Tunajifunza nini kutoka Ivory Coast?

Tunajifunza nini kutoka Ivory Coast?

Chini ni extract kutoka katika FB page ya Malisa JG

TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA IVORY COAST??

By Malisa GJ,

Huyu anayevutwa na Askari sio kibaka, sio mwizi, sio mfuasi wa chama cha upinzani ambao wengi wamezoea kuonewa bila sababu. Huyo ni Rais wa nchi. Ni Rais wa zamani wa Ivory Coast Ndg.Laurent Gbagbo.

Kitaaluma Gbagbo Mkemia, lakini kabla ya hapo alikua mwalimu wa shule ya sekondari. Alihitimu PhD yake ya Kemia mwaka 1979 kutoka chuo kikuu cha Paris Diderot University (Ufaransa).

Hakuwahi kufikiria kuwa Rais wa nchi hiyo licha ya kujaribu kugombea mara kadhaa. Alipata nafasi ya urais kibahati bahati baada ya kiongozi wa mapinduzi wa nchi hiyo Jenerali Robert Guéï kukata jina la mtangulizi wake Henri Konan Bédié, pamoja na jina la Waziri Mkuu wa zamani aliyekua anapewa nafasi kubwa ya kushinda Ndugu Alassane Ouattara.

Wakati Gbagbo akigombea Urais wa nchi hiyo alijipambanua kama mtetezi wa wanyonge, mpenda demokrasia, mtu anayeumizwa na matatizo ya watu maskini, na mpenda haki. Alijipambua kama mtu wa "KAZI" kwa ajili ya kuinua maisha ya watu maskini. Akajinasibu kujenga viwanda hasa vya Cocoa, kahawa na mafuta yanayochimbwa nchini humo.

Lakini alipoingia madarakani akaanza kukandamiza demokrasia, kubana vyama vya upinzani, kubana vyombo vya habari, kupandisha kodi hadi kwenye bidhaa zinazotegemewa na watu maskini. Akaanza kutoa upendeleo kwa watu wa familia yake na kuteua ndugu zake kushika nafasi za juu katika wizara na idara za serikali.

Akamkamata na kumuweka kizuizini Waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Ndugu Alassane Ouattara ambaye aliamua kujiunga na chama cha upinzani cha Republican (RDR) mwaka 1994. Akasahau kwamba wakati Ouattara akiwa Waziri Mkuu yeye alikua Mbunge tu ktk serikali Félix Houphouët-Boigny. Licha ya wafuasi wa chama chake kukamatwa bila sababu, Oattara hakuweka kinyongo. Bado alisalimiana na Gbagbo na kumheshimu kama Mkuu wa nchi.

Lakini Gbagbo akalewa madaraka. Akafikia hatua ya kuona kwamba yeye ndiye mtu pekee aliye sahihi katika nchi hiyo na maneno yake ni sheria. Akapuuza katiba ya nchi. Akaagiza kukamatwa kwa vijana wengi waliokua wafuasi wa vyama vya upinzani wanaomkosoa. Akapiga marufuku maandamano ya kisiasa.

Baadhi ya raia wa Ivory Coast wakalalamika kuwa Rais wao ameanza kuwa "Dikteta". Lakini kila aliyesikika akimuita Gbagbo dikteta aliishia korokoroni. Hatimaye Gbagbo akawa ndiye msemaji wa mwisho, mwenye nguvu na mamlaka juu ya mambo yote na kauli yake haitakiwi kupingwa wala kusahihishwa.

Ziara yake ya kwanza nje ya nchi alimtembelea Rais wa Burkina Fasso, swahiba wake Blaise Compaoré ambaye alikua na elements za udikteta. Compaore ndiye aliyemuua Thomas Sankara (the true son of Africa) na kujitangaza Rais mwaka 1987.

Kwahiyo Gbagbo aliporudi na kuanza kuongoza nchi yake kibabe, kukamata wanaomkosoa na kufungia vyombo vya habari, wananchi wakajua ni matokeo ya urafiki wake na dikteta Compaore.

Hali ya uchumi ya Ivory Coast ikazidi kudorora siku hadi siku. Watumishi wengi wa umma hawakulipwa mishahara yao kwa wakati, wawekezaji wengi wa kigeni wakafunga biashara, hakukua na nyongeza ya mishahara kwa watumishi lakini nyongeza ya kodi ilikua kwenye kila bidhaa na huduma.

Rais Gbagbo akapandisha ushuru/kodi katika Bandari ya Abidjan. Wafanyabiashara wengi wa nchi za Burkina Fasso na Mali wakaanza kupitisha mizigo yao kwenye bandari za Togo, Benin, na Liberia. Rais Gbagbo aliposhauriwa na wachumi juu ya athari ya maamuzi yake alikua mkali na kutishia kuwafukuza kazi waliomshauri. Alisema ni heri zije meli chache zenye kulipa kodi kubwa kuliko meli nyingi zenye kulipa kodi ndogo.

Hatimaye idadi ya meli zinazotua katika bandari ya Abidjan zikaanza kupungua kutoka meli zaidi ya 35 kwa mwezi hadi wastani wa meli 8 hadi 12 kwa mwezi (ingia hapa http://www.marinetraffic.com/…/a…/port:1150/portname:ABIDJAN). Pia mapato ya bandari yakaanza kupungua. Kilimo cha Cocoa ambalo ni zao kuu la biashara nchini humo kikaanza kuporomoka na uzalishaji wa mafuta ukaanza kupungua.

Uchumi ukazorota na hali ya maisha ikazidi kuwa ngumu. Rais Gbagbo akadhani watu wameficha pesa majumbani kwao, kumbe ni matokeo ya mfumo wa uchumi alioutengeneza mwenyewe.

Lakini wakati hayo yote yakiendelea, mamlaka ya mapato ya Ivory Coast (Cote' d’Ivoire General Direction of Taxes) ikawa inatangaza kukusanya mapato makubwa na kuvuka lengo kila mwezi. Wananchi wakajiuliza hayo mapato yanaenda wapi kama watumishi hawalipwi mishahara, huduma muhimu za jamii zimeongezwa kodi, madai ya watumishi hayafanyiwi kazi, miundombinu haijengwi, hospitalini hakuna madawa, benki zimesitisha mikopo, na Rais mwenyewe analalamika pesa haipo katika mzunguko. Je hayo makusanyo makubwa ya kodi yanatoka kwenye vyanzo vipi, na yanatumikaje mbona maisha yanazidi kuwa magumu?

Hatimaye mwaka 2010 wananchi wa Ivory Coast wakashindwa kuendelea kuvumilia shida, manyanyaso, ubabe, hali ngumu ya maisha, ukandamizaji wa demokrasia, na udikteta uchwara wa Rais Laurent Gbagbo. Kwenye uchaguzi mkuu wa November 28 mwaka 2010 wakamchagua Waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo (kipenzi cha watu, mtu asiye na visasi) Alassane Ouattara kwa asilimia 54.1% ya kura zote halali.

Tume HURU ya uchaguzi ya nchi hiyo, Ivorian Election Commission (CEI) ikamtangaza mgombea wa upinzani ndugu Ouattara kuwa mshindi wa kiti hicho cha Urais. Lakini Rais Gbagbo akakataa kuachia madaraka. Akajitangaza kuwa yeye ndiye mshindi na akadai kuwa amepata asilimia 51% ya kura zote halali.

Baada ya kujitangaza mshindi akatangaza pia kuivunja tume ya uchaguzi (CEI) na akatangaza kutotambua matokeo ya Tume hiyo. Pia akatoa amri kwa jeshi la nchi hiyo kufunga mipaka yote ya nchi (ya kuingia na kutoka) na akafukuza waandishi wote wa habari kutoka vyombo vya habari vya kimataifa waliokua wakiripoti uchaguzi huo. Akazifungia Radio na magazeti yote ya nchi hiyo yaliyotangaza kuwa ameshindwa uchaguzi.

Lakini wananchi wakaungana kupinga hatua hizo za kidikteta za Rais Gbagbo. Wakaaondoa tofauti zao za kidini, kikabila na kikanda kama ambavyo wamekuwa wakigawanywa na wanasiasa kwa muda mrefu. Wakaamua kuungana kwa pamoja kupinga maamuzi hayo. Wakristo ambao wengi wapo kusini mwa nchi hiyo na waislamu ambao wapo kaskazini wakaweka tofauti zao chini na kuungana kwa pamoja kupinga udikteta uchwara wa Rais Gbagbo.

Maandamano makubwa ya kumshinikiza Gbagbo kuachia ngazi yakafanyika katika mji mkuu wa Abidjan na kuzingira Ikulu yake. Japo mwanzoni Polisi waliuwa raia walioandamana lakini haiwakukatisha tamaa wengine kuingia barabarani. Hatimaye kufikia Aprili 10 mwaka 2011 Rais Gbagbo akawa amezingirwa na maelfu ya watu katika Ikulu yake. Watu wenye hasira ya uonevu aliowafanyia, watu wenye uchungu wa kuumizwa na kunyanyaswa, watu wenye kiu ya demokrasia.

Gbagbo akajua siku yake ya kiyama imefika, hofu ya mauti ikamvaa. Ikulu aliyoiona kama "paradiso" yake, ikageuka kuwa "bonde la uvuli wa la mauti". Akaomba msaada kwa walinzi wake wamtoroshe. Lakini walinzi wakashindwa kumtorosha kutokana na msongamano mkubwa wa wananchi waliozingira Ikulu.

Wananchi waliokua wamezingira Ikuku hiyo wakadai kuwa wanamtaka Gbagbo atolewe nje wamuadhibu kwa mikono yao wenyewe vinginevyo watachoma Ikulu hiyo afie ndani. Hatimaye serikali ya Ufaransa (mkoloni wa zamani wa Ivory Cost) ikatoa helcopter maalumu na makomandoo kadhaa kwenda kuepusha maafa ambayo yangeweza kutokea.

Makomandoo hao wakafika Ikulu ya Gbagbo na kumkuta amejificha uvunguni mwa kitanda kwenye handaki la chini kwenye ikulu hiyo akiwa na mkewe Simone Gbagbo. Wakamtoa na kuondoka nae. Wakamuepusha na "mauti" kutoka kwa raia wake.

Hatimaye Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo (kipenzi cha watu) Alassane Ouattara akatangazwa na kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo. Na Gbagbo akapandishwa kizimbani ICC ambako anakabiliwa na makosa ya uhalifu dhidi ya binadanu (crimes against humanity), ikiwa ni pamoja na mauaji ya wapinzani wake, ubakaji, vitisho/ubabe na ukiukwaji wa utawala wa sheria (murder, rape and persecution).

#Umejifunza_nini??

Malisa G.J

Ni vizuri tukajizuia kuandika makala ambazo hazina ukweli na zinapotosha maana. Binafsi sifahamu kivipi hali ya Ivory Coast unaweza kuilinganisha na hali yetu ya Tanzania. Pili tanzania hatujawahi kuwa na matatizo ya kikabila kama Ivory Coast. Tatu Malisa kabla ya kutuletea hii habari alitakiwa pia kutuambia historia ya huyu Rais Quattara. Lakini unategemea nini kutoka kwa kada wa chama kukueleza historia ya huyu rais wakati lengo lake ni kupotosha watu hasa akijua Watanzania wengi ni wavivu wa kufanya tafiti na wamejaa na mihemko ya kisiasa.

Ndugu Malisa alitakiwa kuwaeleza wasomaji wake wa FB yafuatayo
1. Quattara aliwekwa madarakani na waajiri wake IMF (alikua mwajiliwa wao)
2. Kwamba Quattara alitaka kukiuka katiba ya nchi na kujitangaza Rais pale rais wa kwanza wa
hiyo alipokua mgonjwa mwaka 1993 alijichukulia madaraka miezi 18 kinyume na katiba ya
Ivory Coast.
3. Kwamba Quattara alikua moja ya mawaziri katika serikali ya Félix Houphouët-Boigny alieyekua rais wa kwanza wa nchi hiyo, ambaye alikua kibaraka wa Ufaransa na alikua katika njama ya mauaji ya rais kipenzi wa waafrika na nchi ya Burkinfaso Captain Thomas Isidore Noël Sankara wakisaidiwa na Blaise Compaore waliyemuozesha mke kutoka Ivory Coast.

