Amani Nyekele
Senior Member
- Jul 8, 2011
- 159
- 26
you must be from ARDHI UNIVERSITY!... WE SHALL REMEMBER YOU MWANAHARAKATI REGIA MTEMA!! rest in peace...!!
Mifuko ya hifadhi hasa NSSF wahakikishe kuwa wanachama wao wanafaidika na michango wanayoitoa kwa kuwapatia mikopo, siyo kupeleka mabilioni ya wanachama wake kwa watu ambao wala hawajui pesa hizo zimetoka wapi, mfano kwa nini wafanyabiashara binafsi wanapewa mikopo na nssf lakini mwanachama hapewi?
Kwanini mabilioni ya wanachama yanapelekwa kwenye miradi hasa ya majengo wakati wanachama hawafaidiki? Hatutaki majibu ya longolongo kwani tumekuwa tukiahidiwa kwa zaidi ya miaka mi5 sasa wakati hatuoni utekelezaji.
Tunahitaji kufaidika na michango yetu sasa badala ya kusubiri "pensheni" ambayo unalipwa kiduuuuuchu miaka michache kabla ya kufa.
kero yangu ni juu ya kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha pili hasa katika sekondari ya kibamba iliyopo katika manispaa ya kinondoni.Kwako Mh: Mnyika.WC,Kilombero ina Wabunge 4,Vitimaalum 3, Suzan Kiwanga-CHADEMA,Getrude Lwakatare-CCM,Regia Mtema-CHADEMA na huyo mwingine wa Jimbo.
kwanza mh regia mtema nakupongeza kwa thread hii.
Pili, napatwa na wasiwasi kama umeweza kuchukua maoni yote zaidi ya 100!!!
Kwa matumaini nawasilisha kero au mapendekezo haya hapa chini:-
a- nssf kukopesha wanachama wake. Unakuta nina akiba kwenye nssf kama 5 mil ila siwezi kukopa.
b- ardhi ni uti wa mgongo wa kilimo, na kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa tanzania.kilimo hutoa ajira, kilimo hulisha nchi.
mimi nashangaa vigogo wanajimilikisha ardhi kama ekari 2000, 1000, 500, 200, 100 wakati wananchi wanatafuta sehemu ya kulima wanakosa. Rejea list ya mh mdee bungeni alivyowataja vigogo.
hapa tanzania kuna hekari nyingi sana zipo wazi, hazilimwi, na mtu akithubutu kulima anaambiwa mvamizi. Hivi kimsingi, je ardhi ya tanzania ni ya rais au ni ya wana wa nchi???
Pia kuna mashamba ya nafco na ranch kibao zipo idle.
Wawekezaji wanakuja wanapewa ardhi bwere ree ila wananchi hasa vijana hawana kimbilio.
Watanzania tupo gizani hatujui ardhi ya kulima itapatikanaje? Wizara ya ardhi, ofisi ya waziri mkuu zote hizo hawako wazi jinsi ya kupata ardhi.
Pia hata viwanja katika manispaa zetu ni ghali mno. Unakuta manispaa wanapima ardhi halafu wanauza zaidi ya million 5, je, wananchi wa hali ya chini na vijana wataweza kununua?
Sasa manispaa hizo hela wanapeleka wapi wakati ardhi ipo bure? Hawajanunua?
nasubiri kusikia hii hoja bungeni , pia ushauri wako ni mzuri, nasuburi mheshimiwa.
Chadema yenyewe kero tu sasa wakiongeza kero zingine yatakuwa mijikero