Tunachotaka kuona ni Rais Samia kuingia mtaa kwa mtaa Kijiji kwa Kijiji Katesh na siyo kufanya mkutano wa hadhara

dr namugari

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
9,410
15,994
Kesho imetolewa taarifa kuwa Rais Samia atakuwepo Kateshi kuwatembelea wahanga wa tukio la mafuriko na mimi pia nitakuwepo kwani mimi nimeoa pale Katesh

Sasa Basi tunataka Rrais aingiee mtaani moja kwa moja kuona athari za mafuriko hatutaki mkutano wa hadhara kesho, kwani watendaji wake wote wameshakuwepo huku na wengine wanazunguka na helkopter wasijue la kufanya

Sasa tunaomba acha mikutano ya hadhara ingia field ujionee mwenywee jinsi watu walivyo achwa bila makazi, wee ndio tegemeo letu.

Mimi mama mkwe wangu amekumbwa na tukio hilo na hana pahala pa kuishi na sasa nafanya utaratibu aje ajisitiri hapa kwangu huku nitategemee serikali itaangalia namna ya kuwapatia wakazi wale angalau mabati na vyakula kwa muda wa mwezi mzima wakati wanajipanga kuanza maisha mapya.

Pia soma > Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 63

Asante sana na karibu ktk wilaya yetu ya Hanang wilaya alikozaliwa Waziri Mkuu Mstaafu ndugu Fredrick Sumaye
 
Back
Top Bottom