Kuna mengi nigeweza kuyaandika lakini nadhani kuna Mathinkers wengi hapa watanisaidia. Najua hali ya uchumi wetu siyo nzuri lakini ifike wakati tuwe makini sana na kuandika uongo zaidi ya ukweli. Hali ya Uchumi inayoendelea sasa hivi Tanzania si ngeni, maana imezikumbua nchi nyingi duniani hata zile kubwa kuzidi yetu. UK, Ireland, Greece kutaja baadhi. Zote zimepita katika hii hali tunayopita sisi. Nichukue mfano wa UK serikali ya Conservative ilipoingia madarakani mwaka 2010 waliingia na measures kama hizi zinazochukuliwa na serikali ya wamu ya tano,maana hakuna njia ya mkato. social services zililimwa vilivyo hata mafao ya walemavu pia yalikatwa. Maandamano mitaani ilikua kila kukicha lakini haikuletwa na wanasiasa japo baadhi waliungana na wananchi. Greece usiseme huko ndiko kulikua hatari zaidi lakini sikuona wanasiasa wakipambana kwa maneno na vijembe badala ya hoja. Hapa kwetu naona ni tofauti baada ya kusaidiana wanasiasa wetu wanakomeshana, na hii inaonesha wazi hawapo kwaajili yetu japo sisi tunadhani wapo kwaajili yetu.

Mwisho japo kuna hali ngumu ya maisha sidhani kama nia ya serikali ni mbaya, nina imani kubwa sana na hii serikali kama tukiipa nafasi mwanga upo mbeleni. Ila labda ushauri wangu kwa serikali ni kujaribu kuwa karibu na upinzani maana migongano yao ianweza kuchangia kuleta hali mbaya nchini hasa ukizingitia kuwa machafuko ktk nchi yeyote ile ni neema ya wengine.

Karibu tuchangie mada ya Malisa GS
 
Duuuh dr Ndalichako vilaza bado wengi huku mjini
 
Hakika Malisa kaonekana ana akili ila wewe huna akili..mana katoa mtazamo wake ambao wewe unaita uchochezi
 
Huyu ni muendelezo wa wale vibendera ,
Tulisha waambia awamu hii watumie akili kufanya siasa.
Siasa za Kufuata mkumbo,kuropoka na kutafuta kick mwisho ilikuwa 2015.
 
Hakika Malisa kaonekana ana akili ila wewe huna akili..mana katoa mtazamo wake ambao wewe unaita uchochezi
Sijasema hana akili ila wewe ndiyo umeamua kutukana. Ndiyo maana nimeandika mwishoni ma Great thinker wanisaidie sikumaanisha wewe.
 
Wakusaidie kwa huu ujinga ulioandika?
Labda hii itakusaidia....
In April 1990, the IMF under the Structural Adjustment Program forced the Ivorian President to accept Ouattara as Chairman of the Inter-ministerial Committee for Coordination of the Stabilization and Economic Recovery Programme of Côte d'Ivoire. While holding that position, Ouattara also remained in his post as BCEAO Governor. He subsequently became Prime Minister of Côte d'Ivoire on 7 November 1990 still under the IMF imposition,[3][9] after which Charles Konan Banny replaced him as Interim BCEAO Governor.[9]

While serving as Prime Minister, Ouattara also tried, illegally and against the constitution, to carry out presidential duties for a total of 18 months, including the period from March to December 1993, when Houphouët-Boigny was ill.[10] Houphouët-Boigny died on 7 December 1993, and Ouattara announced his death to the nation, saying that "Côte d'Ivoire is orphaned".[11][12] A brief power struggle ensued between Ouattara and Henri Konan Bédié, the President of the National Assembly, over the presidential succession in total disregard for the constitution that clearly gave Bedié the legal right to lead the country if Houphouet became unfit. Bédié prevailed and Ouattara resigned as Prime Minister on 9 December.[13] Ouattara then returned to the IMF as Deputy Managing Director, holding that post from 1 July 1994,[2][3] to 31 July 1999.[3]
 
Unaweza kuuita ujinga kwa uelewa wako, na unahaki ya kuuona ujinga sababu zaidi ya kusoma nini Malisa kaandika sidhani kama unajua lolote kuhusu hiyo nchi.
Wewe unaishi Ivory Coast? Maana umenambia hudhani kama najua lolote kuhusu hiyo nchi?
 
Godlisten Malisa ameajiriwa na hii NGO Jhpiego-Tz ambayo mwaka huu iligundulika kuwa inajishughulisha na "KUWAHUDUMIA" mashoga
Hilo silijui ila tatizo lake Malisa kajikita upande moja zaidi hajatueleza Quattara ni nani na alianzia wapi na nini kilimpeleka Ivory Coast kuacha ajira yake ya IMF. Kumchambua Ggabgo kama mkemia na rais halafu kutueleza tujifunze nini ni upotoshaji tu.
 
Labda hii itakusaidia....
In April 1990, the IMF under the Structural Adjustment Program forced the Ivorian President to accept Ouattara as Chairman of the Inter-ministerial Committee for Coordination of the Stabilization and Economic Recovery Programme of Côte d'Ivoire. While holding that position, Ouattara also remained in his post as BCEAO Governor. He subsequently became Prime Minister of Côte d'Ivoire on 7 November 1990 still under the IMF imposition,[3][9] after which Charles Konan Banny replaced him as Interim BCEAO Governor.[9]

While serving as Prime Minister, Ouattara also tried, illegally and against the constitution, to carry out presidential duties for a total of 18 months, including the period from March to December 1993, when Houphouët-Boigny was ill.[10] Houphouët-Boigny died on 7 December 1993, and Ouattara announced his death to the nation, saying that "Côte d'Ivoire is orphaned".[11][12] A brief power struggle ensued between Ouattara and Henri Konan Bédié, the President of the National Assembly, over the presidential succession in total disregard for the constitution that clearly gave Bedié the legal right to lead the country if Houphouet became unfit. Bédié prevailed and Ouattara resigned as Prime Minister on 9 December.[13] Ouattara then returned to the IMF as Deputy Managing Director, holding that post from 1 July 1994,[2][3] to 31 July 1999.[3]
Kwa kuniletea hichi toka Google ndo unadhani kitanisaidia kumwona Gbagbo ni bora kuliko Outarra?
 
Wewe unaishi Ivory Coast? Maana umenambia hudhani kama najua lolote kuhusu hiyo nchi?
Ama
hajui lolote au anataka kutudanganya. Alichokiandika siyo uongo bali ukitaka kutuletea habari unatakiwa kutuletea habari kamili. Mimi siishi huko na wala siyo raia wa huko lakini ninaishi na wa Ivory Coast hata mimi nilikua na mawazo kama ya Malisa kabla sijaonana nao. Na ilinichukua muda mwingi maana zaidi niliamini media. Lakini baada ya kujadiliana na wahusika na kufanya tafiti zangu mwenyewe nikaja kujua kuwa siyo kila tunachoonyeshwa katika TV ni ukweli. Mfano mzuri ni pale mataifa yote ulaya yalipokua yanamwita Mugabe ni Dikteta. Mugabe alishaua watu wa kabila la Ndebere kule Zimbabwe na bado waingereza walimpatia Knighthood lakini hakuna taarifa yoyote ile ilipatikana ya huyu Mugabe kuitwa Dikteta mpaka pale alipoingilia interest zao mwaka 2000 alipowanyang'anya wazungu mashamba ndipo tuliambiwa kuwa Mugabe ni Dikteta. Sasa wakati mwingine inabidi tujiulize kwani wale wandebele hawakua binadamu?
angalia nini huyu Quattara alipoanzia hapa chini nitakuwekea. extract

In April 1990, the IMF under the Structural Adjustment Program forced the Ivorian President to accept Ouattara as Chairman of the Inter-ministerial Committee for Coordination of the Stabilization and Economic Recovery Programme of Côte d'Ivoire. While holding that position, Ouattara also remained in his post as BCEAO Governor. He subsequently became Prime Minister of Côte d'Ivoire on 7 November 1990 still under the IMF imposition,[3][9] after which Charles Konan Banny replaced him as Interim BCEAO Governor.[9]

While serving as Prime Minister, Ouattara also tried, illegally and against the constitution, to carry out presidential duties for a total of 18 months, including the period from March to December 1993, when Houphouët-Boigny was ill.[10] Houphouët-Boigny died on 7 December 1993, and Ouattara announced his death to the nation, saying that "Côte d'Ivoire is orphaned".[11][12] A brief power struggle ensued between Ouattara and Henri Konan Bédié, the President of the National Assembly, over the presidential succession in total disregard for the constitution that clearly gave Bedié the legal right to lead the country if Houphouet became unfit. Bédié prevailed and Ouattara resigned as Prime Minister on 9 December.[13] Ouattara then returned to the IMF as Deputy Managing Director, holding that post from 1 July 1994,[2][3] to 31 July 1999.[3]
 
Hilo silijui ila tatizo lake Malisa kajikita upande moja zaidi hajatueleza Quattara ni nani na alianzia wapi na nini kilimpeleka Ivory Coast kuacha ajira yake ya IMF. Kumchambua Ggabgo kama mkemia na rais halafu kutueleza tujifunze nini ni upotoshaji tu.
Kumfurahisha Magufuli inabidi mjitoe akili kweli
 
hajui lolote ama nataka kutudanganya. Alichokiandika siyo uongo bali ukitaka kutuletea habari unatakiwa ktuletea habari kamili. Mimi siishi huko na wala siyo raia wa huko lakini ninaisha na wa Ivory Coast hata mimi nilikua na mawazo kama ya Malisa kabla sijaonana nao. Na ilinichukua muda mwingi maana zaidi niliamini media. Lakini baada ya kujadiliana na wahusika na kufanya tafiti zangu mwenyewe nikaja kujua kuwa siyo tunachoonyeshwa katika TV ni ukweli kama hapa chini nitakuwekea extract

In April 1990, the IMF under the Structural Adjustment Program forced the Ivorian President to accept Ouattara as Chairman of the Inter-ministerial Committee for Coordination of the Stabilization and Economic Recovery Programme of Côte d'Ivoire. While holding that position, Ouattara also remained in his post as BCEAO Governor. He subsequently became Prime Minister of Côte d'Ivoire on 7 November 1990 still under the IMF imposition,[3][9] after which Charles Konan Banny replaced him as Interim BCEAO Governor.[9]

While serving as Prime Minister, Ouattara also tried, illegally and against the constitution, to carry out presidential duties for a total of 18 months, including the period from March to December 1993, when Houphouët-Boigny was ill.[10] Houphouët-Boigny died on 7 December 1993, and Ouattara announced his death to the nation, saying that "Côte d'Ivoire is orphaned".[11][12] A brief power struggle ensued between Ouattara and Henri Konan Bédié, the President of the National Assembly, over the presidential succession in total disregard for the constitution that clearly gave Bedié the legal right to lead the country if Houphouet became unfit. Bédié prevailed and Ouattara resigned as Prime Minister on 9 December.[13] Ouattara then returned to the IMF as Deputy Managing Director, holding that post from 1 July 1994,[2][3] to 31 July 1999.[3]
Ungekuwa na busara nawe ungekuja na uzi wako unaomhusu Ouattara na kuainisha vitu ambavyo wa Ivory Coast walimpinga? Na ungesema ni kwanini wa Ivory Coast walimchoka na kumtaka Gbagbo ang'atuke na kwa mtazamo wako unadhani walikuwa sawa kufanya hivyo au wangeendelea kuvumilia?
 
Braza acha kubishana na wasomi vilaza , wasio penda kufanya research , kazi yao kupokea pasina kufanya upembuzi yakinifu, hakika hii ni hatari kwa taifa letu.
 
Ungekuwa na busara nawe ungekuja na uzi wako unaomhusu Ouattara na kuainisha vitu ambavyo wa Ivory Coast walimpinga? Na ungesema ni kwanini wa Ivory Coast walimchoka na kumtaka Gbagbo ang'atuke na kwa mtazamo wako unadhani walikuwa sawa kufanya hivyo au wangeendelea kuvumilia?
Lengo si kuleta uzi kuanisha bali ni kuweka sawa nini Malisa kaandika. Ndiyo maana unachangia maana kuna maana umeona na kila unapocomment unapata elimu zaidi.
 
Back
Top Bottom