Tunakosea wapi kuoa/kuolewa?

Utandawazi nao unachangia mahusiano kuvurugika siku hizi..Ni kama humu tu baadhi ya watu wanavyodanganyana..Kuna watu wanabeba vitu kama vilivyo kutoka mitandaoni na kuvipeleka kwenye ndoa..
 
Kwa ufupi mapenzi ya sasa ivi yanaendeshwa na miemko(kama serikali ya ccm)na tamaa ndani ndoa inayeyuka..!
 
Tumemuacha sana Muumba wetu pia hata wazazi wetu hatutaki kuwapa nafasi katika swala zima la kuingia ndoani.
 
Mnalalana weee miaka na miaka hlf eti baadae mnafunga ndoa, mnamdanganya nani hakuna excitement kivile tena, na mwingine mda wote alikuwa anajilazimisha ili aonekane anafaa kwa ndoa baada ya ndoa ndo unaona true colors
 
Ni kwa sababu yote yanayohusu ndoa mnayafanya kabla ya ndoa.. na hata mnadiriki kuitana mume/mke...
 
tatizo ni uvumilivu, wanawake kwa wanaume. kizazi hiki kimekosa uvumilivu kabisa. pili hatuna hofu ya Mungu, watu wanaigiza kuwa wanahofu ya Mungu ili hawana, na ndio maana siku izi hutashangaa anayejiita mpendwa nae anachepuka, au mchungaji ana kesi ya ubakaji.
 
tatizo ni kwamba mwanammke anakuwa hajajiandaa kutulia na mumewe..
hajajiandaa kuwa chini ya mume, mfano akitaka kwenda mahala inakua sio kama zamani anaenda tu lazima umuage mume na akubali
yani unakua chini ya mamlaka ya mume kwa kifupi
sasa na yeye hakuzoea hivo,hapo ndo ndoa inakovunjika anaona anabanwa

Na mume pia hivo hivo..
Na unakuta mume na yeye akishajua nna mamlaka na huyu mwanammke anaanza kufanya anavyotaka, atarudi muda anaotaka
atafanya anavyotaka
kwa sababu kalipa mahari (hasa wanaolipa mahari kubwa, si kashakununua/wewe nimali yake official)
pia kwenye ndoa mnaanza kuishi kwa mazoea sasa..
kwahiyo baadhi ya vijitabia vibaya vinaanza kujitokeza.

hapo ndipo mnapishindwana!
 
La msingi usipoteze fikra nyingi kwa wanawake,kwanza wao hawatupendi ila sisi tu hua hatujui,la muhimu penda na jali wanao tu,kuna mtu aliwahi andika humu nanukuu DO NOT LOVE WOMAN LOVE ONLY YOUR PRODUCT
Duuu watu MNA roho ngumu sana
Hayo maneno mnayatoaje kwa mwanamke unayelala nae uchi days/weeks,months n years?MPE heshima yake bana
 
tatizo ni uvumilivu, wanawake kwa wanaume. kizazi hiki kimekosa uvumilivu kabisa. pili hatuna hofu ya Mungu, watu wanaigiza kuwa wanahofu ya Mungu ili hawana, na ndio maana siku izi hutashangaa anayejiita mpendwa nae anachepuka, au mchungaji ana kesi ya ubakaji.
King'asti mswiti mwenyewe ndio huyu?
 
Siku hizi ndoa nyingi zinavunjika na nyingine migogoro haiishi, lakini siku tunapata muda wa kuwachunguza wenzi wetu kabla ya kuoana, je, tunakosea wapi, mbona zamani watu walioana hata hawajuani lakini ndoa zilidumu. Siku mtu anakaa uchumba miaka 5 lakini wakishaoana ndoa inavunjika tatizo ni nini?
Mapenzi ya siku hizi yapo ki digitali mno, heshima ya ndoa imepungua. Baadhi ya wanandoa hawana kbs hofu ya Mungu. Ukishaingia kwenye ndoa unatakiwa uwe unamshilikisha sn Mungu itasaidia.
 
Siku hizi ndoa nyingi zinavunjika na nyingine migogoro haiishi, lakini siku tunapata muda wa kuwachunguza wenzi wetu kabla ya kuoana, je, tunakosea wapi, mbona zamani watu walioana hata hawajuani lakini ndoa zilidumu. Siku mtu anakaa uchumba miaka 5 lakini wakishaoana ndoa inavunjika tatizo ni nini?
Chukua funzo hapa
Nina miaka 4 kwenye ndoa
Sujawahi laumu kuoa
Siri hii hapa
Alikuwa mchumba wangu kwa miaka 6 kabla ya ndoa
Nilikuwa naye tangu akiwa kidato cha 3 means nilicreat mambo nilikuwa nayataka kwake siku za usoni
Pia
Nilianza kwanza kuchunguza mamake anaishije na babake, wee unaenda kuoa Mtoto kacopy baba na mama hawajatulia wee unategemea Mtoto atatuliaje
Akikutana na magumu ni rahisi kusema mwachane tu
Lakini pia
Mimi pia naishi naye kwa uangalifu mkubwa kama vitabu vya mungu vinavyotaka
maana wanaume nao iko shida sana ubabe mwiiiingi, hatujitambui sema ndo hivyo, maisha yaende malalamiko kibao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom