Tunajifunza nini kutoka Ivory Coast?

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
18,885
2,000
By Malisa GJ,
Huyu anayevutwa na Askari sio kibaka, sio mwizi, sio mfuasi wa chama cha upinzani ambao wengi wamezoea kuonewa bila sababu. Huyo ni Rais wa nchi. Ni Rais wa zamani wa Ivory Coast Ndg.Laurent Gbagbo.

Kitaaluma Gbagbo Mkemia, lakini kabla ya hapo alikua mwalimu wa shule ya sekondari. Alihitimu PhD yake ya Kemia mwaka 1979 kutoka chuo kikuu cha Paris Diderot University (Ufaransa).

Hakuwahi kufikiria kuwa Rais wa nchi hiyo licha ya kujaribu kugombea mara kadhaa. Alipata nafasi ya urais kibahati bahati baada ya kiongozi wa mapinduzi wa nchi hiyo Jenerali Robert Guéï kukata jina la mtangulizi wake Henri Konan Bédié, pamoja na jina la Waziri Mkuu wa zamani aliyekua anapewa nafasi kubwa ya kushinda Ndugu Alassane Ouattara.

Wakati Gbagbo akigombea Urais wa nchi hiyo alijipambanua kama mtetezi wa wanyonge, mpenda demokrasia, mtu anayeumizwa na matatizo ya watu maskini, na mpenda haki. Alijipambua kama mtu wa "KAZI" kwa ajili ya kuinua maisha ya watu maskini. Akajinasibu kujenga viwanda hasa vya Cocoa, kahawa na mafuta yanayochimbwa nchini humo.

Lakini alipoingia madarakani akaanza kukandamiza demokrasia, kubana vyama vya upinzani, kubana vyombo vya habari, kupandisha kodi hadi kwenye bidhaa zinazotegemewa na watu maskini. Akaanza kutoa upendeleo kwa watu wa familia yake na kuteua ndugu zake kushika nafasi za juu katika wizara na idara za serikali.

Akamkamata na kumuweka kizuizini Waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Ndugu Alassane Ouattara ambaye aliamua kujiunga na chama cha upinzani cha Republican (RDR) mwaka 1994. Akasahau kwamba wakati Ouattara akiwa Waziri Mkuu yeye alikua Mbunge tu ktk serikali Félix Houphouët-Boigny. Licha ya wafuasi wa chama chake kukamatwa bila sababu, Oattara hakuweka kinyongo. Bado alisalimiana na Gbagbo na kumheshimu kama Mkuu wa nchi.

Lakini Gbagbo akalewa madaraka. Akafikia hatua ya kuona kwamba yeye ndiye mtu pekee aliye sahihi katika nchi hiyo na maneno yake ni sheria.

Akapuuza katiba ya nchi. Akaagiza kukamatwa kwa vijana wengi waliokua wafuasi wa vyama vya upinzani wanaomkosoa. Akapiga marufuku maandamano ya kisiasa.

Baadhi ya raia wa Ivory Coast wakalalamika kuwa Rais wao ameanza kuwa "Dikteta". Lakini kila aliyesikika akimuita Gbagbo dikteta aliishia korokoroni. Hatimaye Gbagbo akawa ndiye msemaji wa mwisho, mwenye nguvu na mamlaka juu ya mambo yote na kauli yake haitakiwi kupingwa wala kusahihishwa.

Ziara yake ya kwanza nje ya nchi alimtembelea Rais wa Burkina Fasso, swahiba wake Blaise Compaoré ambaye alikua na elements za udikteta. Compaore ndiye aliyemuua Thomas Sankara (the true son of Africa) na kujitangaza Rais mwaka 1987.

Kwahiyo Gbagbo aliporudi na kuanza kuongoza nchi yake kibabe, kukamata wanaomkosoa na kufungia vyombo vya habari, wananchi wakajua ni matokeo ya urafiki wake na dikteta Compaore.

Hali ya uchumi ya Ivory Coast ikazidi kudorora siku hadi siku. Watumishi wengi wa umma hawakulipwa mishahara yao kwa wakati, wawekezaji wengi wa kigeni wakafunga biashara, hakukua na nyongeza ya mishahara kwa watumishi lakini nyongeza ya kodi ilikua kwenye kila bidhaa na huduma.

