekuwa inaimba wimbo wa Kilimo kwanza, na kama tujuavyo vijana ndio taifa la kesho. Sasa serikali inafanya nini kuhakikisha vijana wanapata msingi mzuri ili kesho ikifika wawezi kutimiza dhana ya kilimo kwanza?

La mwisho (kwa sasa) nini vision ya nchi hii? Serikali ya CCM ina vision gani kwa Tanzania? wamefanya nini katika kufikia hiyo vision? Na kama hiyo vision ipo elimu yetu inahusikaje (ki-mfumo) kuhakikisha inajenga vijana (wanafunzi) ambao wataweza ku-realize hiyo vision. Kwa mfano, kama mpango ni wa kuifanya Tanzania iwe manufacturing base kwa Africa, je elimu inayotolewa itamwezesha mwanafunzi kutimiza hayo malengo?
 
Yes,
nadhani hili liunganishwe na swali kwanini migomo inatokea vyuoni?
Wasitafute umaarufu kwa kufukuza watu huku wakishindwa kutoa haki.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom