Tunahitaji shujaa mwingine kwa malipo ya kumaliza ubunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunahitaji shujaa mwingine kwa malipo ya kumaliza ubunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngekewa, Jun 16, 2011.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa vile harakati za kutaka kuondowa malipano yasiyokuwa na Mantiki zimeanza basi tuziendeleze. Wabunge wa CHADEMA kwa nia yoyote ile iwayo inabidi tuwashukuru kwa kutuletea mwanya wa kuweza kudadisi hii hali ya matabaka teule. HILI LA WABUNGE KULIPANA MAMILIONI YA SHILLINGI BAADA YA KIPINDI CHA MIAKA MITANO SI HAKI KABISA!

  Kwa mantiki gani hasa yanalipwa malipo haya wakati miaka mitano hiyo jamaa hawa wanachezea pesa tu . Mara vikao vya kamati, mara safari za nje kuhudhuria mabunge, ndio hivyo mshahara wao unazidia kinuamgongo cha mwalimu aliechezea chaki miaka 25 huku akilipwa mshahar kwa mwezi chini ya kipato cha juu mbali ya mshahara kwa mbunge.

  Tuwe wakweli kuwa wanasiasa wanatuchezea na hawako tayari kuona wananchi wenzao wanaishi angalau kwa matumaini. Kelele Bungeni eti Bajeti haimnufaishi mwananchi lakini huyu anaepiga kelele anahakikisha kuwa miaka mitano anachukua sh. 432 millioni peke yake kwa mshahara na ukijumisha na matumizi mengine kama usafiri na posho za vikao ,perdiem,safari za nje, kamati na visemina vya kiushikaji anaweza akatumia billioni moja kwa kipindi chake cha miaka5. Nafikiri hakuna investment nzuri hapa Tanzania kama siasa na ukiingia ubunge kuendelea na umasikini basi ni mgonjwa.
  NAFIKIRI UMEFIKA WAKATI WANANCHI NDIO WAAMUWE MBUNGE APEWE NINI NA SIO KAMA WANAVYOFANYA SASA ETI KAMATI FULANI INAKAA NA KUAMUWA MASILAHI YAO WENYEWE.
   
 2. m

  mubi JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  ccm ipo hapo kwa ajili ya kulindana ili kuwanyonya wanyonge . Wanyonge wakiamka ccm imekwisha. Mentality ya kulindana ndani ya ccm ndiyo inayoleta umaskini mkubwa Tz. Kiongozi yupo hapo kutumikia wananchi na siyo kuwaduwaza wananchi wasahau what they have and how to deserve it.
   
 3. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Mkuu, nilazima ufahamu wabunge wengi kuanzia wa chama tawala hadi wa upinzani wanependa kung'ang'ania madaraka ili waendelee kufaidika... Wale wote tunaowaona bungeni asilimia kubwa wapo pale kwa ajili ya maslahi yao binafsi... Na usisahau ya kwamba hela wanazopewa mwishoni ndo zinazowasaidia sana wakati wa campaign mkuu!
   
Loading...