Rais Gbagbo akapandisha ushuru/kodi katika Bandari ya Abidjan. Wafanyabiashara wengi wa nchi za Burkina Fasso na Mali wakaanza kupitisha mizigo yao kwenye bandari za Togo, Benin, na Liberia. Rais Gbagbo aliposhauriwa na wachumi juu ya athari ya maamuzi yake alikua mkali na kutishia kuwafukuza kazi waliomshauri. Alisema ni heri zije meli chache zenye kulipa kodi kubwa kuliko meli nyingi zenye kulipa kodi ndogo.

Hatimaye idadi ya meli zinazotua katika bandari ya Abidjan zikaanza kupungua kutoka meli zaidi ya 35 kwa mwezi hadi wastani wa meli 8 hadi 12 kwa mwezi (ingia hapa Vessel ETA in ABIDJAN Port - Recent & Estimated Times of Arrival | AIS Marine Traffic

portname:ABIDJAN ). Pia mapato ya bandari yakaanza kupungua. Kilimo cha Cocoa ambalo ni zao kuu la biashara nchini humo kikaanza kuporomoka na uzalishaji wa mafuta ukaanza kupungua. Uchumi ukazorota na hali ya maisha ikazidi kuwa ngumu. Rais Gbagbo akadhani watu wameficha pesa majumbani kwao, kumbe ni matokeo ya mfumo wa uchumi alioutengeneza mwenyewe.

Lakini wakati hayo yote yakiendelea, mamlaka ya mapato ya Ivory Coast (Cote' d’Ivoire General Direction of Taxes) ikawa inatangaza kukusanya mapato makubwa na kuvuka lengo kila mwezi. Wananchi wakajiuliza hayo mapato yanaenda wapi kama watumishi hawalipwi mishahara, huduma muhimu za jamii zimeongezwa kodi, madai ya watumishi hayafanyiwi kazi, miundombinu haijengwi, hospitalini hakuna madawa, benki zimesitisha mikopo, na Rais mwenyewe analalamika pesa haipo katika mzunguko. Je hayo makusanyo makubwa ya kodi yanatoka kwenye vyanzo vipi, na yanatumikaje mbona maisha yanazidi kuwa magumu?

Hatimaye mwaka 2010 wananchi wa Ivory Coast wakashindwa kuendelea kuvumilia shida, manyanyaso, ubabe, hali ngumu ya maisha, ukandamizaji wa demokrasia, na udikteta uchwara wa Rais Laurent Gbagbo. Kwenye uchaguzi mkuu wa November 28 mwaka 2010 wakamchagua Waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo (kipenzi cha watu, mtu asiye na visasi) Alassane Ouattara kwa asilimia 54.1% ya kura zote halali.

Tume HURU ya uchaguzi ya nchi hiyo, Ivorian Election Commission (CEI) ikamtangaza mgombea wa upinzani ndugu Ouattara kuwa mshindi wa kiti hicho cha Urais. Lakini Rais Gbagbo akakataa kuachia madaraka. Akajitangaza kuwa yeye ndiye mshindi na akadai kuwa amepata asilimia 51% ya kura zote halali.
Baada ya kujitangaza mshindi akatangaza pia kuivunja tume ya uchaguzi (CEI) na akatangaza kutotambua matokeo ya Tume hiyo. Pia akatoa amri kwa jeshi la nchi hiyo kufunga mipaka yote ya nchi (ya kuingia na kutoka) na akafukuza waandishi wote wa habari kutoka vyombo vya habari vya kimataifa waliokua wakiripoti uchaguzi huo. Akazifungia Radio na magazeti yote ya nchi hiyo yaliyotangaza kuwa ameshindwa uchaguzi.

Lakini wananchi wakaungana kupinga hatua hizo za kidikteta za Rais Gbagbo. Wakaaondoa tofauti zao za kidini, kikabila na kikanda kama ambavyo wamekuwa wakigawanywa na wanasiasa kwa muda mrefu. Wakaamua kuungana kwa pamoja kupinga maamuzi hayo. Wakristo ambao wengi wapo kusini mwa nchi hiyo na waislamu ambao wapo kaskazini wakaweka tofauti zao chini na kuungana kwa pamoja kupinga udikteta uchwara wa Rais Gbagbo.

