Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,058
- 11,666
Mimi hata siwaelewi wakina Zitto. Pamekuwa na chaguzi kiasi toka ile ya 2020 na ACT wameshiriki kikamilifu. Kama sikosei ACT wameshinda moja tu tena kwa mbinde. Kuna chaguzi nyingine huku bara wamelalamika kufanyiwa ubabe ule ule wa 2020. Ya mwisho ndio hawakupata hata kura 200. Sasa ikiwa wanachezewa rafu katika nchi ambayo wao ni washiriki kwenye utawala nini kinawaamisha kuwa 2025 hali itakuwa tofauti? Labda kama wanategemea hisani.Wasi wasi wa ACT ni kuwa kuna uchaguzi wa serikali za mitaa 2024. ACT wanaamini watashinda chaguzi hizo. Hivi wakipata viti 5000 dhidi ya 40,000 kuna maana gani?
ACT wanaamini kuna uchaguzi 2025 na Tume huruikiwepo watashinda. Hivi wakishinda viti 50 vya ubunge dhidi ya 200 vya CCM wataleta mabadiliko gani? Hapo si ndipo watapiga mhuri kwa CCM kufanya mauza uza yao.
Kosa la ACT ni lile walilofanya Chadema mwaka 2010. JK alitangaza kuanzishwa mchakato wa katiba mpya. CDM wakasema Rais amefanya jambo jema na Wamefarijika. Tuliwaambi kuwa hiyo si njia sahihi, mchakato ulitakiwa uanzie Bungeni ili waweze kuuratibu
Matokeo yake mchakato ukawa mali ya 'Rais' na matokeo yake tunayajua
Hilo ndilo kosa la ACT kutaka Tume huru na Wajumbe wake wapatikane kwa mazingira ya sasa
Haraka ni ya nini ACT?
Ile chaguzi wala hawakushinda kwa kampeni, lile ni jimbo lao na walitishia kujitoa. CCM waliona isiwe tabu ili kuendelea kuudanganya ulimwengu jimbo moja si deal , wakawapaMimi hata siwaelewi wakina Zitto. Pamekuwa na chaguzi kiasi toka ile ya 2020 na ACT wameshiriki kikamilifu. Kama sikosei ACT wameshinda moja tu tena kwa mbinde.
Huku bara si kwamba wameshindwa tu, bali pia walipigwa sana. Hawajaambulia chochoteKuna chaguzi nyingine huku bara wamelalamika kufanyiwa ubabe ule ule wa 2020. Ya mwisho ndio hawakupata hata kura 200. Sasa ikiwa wanachezewa rafu katika nchi ambayo wao ni washiriki kwenye utawala nini kinawaamisha kuwa 2025 hali itakuwa tofauti? Labda kama wanategemea hisani.
Ni moja ya msingi mkubwa wa kuwa na katiba. Tunakumbuka Mwenyekiti wa NEC aliwahi kuchukua fomu za kugombea Urais kupitia CCM.Fatma Karume alitoa pendekezo zuri sana kuhusiana na cheo cha Spika. Kwa vile inaelekea Spika anajiona kuwa ni Rais mtarajiwa basi anaona ni muhimu ajipendekeze kwa mamlaka yenye nguvu ya kuteua mgombea urais. Fatma alishauri kuwa ili kuepukana na tamaa hizo, Katiba imzuie Spika kugombea nafasi yeyote ya kisiasa muhula wake utakapoisha. Hii itaondoa uwezekano wa kuwa corrupted kwa ahadi ya cheo cha kisiasa. Mimi nashauri iwe hivi kwa Jaji Mkuu, Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi na ile ya Vyama vya Siasa. Aidha, wasimamizi wote wa uchaguzi na wakuu wa vyombo vya usalama nao wasiruhusiwe kugombea kwenye chaguzi kuu mbili baada ya kutoka kwenye nafasi yao. Kwenye uspika, iwekwe wazi kuwa sio lazima kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na mara ukichaguliwa hauruhusiwi kushiriki katika shughuli zozote za kisiasa za chama chako ( hamna mambo ya kuwa mjumbe wa NEC n.k.). Mheshimiwa Rais anyang'anywe pia mamlaka ya kuwaondoa kwenye nafasi zao (kwa kuwapa kazi nyingine, kuwapandisha vyeo n.k) bila kutoa sababu inayoeleweka ambayo itakubaliwa na Tume itakayoundwa (kama Spika, tume iwe na maspika kutoka Jumuia ya Madola). Nadhani tukifanya hivi tutapata watumishi ambao wataweka taifa mbele na sio chama chao cha siasa.
Amandla...
Mimi nawashangaa sana ACT. Wamepigwa, Ado Shaibu na wenzake wameswekwa ndani lakini kimya. Wanaugulia tuu maumivu yao wakitumaini ushindi Zanzibar utawapa uongozi wa upinzani Bungeni.Ile chaguzi wala hawakushinda kwa kampeni, lile ni jimbo lao na walitishia kujitoa. CCM waliona isiwe tabu ili kuendelea kuudanganya ulimwengu jimbo moja si deal , wakawapa...
Kule Pemba kuna Polisi kawa demoted kwa kuruhusu mikutano ya ACT.Mimi nawashangaa sana ACT. Wamepigwa, Ado Shaibu na wenzake wameswekwa ndani lakini kimya. Wanaugulia tuu maumivu yao wakitumaini ushindi Zanzibar utawapa uongozi wa upinzani Bungeni...
TUNAANZA NA TUME HURU YA UCHAGUZI
Hoja ya ACT Wazalendo Juu ya Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya.
Utangulizi.
Tangu kurejeshwa upya kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, hoja ya kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi imetawala medani ya siasa nchini.
Tume ya Jaji Nyalali ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi iliweka bayana kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, ni lazima kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya.
Hoja hizi zimeendelea kutawala medani ya siasa katika miaka 30 ya uwepo wa siasa za Vyama vingi nchini.
Kikao cha Wadau wa Tasnia ya Siasa Dodoma: Ukurasa Mpya?
Utawala wa Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ulijipambanua bayana kuwa dhidi ya vyama vya upinzani. Wito wa viongozi wa upinzani wa kuwepo kwa muafaka wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa ulipuuzwa. Haki za vyama vya upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa uhuru iliangamizwa. Shughuli halali kama vile mikutano ya hadhara ziliharamishwa!
Katika mazingira hayo, ni dhahiri kuwa Kikao cha Wadau wa Siasa Tanzania Kujadili Hali ya Demokrasia Tanzania kilichofanyika Jijini Dodoma kati ya tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 kilikuwa mwanzo mpya uliokosekana katika miaka sita iliyopita!
Kikao hicho kilichowakutanisha viongozi waandamizi wa vyama vya siasa, Mawaziri wenye dhamana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jeshi la Polisi, Asasi za Kiraia na Viongozi wa Dini kilikuwa ni jukwaa muafaka la kutafakari tulipojikwaa kwenye chaguzi zilizopita, hasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 na kutafakari kwa pamoja mwelekeo unaopaswa kuchukuliwa na Taifa kurekebisha dosari hizo kwa maslahi mapana ya Taifa. Makosa hurekebishwa kwa watu kukutana, kuambiana ukweli na kuwa na utayari wa kubadilika!
Kwa Hali yetu, Nini Kianze? Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba Mpya?
Moja ya masuala ambayo yalijadiliwa kwa uwazi na kina kwenye Kikao cha Wadau wa Siasa cha Dodoma ni kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Baada ya kikao, masuala haya mawili, hasa kuhusu nini hasa kinapaswa kutangulia yamepata mjadala mkubwa.
Tunaanza na Tume Huru!
Kalenda ya Uchaguzi inaonesha kuwa mwaka 2024 kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na 2025 Uchaguzi Mkuu. Kwa maoni yetu, ACT Wazalendo tunaamini kuwa tunapaswa kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kisha Katiba Mpya. Sababu zetu zipo wazi;
1. Mchakato wa Katiba Mpya unahitaji kutungwa kwa Sheria Mpya ya kusimamia suala hilo kwa sababu Sheria iliyokuwepo imeshapitwa na muda. Kutokana na unyeti wa suala hilo, ACT Wazalendo tungefurahi jukumu hili nyeti, litekelezwe na Bunge lililochaguliwa Kidemokrasia na Wananchi tofauti na Bunge la sasa ambalo asilimia kubwa ya Wabunge wake ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hawakutokana na matakwa (will) ya Wananchi.
2. Kura ya maoni ya Katiba Mpya itasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Hatuna imani kuwa Tume ya Uchaguzi inaweza kusimamia zoezi hilo nyeti kwa weledi na haki. Tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itasimamia mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya. Tume hiyo ni lazima iundwe sasa.
3. Hata baada ya Katiba Mpya kupitishwa na Wananchi kwenye kura ya maoni, Katiba haitaanza kutumika mara moja. Kutakuwa na kipindi cha mpito kisichopungua Miaka minne. Katika kipindi hicho Sheria mbalimbali zitafanyiwa marekebisho ili kuendana na Katiba Mpya. Kipindi hicho cha mpito lazima tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025 na chaguzi ndogo zozote zitakazokuwa zinatokea kabla ya Katiba Mpya kuanza kutumika.
4. Iwapo kwa sababu zozote zile, Mchakato wa Katiba Mpya hautakamilika hadi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, Tume Huru itakayoundwa itaweza kusimamia chaguzi hizo kwa uhuru na haki.
Tume Itapatikanaje?
Tume ya Uchaguzi ni zao la Katiba na Sheria. ACT Wazalendo tunapendekeza kuandikwa upya kwa Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi. Tunapendekeza kuwa Tume Huru ya Uchaguzi iwe na uwezo wa kuajiri Wasimamizi wa Uchaguzi katika ngazi zote na kuondokana kabisa na Mfumo wa sasa wa makada wa Chama tawala kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi.
ACT Wazalendo tunapendekeza Mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba na ya Katiba Pendekezwa Kuhusu Tume ya Uchaguzi yachukuliwe kama yalivyo au na marekebisho kulingana na hali ya sasa. Msingi wa hoja hii ni ukweli kuwa maoni hayo yanatokana na maoni ya wananchi wenyewe.
Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi Wapatikanaje?
1. Sheria mpya ya Uchaguzi (National Elections Act 2022) iweke utaratibu kuwa Watanzania wanaotaka kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi waombe kazi kufuatia tangazo la wazi kwa umma.
2. Sheria mpya ya Uchaguzi ianzishe Kamati Maalum ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.
3. Kamati ya Uteuzi ifanye usaili (interview) kwa uwazi kwa waombaji wote na kuchuja majina ambayo yatapelekwa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi.
4. Mara baada ya wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kupatikana wataajiri Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye nafasi itatangazwa, kufanyiwa usaili wa wazi na kisha jina kupelekwa kwa Rais kuteua Mkurugenzi wa Uchaguzi.
5. Kamati ya Uteuzi wa Tume itamkwe kisheria kuongozwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kama Mwenyekiti, Jaji Mkuu wa Zanzibar kama Makamu wa Mwenyekiti, Wajumbe wawe ni Rais wa Tanganyika Law Society, Rais wa Zanzibar Law Society, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na kama hakuna Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni basi kutoka chombo kinachojumuisha Vyama vyenye Wabunge Bungeni, Mtu mmoja kutoka Asasi ya Kitaifa ya masuala ya Sheria na Haki za Binaadam Tanzania Bara na mtu mmoja kutoka asasi kama hiyo Tanzania Zanzibar. Kwa vyovyote vile angalau theluthi ya wajumbe wa Kamati ya Uteuzi lazima wawe Wanawake.
6. Kutakuwa na sifa maalum za Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha wanakuwa watu wenye weledi na hawaegemei upande wowote.
7. Baada ya kuteuliwa na Rais, Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume wataidhinishwa na Bunge kwa utaratibu utakaowekwa na Sheria ya Uchaguzi. Kisha watakula kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
Masuala haya, na mengine yatakayoonekana yanafaa kutokana na mashauriano ya wadau, yanaweza kujumuishwa kwenye Sheria Mpya ya Taifa ya Uchaguzi ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi.
Katiba Mpya Itapatikanaje?
Katiba Mpya ni jambo pana! Inahitaji kuwepo kwa muafaka wa kitaifa juu ya jambo hilo.
Jambo la kutia matumaini, mchakato wa Katiba Mpya ulikwishaanza. Tume ya kukusanya maoni ilikwishaundwa, maoni yalishakusanywa na kuwasilishwa kwenye Bunge la Katiba ambalo lilitoka na Katiba Pendekezwa. Changamoto pekee ni kuwa Katiba Pendekezwa haikutokana na maoni ya pande zote kwa sababu Wabunge wengi wa Upinzani walisusia upigaji kura.
Hivyo basi, Taifa litahitaji Katiba Pendekezwa kufanyiwa maboresho. Mchakato wa namna ya kuifanyia maboresho lazima uelezwe kwenye Sheria ya Mchakato wa Katiba Mpya itayoandikwa upya na Bunge. Bunge linaweza kuamua kuundwa kwa Kamati ya Wataalamu (Committee of Experts) ili kutafuta namna nyingine ya kumalizia mchakato bila kuligharimu Taifa.
Hitimisho.
Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ni chanda na pete, vinategemeana. Kwa mazingira yetu kama Taifa kwa sasa, kutangulia kupata Tume Huru ya Uchaguzi kunaweka mazingira mazuri ya kupatikana kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni na matakwa ya Wananchi.
Inatakiwa tushawishiwe kwa hoja Katiba ni ya wananchi sio ya wamiliki wa vyama vya siasa
Bila maridhiano hakuna Katiba mpya na wakushaiwishiwa ni CCM na si mwingine
Shida iliyopo ni Chama kimoja kuona kina haki ya kupata Katiba mpya kitu ambacho ni NDOTO , bila mtawala kuridhia ni ngumu na mtawala anatakiwa ashawishiwe kwa hoja vinginevyo utakuwa wimbo tu wa miaka na miaka
Hujaelewa Act wanataka tume huru ianze ili uchaguzi ujao uwe huru ILI UPINZANI UPATE VITI VINGI BUNGENI,
Maana si mnasemaga ccm huwa wanaiba, ila upinzani wanashindaga miaka yote
Huwezi kupitisha katiba unayoitaka kama huna watu
Sasa unadhani katiba unaipataje bila kuwa na number bungeni?.
Hiyo sheria tu ya kuanza mchakato unadhani nani anaitunga?
Kwa mujibu wa Katiba Tume Tuliyo nayo ni Huru[emoji123][emoji106]TUNAANZA NA TUME HURU YA UCHAGUZI
Hoja ya ACT Wazalendo Juu ya Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya.
Utangulizi.
Tangu kurejeshwa upya kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, hoja ya kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi imetawala medani ya siasa nchini.
Tume ya Jaji Nyalali ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi iliweka bayana kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, ni lazima kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya.
Hoja hizi zimeendelea kutawala medani ya siasa katika miaka 30 ya uwepo wa siasa za Vyama vingi nchini.
Kikao cha Wadau wa Tasnia ya Siasa Dodoma: Ukurasa Mpya?
Utawala wa Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ulijipambanua bayana kuwa dhidi ya vyama vya upinzani. Wito wa viongozi wa upinzani wa kuwepo kwa muafaka wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa ulipuuzwa. Haki za vyama vya upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa uhuru iliangamizwa. Shughuli halali kama vile mikutano ya hadhara ziliharamishwa!
Katika mazingira hayo, ni dhahiri kuwa Kikao cha Wadau wa Siasa Tanzania Kujadili Hali ya Demokrasia Tanzania kilichofanyika Jijini Dodoma kati ya tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 kilikuwa mwanzo mpya uliokosekana katika miaka sita iliyopita!
Kikao hicho kilichowakutanisha viongozi waandamizi wa vyama vya siasa, Mawaziri wenye dhamana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jeshi la Polisi, Asasi za Kiraia na Viongozi wa Dini kilikuwa ni jukwaa muafaka la kutafakari tulipojikwaa kwenye chaguzi zilizopita, hasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 na kutafakari kwa pamoja mwelekeo unaopaswa kuchukuliwa na Taifa kurekebisha dosari hizo kwa maslahi mapana ya Taifa. Makosa hurekebishwa kwa watu kukutana, kuambiana ukweli na kuwa na utayari wa kubadilika!
Kwa Hali yetu, Nini Kianze? Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba Mpya?
Moja ya masuala ambayo yalijadiliwa kwa uwazi na kina kwenye Kikao cha Wadau wa Siasa cha Dodoma ni kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Baada ya kikao, masuala haya mawili, hasa kuhusu nini hasa kinapaswa kutangulia yamepata mjadala mkubwa.
Tunaanza na Tume Huru!
Kalenda ya Uchaguzi inaonesha kuwa mwaka 2024 kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na 2025 Uchaguzi Mkuu. Kwa maoni yetu, ACT Wazalendo tunaamini kuwa tunapaswa kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kisha Katiba Mpya. Sababu zetu zipo wazi;
1. Mchakato wa Katiba Mpya unahitaji kutungwa kwa Sheria Mpya ya kusimamia suala hilo kwa sababu Sheria iliyokuwepo imeshapitwa na muda. Kutokana na unyeti wa suala hilo, ACT Wazalendo tungefurahi jukumu hili nyeti, litekelezwe na Bunge lililochaguliwa Kidemokrasia na Wananchi tofauti na Bunge la sasa ambalo asilimia kubwa ya Wabunge wake ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hawakutokana na matakwa (will) ya Wananchi.
2. Kura ya maoni ya Katiba Mpya itasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Hatuna imani kuwa Tume ya Uchaguzi inaweza kusimamia zoezi hilo nyeti kwa weledi na haki. Tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itasimamia mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya. Tume hiyo ni lazima iundwe sasa.
3. Hata baada ya Katiba Mpya kupitishwa na Wananchi kwenye kura ya maoni, Katiba haitaanza kutumika mara moja. Kutakuwa na kipindi cha mpito kisichopungua Miaka minne. Katika kipindi hicho Sheria mbalimbali zitafanyiwa marekebisho ili kuendana na Katiba Mpya. Kipindi hicho cha mpito lazima tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025 na chaguzi ndogo zozote zitakazokuwa zinatokea kabla ya Katiba Mpya kuanza kutumika.
4. Iwapo kwa sababu zozote zile, Mchakato wa Katiba Mpya hautakamilika hadi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, Tume Huru itakayoundwa itaweza kusimamia chaguzi hizo kwa uhuru na haki.
Tume Itapatikanaje?
Tume ya Uchaguzi ni zao la Katiba na Sheria. ACT Wazalendo tunapendekeza kuandikwa upya kwa Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi. Tunapendekeza kuwa Tume Huru ya Uchaguzi iwe na uwezo wa kuajiri Wasimamizi wa Uchaguzi katika ngazi zote na kuondokana kabisa na Mfumo wa sasa wa makada wa Chama tawala kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi.
ACT Wazalendo tunapendekeza Mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba na ya Katiba Pendekezwa Kuhusu Tume ya Uchaguzi yachukuliwe kama yalivyo au na marekebisho kulingana na hali ya sasa. Msingi wa hoja hii ni ukweli kuwa maoni hayo yanatokana na maoni ya wananchi wenyewe.
Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi Wapatikanaje?
1. Sheria mpya ya Uchaguzi (National Elections Act 2022) iweke utaratibu kuwa Watanzania wanaotaka kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi waombe kazi kufuatia tangazo la wazi kwa umma.
2. Sheria mpya ya Uchaguzi ianzishe Kamati Maalum ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.
3. Kamati ya Uteuzi ifanye usaili (interview) kwa uwazi kwa waombaji wote na kuchuja majina ambayo yatapelekwa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi.
4. Mara baada ya wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kupatikana wataajiri Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye nafasi itatangazwa, kufanyiwa usaili wa wazi na kisha jina kupelekwa kwa Rais kuteua Mkurugenzi wa Uchaguzi.
5. Kamati ya Uteuzi wa Tume itamkwe kisheria kuongozwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kama Mwenyekiti, Jaji Mkuu wa Zanzibar kama Makamu wa Mwenyekiti, Wajumbe wawe ni Rais wa Tanganyika Law Society, Rais wa Zanzibar Law Society, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na kama hakuna Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni basi kutoka chombo kinachojumuisha Vyama vyenye Wabunge Bungeni, Mtu mmoja kutoka Asasi ya Kitaifa ya masuala ya Sheria na Haki za Binaadam Tanzania Bara na mtu mmoja kutoka asasi kama hiyo Tanzania Zanzibar. Kwa vyovyote vile angalau theluthi ya wajumbe wa Kamati ya Uteuzi lazima wawe Wanawake.
6. Kutakuwa na sifa maalum za Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha wanakuwa watu wenye weledi na hawaegemei upande wowote.
7. Baada ya kuteuliwa na Rais, Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume wataidhinishwa na Bunge kwa utaratibu utakaowekwa na Sheria ya Uchaguzi. Kisha watakula kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
Masuala haya, na mengine yatakayoonekana yanafaa kutokana na mashauriano ya wadau, yanaweza kujumuishwa kwenye Sheria Mpya ya Taifa ya Uchaguzi ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi.
Katiba Mpya Itapatikanaje?
Katiba Mpya ni jambo pana! Inahitaji kuwepo kwa muafaka wa kitaifa juu ya jambo hilo.
Jambo la kutia matumaini, mchakato wa Katiba Mpya ulikwishaanza. Tume ya kukusanya maoni ilikwishaundwa, maoni yalishakusanywa na kuwasilishwa kwenye Bunge la Katiba ambalo lilitoka na Katiba Pendekezwa. Changamoto pekee ni kuwa Katiba Pendekezwa haikutokana na maoni ya pande zote kwa sababu Wabunge wengi wa Upinzani walisusia upigaji kura.
Hivyo basi, Taifa litahitaji Katiba Pendekezwa kufanyiwa maboresho. Mchakato wa namna ya kuifanyia maboresho lazima uelezwe kwenye Sheria ya Mchakato wa Katiba Mpya itayoandikwa upya na Bunge. Bunge linaweza kuamua kuundwa kwa Kamati ya Wataalamu (Committee of Experts) ili kutafuta namna nyingine ya kumalizia mchakato bila kuligharimu Taifa.
Hitimisho.
Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ni chanda na pete, vinategemeana. Kwa mazingira yetu kama Taifa kwa sasa, kutangulia kupata Tume Huru ya Uchaguzi kunaweka mazingira mazuri ya kupatikana kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni na matakwa ya Wananchi.
Act kwa Sasa wameshakaribishwa mezani (serikali ya nusu mkate huko Zenji) na wamejihakikishia ruzuku ya kudumu.Ile chaguzi wala hawakushinda kwa kampeni, lile ni jimbo lao na walitishia kujitoa. CCM waliona isiwe tabu ili kuendelea kuudanganya ulimwengu jimbo moja si deal ...
Nakubaliana nawe . Tatizo ni kwamba wanatumika kukwaza au wanatumika kama mpiniAct kwa Sasa wameshakaribishwa mezani (serikali ya nusu mkate huko Zenji) na wamejihakikishia ruzuku ya kudumu.
Kwa Sasa Zitto ameshapata ajira ya miaka 9 ndani ya kikosi kazi hivyo kelele zake zitapungua.
Kiufundi Act na Zitto wameshapata wanachokitaka
Inawezekana Wazenji wametulia kwa sababu kero za muungano zimepatiwa ufumbuzi.Kesho akija Rais mwingine utasikia kelele zinaanza tena,kwasasa wametulia kwasababu wanachotewa tu kutoka Hazina Dar es Salaam, hawahitaji kwenda kazini au kuvua, hakuna shida tena ya katiba mpya wala muungano! ni starehe kwenda mbele
Swali ni kuwa kero hizo zimepatiwa ufumbuzi kwanini imekuwa siri?Inawezekana Wazenji wametulia kwa sababu kero za muungano zimepatiwa ufumbuzi.