Tunachagua viongozi kwa maslahi ya Taifa au maslahi ya vyama vya Siasa?

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
946
Habari wadau. Pole na majukumu ya kujenga taifa. Wananchi wa chini wanapambana vya kutosha kusogeza taifa letu mbele, nguvu kazi zao na jitihada hukwamishwa na sera duni za nchi, sheria duni za nchi, taasisi na serikali isio-lenga kumnasua mtanzania wa chini kwenye umaskini uliokithiri.

Hayo yote yanathababishwa na aina ya viongozi waliopo madarakani, viongozi watunga sheria na sera za nchi.

Ndio maana ya kuuliza swali hapo juu. Kwa mwenendo na mifumo ya vyama vya siasa nchini vinapendekeza wagombea watao-leta maslahi ndani ya chama, Yani wagombea wataongeza wingi wa viti bungeni na wingi wa walioshinda katika chaguzi. Hii dhana inasimamiwa na vyama vyote vya siasa nchini.

Tumekuwa tukichagua viongozi au wawakilishi wetu kwa kuangalia umaarufu wa mtu anaegombea bila kuzingatia uwezo wake katika nafasi za uongozi na chachu yake ya kutuletea maendeleo.

Jimbo la Tandahimba msanii Harmonize anataka kugombea ubunge endapo atapitishwa kwenye kura za maoni kupitia Chama tawala, akienda jimboni kwa wananchi basi msanii huyo kapita. Sio atapita kwa kwa kuzingatia elimu yake au weredi wake au uzoefu wake au udhoefu wake katika tasnia ya utawala bali kwa kuangalia umaarufu wake atakuwa amepita kwa style hiyo.

Aina ya viongozi kama hawa hawana tija kwenye maslahi ya kitaifa, uongozi hauhitaji umaarufu. Hauhitaji umaarufu ili uwe kiongozi.

Haya ni matokeo hasi ya katiba yetu, kwa kuweka viwango vya chini na duni haswa katiks upatikanaji wa wabunge kwamba mgombea akijua kusoma na kuandika tu, akijua kuongea Kiswahili na kiingereza anaweza gombea nafasi hii.

Hivi ni vigezo duni na dhaifu Sana. Sio kamati kuu za vyama vya siasa nchini hazitambui zinatambua lakini kwa sababu zina-angalia maslahi ya vyama vyao vya siasa ndio maana hupitisha watu wenye umaarufu bila kuzingatia elimu yake, weredi, udhoefu na uwajibikaji wa wa mtu.

Tukiwa kama wapiga kura na sisi tunahusika katika kupitisha viongozi kama hawa, maendeleo ya jamii zetu na taifa letu kiujumla hayaletwi na umaarufu wa mtu au kumchagua mtu mwenye jina maarufu nchini.

Kuna muda tunabaki wanyoshea viongozi wetu kwa kufanya maamuzi ya kipuuzi na ya sio na tija kitaifa, tunasahau kwanza na sisi wenyewe wapiga kura tuliowapigia kura. Maana bila sisi wasingekuwepo katika nafasi za uongozi walizopo Sasa.

Tusisahau mtaji wa wanasiasa ni ujinga wetu, tukijielewa sisi tunawaopigia kura hata wale tunaowapigia kura watajielewa na hata kamati zinazopitisha majina ya wagombea wa vyama husika watapitisha watu wenye uelewa na ambao watakuwa na sifa kuongoza na wakutuletea maendeleo chanya kijamii hadi kitaifa.

Ujinga wetu ndio msiba wetu, na msiba wetu tunajitakia wenyewe. Sasa vilio vya Nini?

Ipo wazi na ndio ukweli usiopingika bila wingi wa kura zetu Magufuli asingekuwa raisi au bila kura za wananchi wa jimbo lilipo wilayani Kongwa Job Ndugai asingekuwa mbunge na hata nyadhifa ya uspika asingepata. Na asingeweza lidhoofisha bunge Kama alivyolidhoofisha Sasa.
 
Mkuu Kama tungekuwa tunaangalia maslahi ya taifa letu Magufuli hakusitahili kuwa rais wa nchi hii.sifa hizo hana
 
Ungeeleza basi huyo Harmonize ana mapungufu gani au ndio bado kuna mawazo ya kwamba wanamuziki ni wahuni.

Nielewe utashi wako kwanza unahisi wasanii wetu na kwa elimu zao wakipewa hatamu za kuongoza watakuwa na faida ya kimaslahi ya kitaifa?? Watoe wasanii baadhi waliobahatika kufika chuo kikuu.
 
Back
Top Bottom