Tunaendelea kutumia mali badala ya maarifa

X-bar

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
1,002
1,146
Hadhi ya mtu, jamii au taifa hutokana na vitu viwili tu; mali/rasilimali au akili/maarifa waliyonayo. Yaani utajiri hutokana na matumizi ya kimoja wapo kati ya vitu hivi au vyote viwili kwa pamoja na kinyume chake umaskini hutokana na ukosefu/upungufu wa hivyo.

Kwakuwa si rahisi sana kwa mtu, jamii au taifa kujaaliwa na vyote akili na maarifa kwa pamojja, ndipo swali linakuja kipi bora zaidi kati ya mali na akili. Imekubaliwa na watu wengi (fact) kwamba ni bora Zaidi kujaaliwa akili/maarifa kuliko mali/rasilimali. Hii ina maana kwamba mtu, jamii au taifa ikiwa wamekosa mali wanaweza kutumia maarifa waliyojaliwa kutengeneza mali, bali mali waliyojaaliwa nayo inaweza isiwe na manufaa kwao au kuangamia kabisa kwa kukosa maarifa ya matumizi au utunzaji wake.

Kwakuwa ni kweli kwamba Tanzania na nchi zingine za Africa zimejaaliwa rasilimali nyingi lakini bado ni maskini, basi hakuna ubishi kwamba umaskini huo unatokana na ukosefu wa maarifa. Rais wa awamu ya nne wa nchi yetu, JK, alipojibu “sijui” pale alilpoulizwa kwanini Tanzania ni maskini, hakutoa jibu hilo kwavile hajui kweli.

Bila shaka alikwepa “kujidhalilisha” endapo angesema “tumekosa maarifa” kwakuwa yeye kama rais ndiye msimamizi mkuu wa rasilimali za nchi na kwamba alipaswa kutumia maarifa kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa taifa na kuondoka na umaskini. Badala yake, Kikwete aliishia kupokea misaada ya kutoka kwa “mabeberu” kwa kubadishana na rasilimali za nchi. Hii inadhihirika pale aliposema “ukitaka kula vya wenzio (misaada), kubali na vyako kuliwa (rasilimali)”.

Kwa upande wake, Rais wa awamu ya tano, JPM, yuko tofauti sana na mtangulizi wake kuhusu hatma ya rasilimali za nchi na namna ya kuzitumia kuondokana na umaskini. Kwa mtazamo wa Magufuli, kwavile nchi ina rasilimali nyingi, kupokea misaada ya mabeberu ni kujidhalilisha. Huwa anasema hii nchi ni tajiri na ilipaswa iwe inatoa misaada kwa nchi zingine duniani.

Unaweza kushangaa kwanini deni la taifa limekua mara dufu katika utawala wake na bado anajigamba tunafanya miradi mikubwa ya ujenzi kwa pesa zetu za ndani. Ni dhahiri kwamba tofauti na Kikwete, anachokifanya Magufuli ni kutumia rasilimali za nchi kama dhamana kujipatia mikopo. Anaposema “kama taifa tajiri lazima tujitegemee” hii indo maana yake; wavile hatuna fedha, basi tutumie rasilimali tulizonazo kukopa ili tufanye maendeleo.

Mtazamo wa Rais Magufuli uko sahihi kabisa. Hata hivyo, hicho anachokifanya kinadhihirisha kuwa na yeye ameshindwa kupata maarifa sahihi kuweza “kuchakata” na kuendeleza rasilimali za nchi ili kuondokana umaskini anaochukia. Ukweli ni kwamba kuna hatari kubwa sana ya kutumia mali kama dhamana kujipatia mikopo kwa maana mikopo huambatana na riba na kushindwa kulipa mkopo kunaweza kupelekea hiyo mali kutwaliwa na mkopeshaji na hapa ndipo huja ule msemo wa “nchi imeuzwa”. Kuuzwa kwa nchi maana yake ni kutwaliwa kwa rasilimali iliyotumika kama dhamana ambazo ni sehemu ya ardhi ya nchi. Madhara yake ni kwamba nchi inagawanwa na jamii zingine tofauti na wazawa.

Kiufupi, Tanzania bado hatujapata kiongozi mwenye uwezo wa kujenga maarifa sahihi kuhusu hatma ya rasilimali zetu ili kuondokana na umasikini na utegemezi.
 
Back
Top Bottom