Labda ungeanza kutuambia kiwango chako cha elimu kisha utuambie maana ya "academic qualification" katika soko la ajira.Hivi kwa nini wanapoguswa miungu wenu huwa mnatafuta kila fursa za kuhalalisha upuuzi wenu?
Kila position ya ajira/utumishi ina academic qualification zake,hata aliyefoji cheti cha Elimu anafahamu umuhimu wa Elimu,isipokuwa amekosa uwezo wa kiakili wa kumuwezesha kuifikia ngazi ya kielimu anayoitamani na ndiyo maana alikwapua cheti cha watu ili walau aonekane ana sifa.
Imeandikwa kuwa "utakula kwa jasho lako", kwa nini tunapohoji mtu anayetumia vyeti vya mtu mwingine kujipatia ridhiki/uongozi kwa njia haramu iwe nongwa?Sheria ichukue mkondo wake,kila mtu awe pale alipo kwa njia sahihi na si kwa mbeleko ya kufoji vyeti,kufunga watu viatu na kujipendekeza.
Acha kujitoa ufahamu,unawakumbuka maelfu ya vijana wa UDOM waliofukuzwa chuoni kwa kile tulichoambiwa hawakuwa na sifa stahiki?Kwa nini leo tuwaruhusu vihiyo kushika nyadhifa kwa vyeti vya kughushi.