Tunabalehe, Tunapevuka...Tunakomaa.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunabalehe, Tunapevuka...Tunakomaa..

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Mar 24, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Pamoja na tofauti zetu na mvutano wa hoja tunazojenga kila siku, tunakoelekea ni kwema na kwenye tumaini.

  Ndiyo, bado hatujaweza kuwa na uwakilishi mzuri, lakini kwa udogo wetu, tunajifunza mengi na kuonyesha ni upeo gani mkubwa tulionao zaidi ya ule waliokuwa nao Babu na baba zetu.

  TUmejikusanya humu kutoka kila upande wa dunia. Tukiwa na mvuto wa Gandhi, Mandela, Churchill, Roosevelt, Nkrumah, Toure, Bandaranaike, Somoza, Lenin, Mao, Reagan, Gorbachev, Morales, Lula, Ghadafi, Seretse Khama, Kenyatta, Khomeini na kila mvuto, uwe ni wa kibepari, kijamaa, kijimaa, kikabaila hata leo kwenye soko huria.

  Sisi ni kizazi ambacho kitaiwezesha Tanzania iwe nchi yenye kufuata demokrasia ya kweli.

  Hebu angalia jinsi Kuhani na FMES, wanavyoweza kubanjuana makonzi kwenye hoja moja, kisha wakaelewana kwenye hoja nyingine.

  Angalia tulivyogawanyika katika suala hili la Mwakyembe, Dowans, Madili, Utu na haki, kila mmoja akifafanua upande wake na kuutetea.

  Nakumbuka majuzi ni Susuviri kama si Companero, aliyetoa mfano wa jinsi gani Marekani ilivyoundwa na watu waliokuwa na mtazamo tofauti, ambao walikata shauri wakae chini wakajadili, wakawa na midahalo na mwishowe, wakazalisha katiba moja ambayo inaiongoza nchi yao mpaka leo, miaka zaidi ya 200!

  Sisi ni fursa yetu, katika kizazi hiki, kutumia nafasi hii si kutengemana kwa kuwa hoja zetu zinapingana, bali ni kufungamana na kuheshimu uhuru wetu wa maoni, na kuidumisha Demokrasia inayoturuhusu kusikilizana na kubishana, huku tukinywa maji kwenye kisima kimoja na kukaa kwenye mkeka tukila chakula pamoja.

  Laiti, kama wanasiasa wetu, babu na Baba zetu wangekuwa an mwamko na moyo wa kuwa wazi wenye kukubali kukosoana, kujadiliana na kutafuta kitu muafaka kwa ajili ya vizazi vijavyo.

  Ni aibu kubwa sana, mpaka leo kuna makundi yanayoamini kuwa wao pekee ndio wenye kustahili kuiongoza Tanzania. hawa ni wale wenye kudai Tanzania ina wenyewe, kwamba hakuna mwingine kama wao, na wengine mkiamka kujitutumua kujitangaza, mtakandamizwa na kusahauliwa.

  Mwanafalsafa Socrates alisema "The Unexamined life is not worth living", je sisi nasi tukubali kupokea ya Wazazi wetu ambao mpaka leo wanalataa kufanya tathmini ya kweli ya walichofanya na hata kukiri pale walipokosea.

  Tunabalehe, Tunapevuka... Tunakomaa...

  Idumu Jamii Forum!
   
 2. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Rev,

  Tatizo linakuja pale tunavyosahau kwamba sisi wenyewe ndio tunaipa nguvu siasa. Siasa hajawahi kuwa juu ya mwanadamu, bali inabeba nguvu hiyo kwa kuwe mitizamo yetu ndivyo inavyoona hivyo.

  Tuendelee kuzinduka, lakini tusisubiri nguvu tupewe na viongozi wa siasa, nguvu inakuja pale wananchi wanapotambua mapungufu ya viongozi wao! halafu kinachofuata ni kufanya kwa matendo kuonyesha kutoridhika kwetu, maana Waswahili walisema, maneneo matupu hayafunji mfupa!

  Kwenye matendo ndio tunapocheza rumba!
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Mar 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishoka,
  Mkuu wangu ndio maana mimi hupenda kuwakilisha upande wa pili wa shilingi... ni mtazamo unaweza kuwa na maudhi ukawavuruga watu akili zao wengine wanatoka ktk mada kuwa personal lakini pamoja na yote haya huwa tunafikia mwisho mzuri.. Mwisho wenye picha mbili ambazo hata ikitokea kinyume cha mategemeo ya wengi bado tunaweza kusema tulifahamu hilo litatokea!..
  Msisitizo wangu ni kwamba tuendelee kushindana kwa hoja panapo uwekekano wa kinyume kutokea hivyo inaturahisishia wengi kuona mwanga na kuzisoma alama za nyakati..
  Tanzania yetu Usanii umezidi sana kiasi kwamba tunafikiri tunaweza kumhadaa hata Mwenyezi Mungu..
   
Loading...