Maandamano makubwa ya kumshinikiza Gbagbo kuachia ngazi yakafanyika katika mji mkuu wa Abidjan na kuzingira Ikulu yake. Japo mwanzoni Polisi waliuwa raia walioandamana lakini haiwakukatisha tamaa wengine kuingia barabarani. Hatimaye kufikia Aprili 10 mwaka 2011 Rais Gbagbo akawa amezingirwa na maelfu ya watu katika Ikulu yake. Watu wenye hasira ya uonevu aliowafanyia, watu wenye uchungu wa kuumizwa na kunyanyaswa, watu wenye kiu ya demokrasia.

Gbagbo akajua siku yake ya kiyama imefika, hofu ya mauti ikamvaa. Ikulu aliyoiona kama "paradiso" yake, ikageuka kuwa "bonde la uvuli wa la mauti". Akaomba msaada kwa walinzi wake wamtoroshe. Lakini walinzi wakashindwa kumtorosha kutokana na msongamano mkubwa wa wananchi waliozingira Ikulu.

Wananchi waliokua wamezingira Ikuku hiyo wakadai kuwa wanamtaka Gbagbo atolewe nje wamuadhibu kwa mikono yao wenyewe vinginevyo watachoma Ikulu hiyo afie ndani. Hatimaye serikali ya Ufaransa (mkoloni wa zamani wa Ivory Cost) ikatoa helcopter maalumu na makomandoo kadhaa kwenda kuepusha maafa ambayo yangeweza kutokea.

Makomandoo hao wakafika Ikulu ya Gbagbo na kumkuta amejificha uvunguni mwa kitanda kwenye handaki la chini kwenye ikulu hiyo akiwa na mkewe Simone Gbagbo. Wakamtoa na kuondoka nae. Wakamuepusha na "mauti" kutoka kwa raia wake.

Hatimaye Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo (kipenzi cha watu) Alassane Ouattara akatangazwa na kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo. Na Gbagbo akapandishwa kizimbani ICC ambako anakabiliwa na makosa ya uhalifu dhidi ya binadanu (crimes against humanity), ikiwa ni pamoja na mauaji ya wapinzani wake, ubakaji, vitisho/ubabe na ukiukwaji wa utawala wa sheria (murder, rape and persecution).

# Umejifunza_nini ??
Malisa G.J
1473163614082.jpg
 

kipuyo

JF-Expert Member
Jul 30, 2009
1,611
2,000
Kumbuka kabla ya uchaguzi huo,kulikuwa na serikali ya umoja wa kitaifa kati yake na aliyekuwa waziri mkuu wake ambaye anatokea kaskazini mwa nchi hiyo yenye wahamiaji wengi waislamu.

Kung'ang'ania kwake madaraka kumemgarimu lakini hakukuwa na muunganiko mkubwa wa raia wa dini zote.

Waliomuondoa Gbagbo ni waislamu wa kaskazini wakisaidiwa na wafaransa na ndo maana video nyingi zinawaonyesha wakipiga Takbiiir baada ya jamaa kuondolewa ikulu.

Kuna majeraha mengi hasa ya udini huko Ivory coast yanayohitaji tiba.

Kung'ang'ania madaraka ni kubaya lakini sioni cha kujifunza kwani kulikuwa na udini mwingi.
 

mbinde

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
786
1,000
Nguvu ya umma inahitajika kurudisha vilivyopotea, vilivyonyang'anywa,na kukomboa vinavyoonewa na kikundi cha wachache.
 

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
18,885
2,000
Hii chuki inayopandwa na wapinzani juu ya wananchi waichukie serikali yao na viongozi sio mzuri na inapaswa kukemewa.


Mfano mzuri wenye nyumba yenye upendo huanza na wazazi sasa ukiongea hivyo unakosea tuliombee taifa liwe na umoja visas vibaya huoneshwa na watawala alivyosema ningekuwa mm nisinge toa mkono wangu kusain sasa hiyo sio chuki?
 

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,910
2,000
Tunajifunza kwamba "hakuna nguvu yeyote itakayoshinda nguvu ya umma"
Comrade Malisa Godlisten ametoa somo kubwa sana kwa watawala ambao wapo madarakani wanajiona kila kitu wanaweza kufanya lazima watambue kuna siku nguvu ya umma ikiamua hakuna ambacho kitachoshindikana.

TIME WILL TELL.
 

Benny

JF-Expert Member
Jun 6, 2014
3,258
2,000
Chakujifunza ni kwamba

Ivory coast iliwachukua muda mrefu na vifo vingi mpaka kuapishwa kwa Ouattara
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom