Najiuliza kama kuna watu wameanza kuwa kama mimi; vyama vyote vya kisiasa vilivyopo nchini haviwezi kutupatia kile tunachohitaji kama taifa.
Siyo CCM, CHADEMA, CUF au TLP ambacho kilivyo sasa kinaweza kuwa tumaini la Watanzania.
Je, kuanzisha chama kingine ambacho kitatoka kwa wananchi na chenye ajenda ya mabadiliko ya kweli na kikiongozwa na watu wenye mwelekeo wa mabadiliko na wasioogopa political confrontation na ambacho hakitasita kufanya what is necessary to restore law and order and a constitutional rule kitaweza kuwa na nafasi.
Chama ambacho mrengo wake itakuwa ni kuhakikisha kuwa hakuna kurembuliana macho na mafisadi tena wala kuufafanua ufisadi bali kuushughulikia moja kwa moja.
Chama ambacho kitalenga kuleta mabadiliko ya kimfumo na kimuundo wa serikali yetu ndani ya miaka mitano ya kuingia madarakani kikibeba ajenda ya mabadiliko ya kweli (kikatiba, kisiasa, na kiutendaji) huku kikiwashughulikia kama simba mkali wale wote ambao wamelifikisha taifa letu hapa ikiwemo kutaifisha mali zao, kuwasweka jela na wale ambao ni vigogo wa ufisadi "kunyongwa" kama wanavyofanya huko China!
Chama ambacho hakitawabembeleza wawekezaji kama wakwe zetu!
Au ndiyo tubanane mumu kwa mumu huku tukiulizana "kajamba nani'!
Mimi binafsi nafikiri ss vyama tulivyonavyo vinatosha. Tuviimarishe hivi hivi na tusonge mbele.
Tunachopaswa kufanya ni kuruhusu mawazo na fikira huru kupenya kwenye bongo zetu na kufikiri kwa bidii huku tukiwa na picha kubwa vichwani mwetu juu ya Tanzania tunayoitaka na si vyama utitiri! Kusoma si kutoka mrango mmoja wa darasa na kuingia mwingine bali kuelimika na kujitambua. Hili la kujitambua kwa kweli Watanzania tulio wengi limetupita kushoto vilivyo ndo maana kila mara huwa najiuliza kuwa huwenda tumerogwa na aliyeturoga kesha fariki!! Hainiingii akili kuona wasomi wetu na hata wasio wasomi kujifanya wafalme ktk vyama wanavyo viongoza na wakati wakihanikiza kila kukicha CCM itoke madarakani kwa njia ya demokrasia.
Hii ni sawa na nyani kutoona kundule na utakuwa ni ujanja wa Mbuni kufunika kichwa mchangani ili mwindani asimwone ilihali mwili ute uko nje! Ni aibu kwa vyetu kutopanua demokrasia ili wananchi waweze kuona tofauti kati ya chama kilicho choka na chama kipya na chenye vijana wenye damu changa. Napenda kutoa ushauri ambao ni somo la karibuni kutoka Uganda kwa Kiiza Beseje aliachia chama kwa watu wengine ili waendeleze harakati na si kung'ang'ania tu bila kuonyesha mbinu mbadala za kushindana na chama twawala. Look guys Beseje leo hii hata akisimama jukwaani akawambia wananchi kuchagua chama chake tayari maneno yake na vitendo vyake vina mashiko. Tuje hapa kwetu tuchukulie mfano chama cha CUF. Hivi Mh. Lipumba kuna nn kingine nikiazima maneno ya marehemu bibi yangu alipenda kusema kwa kilugha (Tona ende ubisile heh). Maana yake huna jingine uliloficha. Kwa maana kwamba kama ni kwenye vita huna mbinu mpya ambayo kwayo hiyo ukiitumia basi mgomvi au adui yako ndo utakuwa mwisho wake.
Niambieni waJF kwamba kwa kuendelea kugombea kwa Mh.Lipumba kunaisadia CUF au ndo kunaendelea kuizika CUF? Je, leo hii ikitokea (simwombei) Mh. Lipumba amefariki ghafla ni nani amemwandaa kuwa mrithi wake asiye kuwa na shaka kushika nafasi hiyo na si peke yake na wanachama wote wakubaliane naye kwa kwa fulani aah hatuna shaka chama chetu kitaendele kuwa salama ni nani waJf niambieni!. Jibu ni hakuna the same na vyama vingine Bussines as usual kutahamaki 2015 CCM imerudi madarakani!!!!!!!!!!!!!!! Tutamsaka paka wa kuvisha kengere huyo! Tutaenda Sumbawanga kumtafuta mchawi tutaambiwa yuko Kigoma huko tutaenda hatutampata mchawi wetu na kumbe mchawi tunaye kwenye miguu yetu aibuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!
Mwisho napenda nisistize tena kuwa tuna muda wa kujisahihisha na kuerkebisha makosa yetu. Kuliondoa dude linalo itwa CCM si kazi ya kufanyia mzaha.
Ukicheka na CCM utavuna
1. Kung'olewa meno bila ganzi.
2. Watoto wako kusoma kwenye vituo vya kukulia watoto wao waviita shule.
3. Tembo kuisha Serengeti Na mbuga zote.
4. Kuuziwa sembe-(madawa ya kulevya) kwa maroli kama Azam anavyofanya.
5. Kama ww ni msanii kama Ray C basi Rais atakutibu ukiathirika.
6. Ukiiba uombe usikamatwe, ikishtukiwa tu unaambiwa urudishe kwa raha zako n.k.
Napita tu jamani mm mwenyewe mgeni nahurmia kucha na meno yangu!!!!! Magamba OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.