Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 988
Mjadala wa katiba mpya unaendelea na unapata waelewaji wengi kadiri siku zinavyokwenda.
Lakini kadiri unavyoendelea ndivyo unavyodizi kufunika mambo mengine ambayo pia ni ya msingi na yanapaswa kushugulikiwa.
Ukizikagua kanuni kanuni za bunge utaona tunapiga kelele kila siku kulalamika madaraka makubwa ya rais.
Lakini tunasahau kumbe hata spika ana madaraka makubwa vilevile. Mbunge anaweza kufukuzwa kikaoni na ata kufungiwa kama ilivyotokea ka Zitto Kabwe na kama Samwel Sitta wakati fulani alimtoa nje John Cheyo.
Lakini hakuna kifungu hata komoja kinachoeleza kwamba spika anaweza kuwajibishwa akivunja kanuni.
Mtakumbuka bunge hili la Anne Makinda yametikea makosa kadhaa moja kwa moja yakimhusu Spika.
Wakati wa kugombea unaibu spika tunakumbuka CC na CHADEMA waliweka wagomea. Yule tuliemuita mpambanaji wa ufisadi Engineer Rozi Manyanya alileta swali kwa mgombea wa CHADEMA akiuliza Chama chama chake kimesema kutomtambua rais sasa anawezaje kuongoza bunge?
Tundu Lissu aliinua mkono na kufafanua swali hilo si sehemu yake kwani hoja iliyop si ya uchaguzi wa rais bali ni uchaguzi wa naibu spika. Anne makinda badala ya kukiri au kukataa alirukia na kusema "Na wewe hivyohivyo Tundu Lissu unaingilia mawazo ya mwenzio".
KIla aliyetazama aliona spika kachemsha kwani hata hakutaja mwongozo kama nilivyomnukuu. Ndipo mgombea wa CHADEMA akalazimishwa kujibu swali.
Wakat analijibu alisema "pamoja na kutengua kanuni" na wala hakufika mbali Spika akarukia na kusema "ondoa hiyo kauli, nani kavunja kanuni, ina maana mimi spika nimevunja kanuni?".
Huu ni mfano wa spika kuwa katika hali ya kutowajibishwa. Ukweli kanuni ilivunjwa.
Mfano mwingine ni pale Sofia Simba alipoteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya SADEC wakati hakuhojiwa kama wengine. Akina Zitto walikuja na kusisitiza bunge linatakiwa lifuate kanuni lakini haikufua dafu.
Hii yote ni kwa sababu kanuni zimemuweka spika kama vile yuko juu ya sheria.
Naamini spika atapenda tuendelee hivihivi tumsahau upande huu.
Kumbe huku nako kunahitaji kushughulikiwa. Tunaweza kujidhani kanuni hazituhusu lakini ukiachilia mbali ukweli kwamba kila mmoja ni mbunge mtarajiwa, bado hata sasa uwezekano wa mbunge kunyanyaswa na spika huku spika akijua wazi hakuna litakalomtokea.
Mnaionaje hii.