Wana jamii forums nimesoma kwenye gazeti la IPP la tarehe 6 July, na kuna maelezo kuwa Unesco wamekubali kuachia kilomita 200 za mraba katika mbuga ya Selous kwa ajili ya uchimbaji wa uranium, kinachonishangaza ni baadhi wa wahusika katika kujenga nchi hii kufurahia na kuona ni hatua ya kuongeza kipato kwa Taifa hili la Tanzania kwa mgao wa bilioni 8 dhidi ya bilioni 320 kwa mwaka, kweli hii ndiyo haki au ndiyo aliyeturoga ameshakufa, naomba maoni yenu wana Jamii.