Siku zote wazo hutoka kwa mtu mmoja na kufanyiwa marekebisho na wengi! Wengi hawawezi kutoa wazo moja kwa wakati mmoja!
Kitila Mkumbo katoa wazo, kwamba tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA, katoa na hoja alizodhani zinatetea wazo lake, wengi tulimuunga mkono na wengi hawakumuunga mkono, wale tuliomuunga mkono naamini tulikubaliana naye na wale ambao hawakumuunga mkono hawakukubaliana naye!
Naamini, sasa ni wakati wa wale tuliokubalina naye kujitoa kwa ajili ya kuboresha wazo lake ili hata wale wanaomuona kwa mtazamo hasi basi waweze kuungana na sisi tuliokubaliana naye katika kuifikia Tanzania tuitakayo!
>Tunapokubali kuwa sasa tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA hatumaanishi kuwa tunahitaji chama chenye jina tofauti na CCM au CHADEMA! Bali tunamaanisha tunauhitaji wa chama cha siasa chenye kuwaza, kunena na kutenda tofauti na CCM na CHADEMA.
Sasa swali la msingi linakuja, je tutakipataje chama kitakachowaza, kunena na kutenda tofauti na CCM au CHADEMA?!
Binafsi nimepata majibu haya:-
1) Tunahitaji chama ambacho mtu binafsi au kikundi cha watu fulani hawatajiona kuwa wao wanachembechembe za umiliki wa hicho chama! Mfano, tunaamua kulifanyia kazi hili wazo na kufanikiwa kutengeneza chama mbadala, baada ya muda hatutapenda kumuona Dr. Kitila Mkumbo akijipa umiliki kisa tu eti yeye ndiye aliyetoa wazo! au kuona kikundi cha watu wakijipa umiliki kisa tu eti wao ndiyo waasisi wa chama! Tunahitaji kuunda chama ambacho kitakuwa mali halisi ya wanachama kidhahania na kialisia!
2) Tunahitaji chama kinakachoundwa kutokana na mawazo ya wanachama/watanzania. Vyama vingi vya kiafrika uundwa kuwa kuiga aidha kutoka vyama vikongwe (kama vilivyo vyama vyetu hapa Tanzania karibia vyote vimeundwa kwa kufuata muundo wa CCM) Au kutoka vyama vya mataifa yaliyoendelea. Chama hiki mbadala kinatakiwa kiundwe kutokana na mawazo ya wananchi, utafiti ufanyike, wananchi waulizwe na wajibu yao yafanyiwe kazi!
3) Misingi na Sera za chama mbadala, Vyama vingi vya kiafrika ni vizuri katika kuhubiri mapungufu ya chama pinzani kama chama na si kuhubiri madhaifu ya ya sera na misingi ya chama pinzani, lakini pia vyama hivi vya kiafrika ni vizuri katika kuhubiri shida za waafrika kuliko kuhubiri ni namna gani misingi na sera zao zitawanufaisha na kuwasaidia waafrika, Mfano, ".... CCM ni chama cha kifisadi kimeuza nchi yote ndio maana pamoja na utajiri wetu wote sisi bado ni maskini....... mkikichagua chama chetu tunapitia mikataba yote ya madini ili rasilimali zetu zitunufaishe sisi wenyewe....." kwa hotuba hii naamini wafuasi wako tu na wale walioichoka CCM ambao wako tayari kuiona CCM ikitoka madarakani bila kujali nani anaingia badala ya CCM ndio watakaokuunga mkono, lakini kwa jamii ya waelewa wataona kwa hali hii ni bora CCM iendelee kubaki madarakani tu! na kwa aina hii ya hotuba ndio maana hakuna mwananchi wa kawaida asiyejisumbua na kusoma anayejua misingi na sera za vyama vyetu! Tunahitaji chama mbadala kiwe na misingi na sera kwanza, zenye maneno machache na pili zenye kueleweka na tatu rahisi kuhubirika, Tutamani kiongozi wa chama mbadala atakaposimama jukwaani kuhutubia aseme "........Pamoja na utajiri tulionao, tunaendelea kuwa maskini kwa sababu ya sera na misingi inayosimamiwa na CCM, Msingi wa CCM unaegemea kwenye .......... na ndiyo maana sera zao za uchumi zinawafanya wafanye 1,2,3 mfano sera yao ya uchumi inasema ..........., hii sera ina madhaifu 1,2,3 na ndio maana hali hii iko hivi lakini mkitupa ridhaa sisi (chama mbadala) ambao msingi wetu umeegemea kwenye ........... hii inatufanya tuwe na sera 1,2,3 kutokana na hizi sera zetu ni lazima tukiingia madarakani tutafanya 1,2,3 na tukifanya haya wewe kama mtanzania wa kawaida utanufaika kwa ..........!
Kwa kifupi chama mbadala kiwe chama kitakachofanya mapinduzi katika siasa za kitanzania/kiafrika, kiwe chama cha kuwafanya watanzania kuchagua chama kutokana na uhitaji wa muda husika na si kuchagua chama ilimradi, kwamba kama uchumi umelegea legea basi watanzania tuchague chama chenye sera nzuri zaidi za uchumi, kama huduma za jamii zimelegea legea basi tubadilishe chama na kuchagua chenye sera nzuri zaidi za huduma za jamii au kama tutaona sasa ni wakati wa kuimalisha ulinzi na usalama basi chama chenye sera nzuri zaidi za ulinzi na usalama kipewe dola.